Kuna mzimu gani CCM?

Kuna mzimu gani CCM?

Kuna mzimu fulani ndani ya CCM ambao una nguvu kubwa kuliko ambavyo mtu anaweza kufikiria. Mzimu huu haonekani wala hwezi kuushika. Lakini upo.

Mtu anapokuwa nje ya mfumo wa CCM na serikali yake anaweza kuonekana kuwa mtu wa busara na hekima. Mtu kama kama huyu akiongea huwa anatema nondo tu.

Chukua wanazuoni waliokuwa maarufu kama Prof Kabudi, Dr Mwakyembe na kadhalika. Watu hawa walikuwa wanatema nondo kila mara walipokuwa wanazungumza

kwenye midahalo iliyokuwa inarushwa kwenye runinga. Lakini walipoingia ndani ya mfumo wa CCM wakakumbana na mzimu wa CCM na nguvu zake. Walifanya turnaround ya 360 degrees

na kufanya kinyume cha kile waliokuwa wakikiamini hapo awali. Wengine kama Dr Mwakyembe walikana maadiko yao. Yote haya ni matokeo ya mzimu huu wa CCM.

Lakini ngoja niwaambie kitu kimoja. Mzimu huu haufuati watu wa kawaida tu. Unaweza kufikiri kwamba mzimu huu unaongozwa na kuratibiwa na kiongozi mkuu wa nchi. Na ni sahihi kufikiria hivyo. Lakini sivyo.

Hebu turudi nyuma mwaka 2011 ambapo Rais JK alianzisha mchakato wa kupata katiba mpya. Binafsi naamini JK alikuwa na dhamira ya kuipatia nachi katiba mpya ambayo mwenyewe alisema inaweza kulipeleka taifa mbele miaka 50 ijayo.

Hata mapendekezo ya tume ya Warioba yalipotolewa aliwaambia wana CCM wenzake kwamba wajiandae kisaikolojia kuwa na serikali 3. Ghafla mzimu usioonekana akini wenye nguvu ukajitokeza.

Siku anahutubia bunge la katiba akawa si JK tuliyekuwa tunamjua hapo awali. Tayari akwa ameshakuwa mhanga wa mzimu wa CCM. Mzimu usioonekana lakini wenye nguvu sana.

Kila nikichingulia ndani ya CCM siuoni mzimu huo lakini upo na unafanya kazi. Wala usidhani mzimu uko ndani ya Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya CCM.

Hivi ni vyombo ambavyo Rais ndo mwenyekiti wake na anaweza kuviongoza na kuelekeza anavyoona inafaa. Lakini mzimu huu hauko katika vyombo hivyo.

Angalia sasa Rais Samia na suala la katiba mpya. Huyu alikuwa Makamu Mwenyekiti wa bunge la katiba na alikuwa muumini wa katiba mpya. Ungedhani baada ya kupata madarka ya ofisi nr 1 angemalizia mchakato wa katiba. Lakini naye tayari naye amekuwa mhanga wa mzimu ambao uko ndani ya CCM.

Na kwa sababu amekuwa mhanga eti anazungumzia kwanza kujenga uchumi kana kwamba kujenga uchumi na kuwa na mchakato wa katiba mpya haviwezi kwenda pamoja!

Tufanyeje tuuondoe huu mzimu CCM?
CCM haiondoki mkuu ....

CCM ni Tanzania na Tanzania ni CCM.....

Hebu nielewe hivi......

Umepata kufahamu kuwa Tanzania ni "shock absorber" ya matatizo ya nchi zote zinazoizunguka?

#JMTMilele
#SiempreCCM
#VivaCCM
 
Bila shaka Profesa MajiMarefu na Kingunge Ngombale Mwiru wamekufa na siri nzito sana, pasina shaka Edward Lowassa anafahamu sirikali za hii DEEP STATE. Baada ya Uhuru, ChamaChaWalozi(CCW) kilimruhusu Nyerere pekee kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika na baadae kuwa Raisi, na kikaweka MWIKO kwa Waziri Mkuu yeyote kuwa Raisi baadae.
Lowassa pamoja na kuutambua huu Mwiko, aliamua kupimana ubavu na Walozi; na hata alipoukosa Uraisi na kurudi chamani, hawakuwa na ubavu wa kumuadhibu kwa kuvunja miiko ya chama kwa kuwa ameshikiria nguvu za Makafara ya upande wa Kaskazini. Ukiachana na Makafara ya Bagamoyo na Lindi(Kingunge pia amezaliwa Kilwa), Nchi yetu pendwa imefanyiwa Makafara pande zote nne, kuna Makafara ya Handeni Tanga, Ziwa Tanganyika (Kigoma Vijijini na Sumbawanga,Nkasi-Namanyere), Ziwa Nyasa-Mbinga, Ziwa Nyanza na Zanzibar.
Hii ni vita ya KIROHO, ni lazima tuchunguze na kuvunja MAAGANO yote ndio tutaikomboa Nchi, IMANI bila MATENDO imekufa. Mambo ya Kisayansi hutatuliwa kisayansi, Maombi matupu bila kujua mbinu za adui yako ni sawa na kujirisha upepo, ni lazima tujue maeneo yote ya Makafara, ni kupiga kambi, kuomba na kuteketeza kwa MOTO.
 
Back
Top Bottom