Kuna nini mpaka siku hizi ndugu hatutembeleani?

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,036
71,262
Hivi wakuu nanyie mnaona kama mimi au?

Mbona kama ile Tamaduni yetu ya kutembeleana haipo tena.

Unajua ile tunakua, ilikua unasikia..Likizo hii tunaenda kwa Shangazi..kwa Baba mdogo. Kwa Mjomba... Kwa Bibi ...n.k

Lakini siku hizi hii kitu haipo

Au Mitandao yakijamii imechukua nafasi...yaan ukiona picha ya Ba mdogo kapost, unalike, unakoment.. Imeishaaa hiyooo

Au ukiona status yake wasap... Imeishaaaaaaa hiyo. Ndio salamu, ndio kujuliana hali?.
 
Utandawazi ushaingia mtu aache kutafuta hela ahangaike kutembeleana zamani maisha yalikua rahisi, leo hii usipohangaika itakula kwako kila mtu anahangaika kivyake kimsingi haya ndio maisha magumu sasa, tulikua tunayaona ulaya sasa yako hapahapa kwetu.
 
Kwanza mtindo wa maisha umeongeza sana majukumu alafu teknolojia ndio ikaja kuharibu kabisaaaaaaa, siku hizi watu mnachat mnapigiana kila baada ya dakika 10. Kwahiyo habari zote kila mtu anazipata real time.

Kumbuka zamani ilikuwa njia ya mawasiliano ni barua na kama mnakaa mkoa mmoja hamuandikiani barua ndio ilikuwa mnajipanga mnatembeleana.
 
Naweza kusimama na hii komenti kwa kiasi fulani
Mkuu hata mimi hii naiwaza lkn daah naona bado haitoshi

Mf ,mimi binafsi kwa Hapa Dar nina Jamaa wengi mnoo wa Damu ,upande wa Mama na Mzee.

Lkn tunaishia kutizamana kwenye mitandao yakijamii tuu..

Daah hata kukaribishana hamnaa, wake/wapenzi wetu wanatuzalia watoto , hata kutembeleana kupeana pongezi hamna

Tena sisi wanaume ndo tumezidi...bora wanawake wanakumbukana aisee
 
Kwanza mtindo wa maisha umeongeza sana majukumu alafu teknolojia ndio ikaja kuharibu kabisaaaaaaa, siku hizi watu mnachat mnapigiana kila baada ya dakika 10. Kwahiyo habari zote kila mtu anazipata real time. Kumbuka zamani ilikuwa njia ya mawasiliano ni barua na kama mnakaa mkoa mmoja hamuandikiani barua ndio ilikuwa mnajipanga mnatembeleana
Nakubaliana nawewe mkuu.. Kwahiyo tupo kwenye njia sahihi??

Unajua siku hizi, Misiba na sherehe ndo kidogo inakutanisha watu

Na unaenda msiban, ndo unajua aliyekufa ni mtoto wa shangazi
 
wewe unasema kutembeleana kwa jinsi mfumo wa maisha unapoelekea hata mambo ya ndugu yataanza kuondoka

utajikuta watoto wako wanakujua wewe na mama yao na wao wenyewe basi

mimi naona ni mabadiliko tu ya mifumo ya maisha ni kama siku hizi sikukuu zilivyobadilika na kuwa kama siku za kawaida tu

leo hii mwanako hawezi kujua utamu wa Xmass/eid/pasaka ule tuliojua sisi enzi tukikuwa
 
Kwanza mtindo wa maisha umeongeza sana majukumu alafu teknolojia ndio ikaja kuharibu kabisaaaaaaa, siku hizi watu mnachat mnapigiana kila baada ya dakika 10. Kwahiyo habari zote kila mtu anazipata real time. Kumbuka zamani ilikuwa njia ya mawasiliano ni barua na kama mnakaa mkoa mmoja hamuandikiani barua ndio ilikuwa mnajipanga mnatembeleana
Nakubaliana nawewe mkuu.. Kwahiyo tupo kwenye njia sahihi?

Unajua siku hizi, Misiba na sherehe ndo kidogo inakutanisha watu.

Na unaenda msiban, ndo unajua aliyekufa ni mtoto wa shangazi
 
Utandawazi ushaingia mtu aache kutafuta hela ahangaike kutembeleana zamani maisha yalikua rahisi, leo hii usipohangaika itakula kwako kila mtu anahangaika kivyake kimsingi haya ndio maisha magumu sasa, tulikua tunayaona ulaya sasa yako hapahapa kwetu.
Haha Hela hela...alafu huwez amin, siku hizi kila mtu anapigania chake

Yale mambo ya, Namchukua mwanao akasomee kwangu, nitamsomesha ..hayapo
 
Back
Top Bottom