wasalaam wanaJF?
Nimekuwa mfatiliaji sana wa siasa za hapa nyumbani kwa mda mrefu,ila sijawahi shuhudia mh mwigulu akimkosea adabu mh zitto kabwe kama anavyofanya kwa katibu mkuu dr slaa,hawa watu vyeo vyao viko sawa ndani ya vyama vyao,zitto kabwe ni naibu katibu mkuu wa chadema na mh mwigulu nae ni naibu katibu mkuu wa ccm.
Katika mda tofauti watu hawa wamekuwa wakialikwa kwenye vipindi vya Tv kwa pamoja ila kuna mda mmoja nashindwe kutokea<mara nyingi watangazaji husingizi foleni,kuwa mgeni wetu kashindwa kuja sababu ya foleni,mfano,kuna siku star tv waliwaalika naibu katibu mkuu wa cuf mtatiro,naibu katibu mkuu wa chadema zitto,na naibu katibu mkuu wa ccm mwigulu ila mh zitto kabwe hakutokea na siku hyo mwigulu aliutangazia umma kuwa anao mkanda unaonyesha viongozi wa juu wa cdm wakupinga mauaji:
Nimekuwa nikiwaangalia hawa watu kwa jicho la3 mda mrefu sana,mh mwigulu kajikita sana kumshambulia dr slaa,vile vile mh zitto kabwe nae kajikita sana kwa waziri mkuu mh pinda mpk ilifikia hatu ya kukusanya sahihi za kutokuwa na imani na waziri mkuu,na sasa kaja na swala la mshahara wake,nikirudi upande wa mwigulu imefikia hatua mpk kaajiri vijana ambao wanatumia Id zaidi ya 4 kwa mtu mmoja ili kumdhalilisha dr slaa na mara chache mh mbowe,kuna mambo mengi sana hayako sawa na ukiyafatilia utagundua nachoongelea hapa,kwani kuna mambo mengi sana mabaya ambayo mh mwigulu kaifanyia cdm mpaka sasa lakini kamwe hutamsikia zito kayakemea pia upande wa zito kuna vitu vingi sana kaviibua kuhusiana viongozi wa ccm mfano fedha za uswiz and so on ila hutamsikia mwigulu kamsema zito kwa lolote kama alivyozoea kuwasema slaa na mbowe:
Swali la msingi: watu hawa kuna makubaliano yoyote waliyoyafanya ili kutunziana heshima? sina nia ya kuwachonganisha zitto na mwigulu bali wao ni public figures na matendo yao yanafatiliwa kwa ukaribu mkubwa na watu mbali mbali nje na ndani ya nchi yetu.
Ombi: tusijadili maisha yao binafsi bali kazi zao na harakati zao ndani ya vyama vyao