Mkuu wewe mbona kichwa chako nikigumu kuelewa Nimekuuliza tunatumia logic ipi kupata maana sahihi ya Neno Mungu ?
We unasema wa biblia na Qur'an Mimi sijauliza Mungu gani nataka maana ya Mungu
Mboka akili yako Ni nzito sana!!
Ukishindwa waombe msaada kina scar wakusaidie.
Basically huwa tuna define the same exact way mnavyo define nyinyi ila utofauti ni kuwa sisi tunaanza na neno "fictional" mwanzoni mwa maelezo
Hili swala nishawahi kulitolea ufafanuzi humu
Mara nyingi kwenye mijadala inayowakutanisha Atheists na Theists, Atheists wamejikuta wakiambiwa watoe maana ya Mungu kwa namna yao wanayoijia wao.
Sasa swali hili linaweza kuonekana kama ni swali la kiudadisi (curious) kutoka kwa anayeamini, lakini ukweli ni kwamba swali hili typically linakuwa katika mfumo mmoja unaitwa "gotcha"
Aina ya maswali ambayo yanaulizwa ili kumtega mtu. Kama atheist akashindwa kutoa maana ya kile ambacho wamedai kutokiamini, then hoja itayofuata hapo ni kuwa atheists hawana justification ya kusema kitu fulani hakipo au hawakiamini.
Lakini ikatokea atheist amejibu kwa usahihi maana ya kile wasicho kiamini, hoja itayofuata hapo ni kuwa theist watakuja kupoint nukta chache kuonesha tofauti wa kile ambacho atheist wanaki define na kile ambacho wao wanakiamini, na kisha kusema Atheists hawajui wanachokipinga.
Utawasikia "unadai huamini concept hiyo ya uwepo wa Mungu, lakini ukweli ni kwamba hiyo sio maana halisi ya concept ya Mungu"
Kiukweli dhana ya uwepo wa Mungu ni dhana ya zao la ujinga inaweza kuwa dismissed hata na mtoto mdogo au hata half brain.
*****************************†**************
Put yourself in our position
Je Theists mna amini Santa Claus?
Kama jibu ni hapana, je theists mnaweza kufafanua maana ya Santa Claus ni nini? Na kitu gani kinawajia akilini mnaposema kuwa hamuanini Santa Claus?
Je huamini Santa Claus baada ya picha iliyooneshwa katika matangazo ya Cocacola ambayo ilitokana na shairi maarufu la Clement Moore?
Lakini vipi ikiwa ningesema kwamba Santa Claus halisi alikuwa "Father Christmas"
Au vipi kama nikikuambia Santa Claus ya ukweli ilikuwa ni ile ya sinterklaas ambaye, licha ya kuwa chanzo kikuu au nembo maarufu ya Krismasi ya Santa Claus, huonekana na kutenda tofauti sana na toleo la Clement Moore?
Je, maelezo kuhusu toleo gani la Santa Claus yana matter kwa Theists ambaye amedai kutoamini Santa Claus ipo real?
Au inatosha kufafanua Santa Claus kwa upana zaidi kama mtu wa hadithi (mythical) kibabu mwenye midevu myeupe mwenye miujiza ambaye huja majira ya karibu na msimu wa Krismasi na kuleta zawadi kwa watoto?
NB: Na ukumbuke tunaweza tukalirudia hili zoezi kwa idadi yeyote ya vitu ambavyo unadai kutoviamini