Kuna mzimu gani CCM?

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Kuna mzimu fulani ndani ya CCM ambao una nguvu kubwa kuliko ambavyo mtu anaweza kufikiria. Mzimu huu haonekani wala hwezi kuushika. Lakini upo.

Mtu anapokuwa nje ya mfumo wa CCM na serikali yake anaweza kuonekana kuwa mtu wa busara na hekima. Mtu kama kama huyu akiongea huwa anatema nondo tu.

Chukua wanazuoni waliokuwa maarufu kama Prof Kabudi, Dr Mwakyembe na kadhalika. Watu hawa walikuwa wanatema nondo kila mara walipokuwa wanazungumza

kwenye midahalo iliyokuwa inarushwa kwenye runinga. Lakini walipoingia ndani ya mfumo wa CCM wakakumbana na mzimu wa CCM na nguvu zake. Walifanya turnaround ya 360 degrees

na kufanya kinyume cha kile waliokuwa wakikiamini hapo awali. Wengine kama Dr Mwakyembe walikana maadiko yao. Yote haya ni matokeo ya mzimu huu wa CCM.

Lakini ngoja niwaambie kitu kimoja. Mzimu huu haufuati watu wa kawaida tu. Unaweza kufikiri kwamba mzimu huu unaongozwa na kuratibiwa na kiongozi mkuu wa nchi. Na ni sahihi kufikiria hivyo. Lakini sivyo.

Hebu turudi nyuma mwaka 2011 ambapo Rais JK alianzisha mchakato wa kupata katiba mpya. Binafsi naamini JK alikuwa na dhamira ya kuipatia nachi katiba mpya ambayo mwenyewe alisema inaweza kulipeleka taifa mbele miaka 50 ijayo.

Hata mapendekezo ya tume ya Warioba yalipotolewa aliwaambia wana CCM wenzake kwamba wajiandae kisaikolojia kuwa na serikali 3. Ghafla mzimu usioonekana akini wenye nguvu ukajitokeza.

Siku anahutubia bunge la katiba akawa si JK tuliyekuwa tunamjua hapo awali. Tayari akwa ameshakuwa mhanga wa mzimu wa CCM. Mzimu usioonekana lakini wenye nguvu sana.

Kila nikichingulia ndani ya CCM siuoni mzimu huo lakini upo na unafanya kazi. Wala usidhani mzimu uko ndani ya Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya CCM.

Hivi ni vyombo ambavyo Rais ndo mwenyekiti wake na anaweza kuviongoza na kuelekeza anavyoona inafaa. Lakini mzimu huu hauko katika vyombo hivyo.

Angalia sasa Rais Samia na suala la katiba mpya. Huyu alikuwa Makamu Mwenyekiti wa bunge la katiba na alikuwa muumini wa katiba mpya. Ungedhani baada ya kupata madarka ya ofisi nr 1 angemalizia mchakato wa katiba. Lakini naye tayari naye amekuwa mhanga wa mzimu ambao uko ndani ya CCM.

Na kwa sababu amekuwa mhanga eti anazungumzia kwanza kujenga uchumi kana kwamba kujenga uchumi na kuwa na mchakato wa katiba mpya haviwezi kwenda pamoja!

Tufanyeje tuuondoe huu mzimu CCM?
 
Mzimu wa CCM kizazi hiki cha dot com kizazi laini hakiwezi kuondoa huo mzimu.

Labda mbeleni huko ila kwa nyinyi wa sasa mmelegea sana.
 
Mzimu huo unaozunguzia hapa bila shaka chimbuko na asili yake hasa ni Chadema. Ebu fikiria mtu kama Lisu ambae alikuwa na misimamo na kauli zisizoyumbishwa na mtu yoyote, lkn mwaka 2015 kakubali kuyumbishwa na deki barabarani kapigishwa kama kawa na Lowasa. Hapo sijamzungumzia Mbowe ambae ni mweupe kbs ki misimamo.

images (7).jpeg

images (12).jpeg

images (10).jpeg
 
Kuna mahali uliniambia pia kuhusu hili natamani kujua zaidi
Kafara la pili kubwa baada ya la bagamoyo lilifanyika mkoa wa Lindi kwa masharti ni lazm mkoa uliofanywa kafara hilo la kuitambikia nchi uwe masikini yaani watu wake wawe na ufahamu duni.Lindi ndio mkoa masikini kuliko yote tza watu wake wamefungwa ufahamu japo Wana raslimali tele
 
Pale msitu was Ngende

Hii nchi inahitaji ukombozi wa mara ya pili haiji akilini nchi ya pili kwa raslimali virgin dunia nzima ikawa fukara dhoofu hali watu kufa kwa kukosa 500 ya Panadol,hali mali chekwa kila mahali.
Ukiingia tu porini na sururu unajichotea tu madini nguvu yako na mambo yanakwenda tu.Ardhi bure inayostawi chochote mfano katani,karanga,mtama,Mihogo,kunde,mbaazi bila hata dawa na ukatoka.
Kama sio matambiko yaliyofanyika kutufunga akili huku tukirogwa kupitia mwenge ni nini sasa.
 
Kwakweli kila siku nawaza unavyowaza kuhusu hili, kuna vyanzo vingi sana vya mapato Tz kubwa ina kila kitu, Serikali ya ccm badala ya kutengeneza ajira kwa vijana kutokana na rasilimali zilizopo nchini wanaishia kutoza makodi mengi bila ya kuimarisha ajira, inamaa wananchi watawezaje kulipa makodi mengi bila ya vyanzo vya mapato?? Alafu utakuta kijana bado anashabikia sjui huwa wametolewa akili ?
 
Huwezi tenganisha ccm na umasikini.Umasikini ukipungua na ccm itatoweka.Ni nadra Sana kukuta mtu aliyeelimika akashabikia ccm labda tu kuna maslai anapata.Maana ccm ni muunganiko wa vyama vya kichawi vilivyoungana kumuomba shetani awasaidie kuwaondoa wakoloni rejea matambiko ya mapangoni bagamoyo kupitia shehe yahya, Forozo Ganze na wazee wengine masharti yepi waliambiwa na shetani wakayakubali hadi wakoloni wakafungasha bila damu, Nyerere akudai UHURU bidii ilifanywa na wazee Nyerere alipewa tu udereva lakini hakununua gari.Baada ya kupewa udereva akaanza kuwafifisha waliompa udereva,moto ulipotaka kuwaka baada ya kwenda kinyume nao akawaanzishia bakwata Ili kuwapooza.Huwezi ukatenganisha ccm na umasikini.Umasikini uleta ujinga na mtu akiwa mjinga ni rahisi kudanganywa.
 
Back
Top Bottom