Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,992
- 146,309
Sawa.Kuna kosa la msingi huwa unalifanya.
Kitendo Cha kuthibitisha au kutothibitisha uwepo wa Mungu haifanyi hiko kitu kuwepo au kutokuwepo.
Mfano;
Mimi nimeua Kisha nikapelekwa mahakamani kusomewa mashtka, kabla ya hukumu nikapewa nafasi ya kujitetea "nithibitishe" kwamba sijaua. Hapo mahakamani nikatoa maelezo yangu ya utetezi Kisha wakati wa hukumu Sheria ikaona Sina kosa na hivyo kuikwepa hukumu ya kifungo au kunyongwa kwa kosa la mauaji. Nimekuwa huru kwa mujibu wa Sheria.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba, Sheria imeshindwa kuthibitisha kwamba Mimi ni muuaji(nimeua).
Ila ukweli ulio wazi ni kwamba niliua/nimeua. Ila Sheria imeshindwa kuthibitisha hivyo ikashindwa kunihukumu.
Nahitimisha kwa kusema kuwa MUNGU ANASIMAMA KAMA KWELI.MUNGU NI KWELI. Kweli inasimama Kama moja. Kweli haithibitishiki. Either unishinde kwa hoja au nikushinde,hiyo haifanyi kutokuwepo kwa Mungu.
Ni Kama uchawi tu, either uuthibitishe au usiuthibitishe haifanyi uchawi usiwepo. Uchawi upo na kupitia nguvuna matokeo ambayo binafsi nimezishuhudia kwa macho Kama mtu aliyekufa kisha kuwekwa msukule kisha kumuona akiwa mzima miaka mingi baadae ikiwa imeenda. Kama tusivyoweza kuona uchawi ila tunauona kupitia matokeo ndivyo ambavyo hatuwezi kumwona Mungu na kumthibitisha katika namna ambayo wasioamini wanataka tuthibitishe ila tunaona nguvu zake zinavyooperate.
Mungu yupo.
NB: Hili la uchawi nimechomekea tu,tusifanye kuwa mjadala.
1.Kuna vitu vipo, na vinathibitishika kuwa vipo. Hivi tunapata uhakika kwamba vipo, havina tabu.
2. Kuna vitu havipo, kimakosa vinathibitishika kuwa vipo. Hivi tunapata uhakika wa uongo kwamba vipo.
3. Kuna vitu vipo, na havithibitishiki kwamba vipo. Hivi tunataka kuvichunguza na kuvihakikisha kwamba vipo tupate uhakika kwamba vipo.
4.Kuna vitu havipo, na havithibitishiki kwamba vipo au havipo, kwa sababu havipo, na kama havipo, havithibitishiki kuwa vipo au havipo, kwa sababu falsafa ya kuthibitisha kiuhalisia (other than logical proofs such as proof by contradiction) ni kwa vilivyopo, visivyopo havithibitishiki, kwa sababu havipo.
Sasa, umetoa hoja nzuri, kwamba kushindwa kuthibitisha kitu hakumaanishi kitu hakipo. Inawezekana kitu kipo, lakini hakithibitishiki tu. Hili nalielewa na nimelielezea mara kadhaa hapa.
Lakini je, utajuaje kitu kipo, na hakithibitishiki tu, na si kwamba hakithibitishiki kuwa kipo kwa sababu hakipo?
Kabla ya uthibitisho, utajuaje tofauti?
Hatutakiwi kukubali tu kwamba kitu kipo ila hakithibitishiki tu, kwa msingi huo, mimi naweza kukuambia kwamba mimi ndiye Mungu, ila wewe kwa akili zako za kibinadamu huwezi kuthibitisha hilo, utakubali?
Zaidi ya hilo, pingamizi langu kuhusu uwepo wa Mungu si tu kwa sababu wewe huwezi kuthibitisha Mungu yupo.
Pingamizi langu kuhusu uwepo wa Mungu, hususan huyu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni kwamba, hoja ya uwepo wake ina internal contradiction. Uwepo wa Mungu huyu ni sawa na mtu akwambie katika Euclidean planes, kuna pembetatu ambayo hapohapo ni duara, wakati unajua pembetatu na duara ni vitu tofauti, na haiwezekani kuwapo pembetatu ambayo hapohapo ni duara.
Kwa hivyo, ninapokupa mtihani wa kuthibitisha uwepo wa Mungu, tayari najua huwezi kuthibitisha Mungu yupo.
Mungu huyu hayupo, si kwa sababu wewe huwezi kuthibitisha yupo (tushaona kuna vingine hatuwezi kuvithibitisha lakini vipo, inatuchukua miaka mingi kuvithibitisha), lakini, Mungu huyu hayupo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake ina internal contradiction.
You can either have an omnipotent, omniscient and omni benevolent God, or have a universe in which evil is possible.You can't have both logically. The two are mutually exclusive.
And since we have a world in which evil is possible, by using the very definition of people who believe God exists, then that God does not exist.
1. Ni muhimu kuweza kuthibitisha kitu kipo, hata kama kutoweza kuthibitisha kitu kipo hakumaanishi kitu hakipo.
2. Namba 1 hapo juu ni muhimu ili tujue kwamba hatuamini kitu kipo wakati hakipo. Kwa sababu, tukisema tu kitu kipo ila hatuwezi kukithibitisha, inawezekana ikawa hatuwezi kukithibitisha kwa sababu hakipo, tukaamini kipo, wakati hakipo.
3.Muhimu zaidi, sitegemei wewe kushindwa kwako kuthibitisha kwamba Mungu yupo kama uthibitisho wangu kwamba Mungu hayupo. Uthibitisho wangu kwamba Mungu hayupo unatokana na problem of evil/ Epicurean Paradox.Wewe kushindwa kuthibitisha Mungu yupo nakuonesha umeshindwa kuthibitisha Mungu yupo kwa sababu hayupo, si kwa sababu nyingine.
Sijui kama umenielewa.