Kuna mtu anataka kunitapeli naomba msaada

Huyu mtu anafanya biashara na watu ambao nawafahamu nakuna mmoja alitoka huko ndo akaniambia nenda ila nilikuwa nasafarisha songea
Kama umewaamini hao ndugu zako kwa kuwa wanafanya nao biashara kwa nini usiwaite uwaelezee kilichotokea ili wakusaidie kukuchukulia pesa yako kwa huyo bwana unayemuita tapeli mara unasema unamwamini kwa vile alifanya biashara na ndugu zako
 
Ungenisoma mstari kwa mstari ungegundua tayari swali lako lina jibu kwenye maelezo yangu!!!
Nafikiri angekuwa anapokea simu na kutoa ushirikiano wa mwenendo mzima wa huo mzigo wala huu uzi usingekuwepo hapa.

Maoni yako nimeyapitia vizuri tu na kuyaelewa. Ni mazuri sana. Itoshe kusema huyo dalali/ mchuuzi si muungwana.
 
Kuna 1385 na kuna 1835 ipi ni namba sahihi.. Unajua nyinyi wananchi mnaojiita wanyonge kumbe kweli kichwani wanyonge unafanya biashara kabla ya kujumlisha cost zingine tayari unahasara.. Biashara gani hii unapata 250,bora huyo jamaa akutapeli ili ujifunze
Inamaana ujasoma idadi ya walioharibika.
 
Ushadi wa vibali na ushulu kwa sasa sina nimetafuta sana risti ya malipo ya mzigo ya serikali sijaiona pia niliamini biashara nimisha maliza hivyo kibali cha kusafirishia mzigo kilisha pita muda wake labda shaidi kipindi namuuzia alikuwepo
Sasa wewe,nakuonea huruma sana.
Mtafute huyo bwege,muulize pia mama walimalizana vp then ulipe visasi viwili,otherwise alipe deni lako na riba then dai pia za mama.
Akizingua mvizie siku mbanike km samaki,utaalam unao
 
Duh biashara za mazoea hizi! Unafanya biashara ya laki tisa unapata faida ya tshs 250 tu halafu ni graduate unafanya biashara ya bila mkataba na mtu kienyeji tu hivi.Mungu akusaidie!
Utapeli hata ukiwa na phd unaweza tapeliwa kutokana na mazingira husika
 
Ushadi wa vibali na ushulu kwa sasa sina nimetafuta sana risti ya malipo ya mzigo ya serikali sijaiona pia niliamini biashara nimisha maliza hivyo kibali cha kusafirishia mzigo kilisha pita muda wake labda shaidi kipindi namuuzia alikuwepo
Pole sana aisee....pole sana.chuo gani ulichosoma?,bora hata ungemshirikisha bi mkubwa angekupa uzoefu. Huu uandishi sio wa mtu aliyemaliza chuo.hapo hiyo hasara tayari,la msingi umejifunza kitu,hutarudia tena makosa,usikate tamaaa,endelea kupambana.
 
Una invest vipi savings yote kwenye biashara changa? Hapo ndo ilipozongua. Kwa hiyo 900,000/= Kuna biashara nyingi ungeweza kufanya ya kukuingizia hadi nusu ya mtaji. Pole sana
 
Mimi ni kijana niliye maliza masomo yangu mwaka huu, kipindi nikiwa chuo nilikuwa najiwekea akiba kutoka kwenye boom langu ili nikimaliza basi niwe na mtaji ili nianze kufanya biashara, nimefanikisha kuwa namtaji .TZS.1000000/= tarehe 2.9.2020 nilienda wilaya ya simanjiro (manyara)kijiji cha kimotoroki kufata samaki aina ya kambale nili nunua samaki 2000 walio gharimu Tzs. 900000 hapo kuanzia manunuzi hadi kuwabanika kwa moto, niliwasafirisha hadi dodoma kwenye soko la chang'ombe ambapo niliwasiliana na boss ambaye alisema anachukua mzigo wote ananipa pesa yangu siku hiyo hiyo.

Tulifungua samaki akahesabu akapata samaki 1385 kati ya samaki 2000 kutokna na usafiri hao wengine walivunjika hivyo hawakuhesabiwa hiyo ilikuwa tarehe 18/9/2020 , kwa samaki 1835 ilitakiwa anipe TZS. 900250 ila aliomba pesa yangu atanitumia baada ya siku tatu,basi kiungwana nikakubali mimi nikaondoka nikijua pesa ata nitumia hadi sasa hajanitumia pesa na nikimtafuta simu hapokei Wala sms hajibu, Leo nimemtafuta kapokea kaniambia niende dodoma nikafate samaki wangu.

Baada ya kumsumbua sana kuhusu pesa yangu, naomba msaada wenu wa mawazo mimi ni mtoto wamvuvi tena mvuvi wa hali ya chini na mama anafanya uchuuzi wa samaki ila mala nyingi matapeli kama hawa wanatufanyia hivi tukipeleka mizigo sokoni
mtafutie polisi laki mbili jokoe laki Tisa ikishindikana mtafute shehe italudi mkuu
 
Mdogo wangu biashara haiendi hivyo..wachache sana wanafanya hivyo na kufanikiwa..ulitakiwa uanze hata na samaki wa laki 2,then ukiona clients wako wanaeleweka ndo unaongeza mzigo kidogo dogo..hata mtu akila lak 2 yako..bado unakua na nguvu hakufanya biashara regardless ya hasara uliopata..huyo mpeleke polisi..
 
Back
Top Bottom