Kama ndoa yako au mahusiano yenu yanakaribia kuvunjika dawa hii hapa

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,556
2,560
Wale wote waliopo kwenye ndoa na mahusiano ambayo yanapumulia mashine muda wowote yanaenda kuzimu basi leo kuna mwarobaini wa tatizo lenu hapa.
Ukitaka kuishi na mke wako bila ugomvi inabidi ufanye kitu kimoja rahisi sana. Wala usipate shida maongezi yenu inabidi yawe kama ifuatavyo:

ASUBUHI
mkeo: baby leo ninajisikia kuchokachoka hata sijisikii kunywa chai
Wewe: usijali baby ngoja nitakuandalia maziwa na mkate siunajua jana nilirudi na siagi naimani utaenjoy tea leo
mkeo: baby huyu mtangazaji wa kipindi hiki cha magazeti simpendi sijui yupoje hajui hata kutangaza mie ananiboa
Wewe: umeona eeh dia, siku hizi mtu ukiwa muongeaji tu basi unaajiriwa tu redioni yani mimi mwenyewe huyu mtangazaji simpendi
Mkeo: baby naomba unifumue nywele nataka nikanyoe sikuhizi sipendipendi manywele
Wewe: umeona eeeh baby yani nywele siku hizi zinazingua mimi mwenyewe zangu sizipendi

MCHANA
mkeo: my husband leo najisikia tutoke nimemiss kwenda beach sana
Wewe : unataka twende beach gani ? Yani kama ulikuwa kwenye kichwa changu mimi mwenyewe nimemiss kwenda beach kinoma.
mkeo: baby mi sipendi upepo wa leo unatoka west kuelekea east mi napendaga ule upepo unaotokea east bhana
Wewe: basi baby, kitu kidogo tu unanuna usijali soon utabadili direction

USIKU
mkeo: baby leo sitaki kunywa mirinda ina sukari nyingi
Wewe: umeona mke wangu yani hii soda bhana masukari kibao utazani asali bhanaa
Mkeo: baby hivi nyie simba viporo vyenu mnamaliza lini sie yanga hatuna kiporo hata kimoja
Wewe: umeona baby yani timu ikiwa na kiporo inaniuzi yani mi mwenyewe nataka nihamie yanga
Mkeo: baby njoo tulale basi acha kuingia Instagram mi nakereka bhana
Wewe: kweli baby yanii insta sometimes inakera

Basi ndo kama hivyo, ukitaka kuishi na hivi viumbe we mkubalie tu kila kitu utaona kama ndoa yako au mahusiano yako yatayumba tena
MSISAHAU KUJA KUTUPA MREJESHO
 
Hivi ndoa au mahusiano yanakaribia kufa unayajua watu hata salam hakuna eti beby acha mchezo nahisi kichwa cha habari ndo umekosea ila kama kuboresha mahusiano ama ndoa ambayo haina matatizo makubwa uko sahihi
 
Duuh kila kitu unasapoti

Balaa linakuja anapoliamsha mbele za watu msimamo kama mwanaume inabidi tu
 
Hayo yote yanawezakana ila sio kwa hawa mademu wa kuokota uwanja wa fisi...labda kama demu nikimkuta bikra...eti, au nasema uongo ndugu yangu Jokajeusi
 
Back
Top Bottom