CHADEMA mmejipangaje na wabunge 19 wa viti maalumu kutorudi bungeni tena mwaka 2025/26?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
42,451
56,927
CHADEMA mna mkakati wowote wa kuwazuia wabunge wa viti maalumu waliopo bungeni wakati huu kutorudi bungeni wakati na baada ya uchaguzi wa mwaka 2025?

Mtawazuiaje ikiwa mtaona wao ndio wamepewa fursa ya kugombea na wanapeperusha bendera ya CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2025?

Mtawazuiaje ikiwa mtawaona wao ndio wabunge wa viti maalumu tena baada ya uchaguzi?
 
Uharo wako umeuhamisha kutoka kuishambulia HAMAS umekuja kuhara huku
 
Covid19 walikisaliti Chama katika kipindi kigumu sana sana na kama watarudishwa Bungeni basi nitaamini walisapotiwa all along IMANI yangu kwenye Chama nikipendacho ITATOWEKA.

Na nitaacha kuwa Mwanachama.
 
Huo ni upande mmoja, vipi wakiingizwa tena bungeni na spika ajaye kama walivyoingizwa na Ndugai??
 
Covid19 walikisaliti Chama katika kipindi kigumu sana sana na kama watarudishwa Bungeni basi nitaamini walisapotiwa all along IMANI yangu kwenye Chama nikipendacho ITATOWEKA.

Na nitaacha kuwa Mwanachama.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo hakina ubavu wa kuwakataa hawa wabunge wao.

Kwanza, kuna viashiria kila mahali kwamba wako bungeni kufuatia nia, mchakato, na baraka za chama.

Pili, itaibuka hoja tunapoelekea kwenye ngwe za uchaguzi mwakani, kwamba kama walipokelewa mapapa wa mafisadi kama akina Lowassa, Sumaye na Lazaro Nyalandu, wakasafishwa, wakasifiwa na kugombea, seuze akina Halima Mdee?

Hii hoja moja tu inatosha kutuliza hali ya hewa na kuleta mtangamano Chademani.

Isitoshe, mwenyekiti atadai, kama anavyodaigi kila mwaka, kwamba hii ni fursa ya pekee kuunganisha nguvu zote za peponi na motoni za wafuasi watiifu na wasaliti ili kuingia Ikulu kwa kishindo, au kama wao waitavyo - mafuriko!

Mwisho, siasa hainaga maadui wala marafiki wa kudumu. Ndiyo maana juzi Zitto Kamwe alikuwa Msisiemu, jana akatimkia Chadema, leo yuko siti ya mbele kabisa Eisitii, na, nani ajuaye, huenda kesho akapokelewa kwenye chama cha Republican Marekani!
 
Isitoshe, mwenyekiti atadai, kama anavyodaigi kila mwaka, kwamba hii ni fursa ya pekee kuunganisha nguvu zote (za wafuasi watiifu na wasaliti) ili kuingia Ikulu kwa kishindo, au kama wao waitavyo - mafuriko!
Dokta Slaa anarudi huyo tunakubali kwa asilimia 100 na ataingia Bungeni kwa Viti maalum vya Wazee wa CHADEMA.

Na tunataka Mwabukusi ili timu yetu ikamilike hao Covid19 waende CCM hawawezi mapambano makali walishafeli wakati wa mikiki mikiki ya Jiwe.
 
Inasemekana Mwabukusi ni mpinzani wa kweli, wakati Chadema yenyewe ni kivuli tu cha Sisiemu, hususan viongozi wa juu wanaojua kilichomo chunguni.
 
Safari hii Timu itakamilika tu Slaa ndani Mwabukusi ndani Mwanamapinduzi ndani.

Hatutaki Waogawaoga au wapenda Asali.
 
CDM wanacheka na Ruzuku zinazotokana na hao wabunge yaani wanajitekenya na kucheka wenyewe,Msigwa unajua utamu wa Ruzuku.
 
Dokta Slaa anarudi huyo tunakubali kwa asilimia 100 na ataingia Bungeni kwa Viti maalum vya Wazee wa CHADEMA.

Na tunataka Mwabukusi ili timu yetu ikamilike hao Covid19 waende CCM hawawezi mapambano makali walishafeli wakati wa mikiki mikiki ya Jiwe.
Hakuna viti maalum vya wazee bungeni, kuna viti maalum vya wanawake tu.

Umri ule Dr Slaa agombee ubunge amesahau nini?
 
CHADEMA mna mkakati wowote wa kuwazuia wabunge wa viti maalumu waliopo bungeni wakati huu kutorudi bungeni wakati na baada ya uchaguzi wa mwaka 2025?

Mtawazuiaje ikiwa mtaona wao ndio wamepewa fursa ya kugombea na wanapeperusha bendera ya CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2025?

Mtawazuiaje ikiwa mtawaona wao ndio wabunge wa viti maalumu tena baada ya uchaguzi?
Hao siyo wanachama wa Chadema. Huyo Rango mwenyewe anajua anawafuga kwa tiketi ya chama gani hapo mjengoni.
 
Umeuliza maswali muhimu sana mleta mada, lkn wasioona mbali wanakushambulia.

CCM inaweza kufanya chochote muda wowote na kupelekea haya unayoyahofia yakafanyika.
 
CDM wanacheka na Ruzuku zinazotokana na hao wabunge yaani wanajitekenya na kucheka wenyewe,Msigwa unajua utamu wa Ruzuku.
Usichangie jambo usilolijua,Ruzuku haitokani na wabunge wa viti maalumu bali kutokana na idadi ya kura za mgombea urais, na hata hao wabunge wa wamepata hizo nafasi kutokana na idadi ya kura za mgombea urais.
 
Back
Top Bottom