Kuna ndoa au mahusiano yenye raha siku zote pasipokuwa mikwaruzano?

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,713
1,263
Wadau Asalaam aleykumu/Bwana Yesu asifiwe sana.

Wadau naomba mchango wenu kwenye hili, kila atakayechangia awe kwenye mahusiano au ndoa.

Tangu umeanza mahusino, kuoa au kuolewa umewahi kukutana na machafuko? Je uliyatatua vipi? Nini kilichopelekea kuwa hivyo? Kila mtu atoe kisa cha ukweli kwa kufanya hivyo kuna wale ambao wanafikiri kwamba ndoa ni kula bata kila siku hakuna migongano wala mikwaruzo.

Asanteni kwa kuchangia.

Muwe na siku njema

CD
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mpenzi huwa watu wengi hawatoagi visa vya ukweli. Ila ngoja tusikilizie. Machafuko hayakosekani labda kama mmeanza mahusiano sahivi.
 
Machafuko yapo, lakini tumesimama kwenye neno kuwa 'he will not let you be tempted beyond what u can bear' hivyo unapata Mlango

Kwa ujumla sana uhakikishe hulali mkiwa mmenuniana myamalize....kuweka visa hapa ni mtafaruku sote members hapa!
 
Machafuko yapo sana tena makubwa.Ila yote yanawezekana kwa kumshirikisha Mungu,ukimkabidhi Mungu yote yanakuwa mepesi.
Kuhusu kusimulia visa hapa utakaposikia utadhani ni hadithi za kutunga na pia haitakuwa vema italeta kesi
 
ulimwengu wa saiv hamna nyumba ambayo watu wanaishi kwa salama ni watu wawe wastahamilivu basi,na kumtanguliza allah s.w pale kila mitihani inapo kufika na ata isipo kufika kwani yy ndie haqqim.
 
sio lazima kua kila anae changia awe ktk mahusiano au ndoa .unaweza kujua tu bcz unaishi na watu unaona ktk macho yko ambayo yanatokeaa:A S cry:, kwahiyo si lazima hivyo bro ,la msingi ushauri ,
 
Machafuko yapo lakini si busara kutoa siri za ndani ya nyumba hadharani, nikishasema ili iweje utakuja kusaidia au?

kwan nan anakujua ata km ukisema?
yap si vyema kutoa siri za ndan..bt uyu ajakwambia umpe siri zako yeye anatakla vsa mkasa ili apate kujifunza..vsa ni lazima vilikuwa vnajulikana kdg na sio siri kivile km ambavyo mtu angekuuliza mkeo ana alama gan kwenye.....

so apa uyu ajaomba ajue siri zenu anataka VISA MKASA VILE aMBAVYO ANAWEZA KUJIFUNZA KITU...
 
hata vikombe kabatini vinagongana,kwahyo migongano hata kwa binadamu wa kawaida ni lazma iwepo.
 
ulimwengu wa saiv hamna nyumba ambayo watu wanaishi kwa salama ni watu wawe wastahamilivu basi,na kumtanguliza allah s.w pale kila mitihani inapo kufika na ata isipo kufika kwani yy ndie haqqim.
la kutangulaiza Mungu ni muhimu sana, ila lifuatiwe na kuwekana wazi kwa kila jambo, i mean kwa kila jambo kwel kwelii, kwani kufichana fichana ndo chanzo kikubwa cha migogoro, kama una jambo ni vema mwenzako akalijua , kwani hawezi kuwa malaika wa kujua mawazo yako, openess is the key... share kero zote , na furaha zote hata kama ni kitu kidogo tu . principal share, share ,share, .. be positive..
 
makwaruzano ni kitu cha kisichoepukika kwani hakuna aliye mkamilifu. cha msingi ni kuangalia wapi mlikoseana na kusuluhisha, kwa wale ambao bado hawajaingia lazima wajue kuwa kuna makwaruzano ili kuepuka talaka zisizo na msingi.
 
kuwa mme wangu wa muda halafu changia.

hahahahahah matatizo yapo kila mahali sema unachotakiwa ni kukaa na mume/mke wako mkayatatua. kama mliweza kukutana kwa maneno mkaelewana kwa maneno na kuoana. hata matatizo mtayamaliza ninyi wenyewe kwa maneno yenu wenyewe na si watu kutoka nje.
 
Yes zipo ndoa zenye furaha kila siku. Zile ambazo kuhojiwa, kujieleza, kuhoji, kueleza, kubrainstorm and kudiscuss critically, changamoto zote wanazikubali na kuzichukulia kama chachu na msingi wa mapenzi yao.
 
kwan nan anakujua ata km ukisema?
yap si vyema kutoa siri za ndan..bt uyu ajakwambia umpe siri zako yeye anatakla vsa mkasa ili apate kujifunza..vsa ni lazima vilikuwa vnajulikana kdg na sio siri kivile km ambavyo mtu angekuuliza mkeo ana alama gan kwenye.....

so apa uyu ajaomba ajue siri zenu anataka VISA MKASA VILE aMBAVYO ANAWEZA KUJIFUNZA KITU...

Nakubaliana nawe Rose lakini mtoa mada keshasema tutoe visa vya ukweli na siyo kutunga hadithi, sasa kuanza kujieleza oh kilikwenda kikarudi hivi na vile nadhani haimsaidii sana. na hata kama hakuna anayenifahamu lakini ni kama kudhalilisha wanandoa tu na kuwaogopesha walioko nje bado, wacha waingie wakajionee wenyewe ndoa ni realty.
 
Back
Top Bottom