Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,371
- 14,481
Msamehe tu,jitafutie mtaji mwingine.
Alipaswa afanye research ya kutosha kabla ya kwenda kupeleka mzigo lazima ujue soko na nani utamuuzia na ujue unapataje faida, uzembe mdogo tu kwenye biashara unapata hasara kubwa sana, biashara unatakiwa uchukulie serious umemwaga mtaji wote humo then huchukui tahadhariduh biashara ya kuoza angefanyaje?
Kosa la kwanza ni hili.Huyu mtu anafanya biashara na watu ambao nawafahamu nakuna mmoja alitoka huko ndo akaniambia nenda ila nilikuwa nasafarisha songea
Pole Sana kijana wangu, madalali wa Dodoma ni matapeli sana na ukiripoti polisi hakuna msaada maana wanajuana nao, sidhani kama utapata pesa yako hapo, siku nyingine biashara peleka popote sio Dodoma hapo wanawezana wenyewe. Kuna binti niliishi naye nyumba moja Dar mwaka juzi kaleta Maembe kayafikishia Sabasaba alitapeliwa mzigo wote wakamwambia ukitaka nenda polisi, akaenda kushtaki akaahidiwa atashughulikiwa kawasubiri polisi hakuwaona siku ya pili asubuhi anamwona polisi wake yupo pale kwenye Maembe kabeba anayoyataka kawekewa kwenye mfuko kaondoka alichofanya binti akazoa Maembe yake akakaa pembeni akauza ili apate nauli akajiondokea zake maana hata guest alihama akahamia kwangu, hao ndio madalali wa Dodoma. Kosa kubwa kuondoka wenzako wanakaa hapo hapo mzigo ukiuzwa anachukua pesa yake hata kama ni rejareja kila asubuhi yupo nao hata wakikutisha wewe huongei wanauza unapokea hela. Madalali wa Masoko Dodoma wanalitia aibu jiji na hawana wasimamizi wa maanaMimi ni kijana niliye maliza masomo yangu mwaka huu, kipindi nikiwa chuo nilikuwa najiwekea akiba kutoka kwenye boom langu ili nikimaliza basi niwe na mtaji ili nianze kufanya biashara, nimefanikisha kuwa namtaji .TZS.1000000/= tarehe 2.9.2020 nilienda wilaya ya Simanjiro (Manyara)kijiji cha Kimotoroki kufata samaki aina ya kambale nilinunua samaki 2000 walio gharimu Tzs. 900000 hapo kuanzia manunuzi hadi kuwabanika kwa moto, niliwasafirisha hadi Dodoma kwenye soko la Chang'ombe ambapo niliwasiliana na boss ambaye alisema anachukua mzigo wote ananipa pesa yangu siku hiyo hiyo.
Tulifungua samaki akahesabu akapata samaki 1385 kati ya samaki 2000 kutokna na usafiri hao wengine walivunjika hivyo hawakuhesabiwa hiyo ilikuwa tarehe 18/9/2020 , kwa samaki 1835 ilitakiwa anipe TZS. 900250 ila aliomba pesa yangu atanitumia baada ya siku tatu,basi kiungwana nikakubali mimi nikaondoka nikijua pesa ata nitumia hadi sasa hajanitumia pesa na nikimtafuta simu hapokei Wala sms hajibu, Leo nimemtafuta kapokea kaniambia niende Dodoma nikafate samaki wangu.
Baada ya kumsumbua sana kuhusu pesa yangu, naomba msaada wenu wa mawazo mimi ni mtoto wa mvuvi tena mvuvi wa hali ya chini na mama anafanya uchuuzi wa samaki ila mara nyingi matapeli kama hawa wanatufanyia hivi tukipeleka mizigo sokoni
Hukopeshi mkuu wao wanakwambia nenda tutakutumia hapo ujue tayari maumivuBiashara gani ya kukopesha halafu unapata faida ya 250/=
Hawa madalali wanatabia ya kushuhudiana wenyewe hivyo kukiwa na shahidi ni tapeli mwenzieShahid alioshuhudia mkiuziana, what if akakuruka watu ni waoga kutoaga ushahidi mahakamani, je una plan B?
Umemchambulia kama CPA (T) kabisa.Ki accounts huyo uliyemkopesha tunamuita "Bad debt "...kwenye vitabu tuna treat kama expense ...yaani inapunguza gross profit..akija kukulipa tuta treat kama "Recoverable bad debt" tuta add na gross profit ...asipokulipa... tutamuweka kwenye "Provision for Doubtful debts" kwa asilimia zetu...na at the end of the year(tunapofunga books of the accounts) tunaenda kumpunguza kwenye Debtors( Accounts Receivable) ...mchezo unakuwa umeisha ...hope umenielewa mkuu...
Polisi hamna msaada maana hio kesi ya mahakaman na hana ushahidi in writings. Cha kufanya labda akam confront mdeni wake akijibu shit akaandikie kesi kwamba kamtishia maisha ndo watamuweka ndani.😂😂😂Mdogo wangu biashara haiendi hivyo..wachache sana wanafanya hivyo na kufanikiwa..ulitakiwa uanze hata na samaki wa laki 2,then ukiona clients wako wanaeleweka ndo unaongeza mzigo kidogo dogo..hata mtu akila lak 2 yako..bado unakua na nguvu hakufanya biashara regardless ya hasara uliopata..huyo mpeleke polisi..
Hivi vitu vyetu chief...Umemchambulia kama CPA (T) kabisa.
Hahahahah imagine umeshusha Fuso ya mzigo halafu baada ya siku 3 dalali analeta usenge. Hio shangazi yangu alishapigwa 16M akatoka from hero to zero. Na alikuwa mzoefu kwenye game wenzake wakapigwa 300M walifanyia biashara Zambia.Mie niko poa best, ya huyo kijana we acha tu!!
Hawa wanaomkejeli natamani kuwapiga makofi... mbaya zaidi wanamkejeli kwa kitu wasichokijua manake wangekuwa wanafahamu biashara za jumla masokoni zinaendeshwaje wala wasingekuwa wanamkejeli!!
Una umri gani dogo?
Ushapigwa tayari
biashara ngumu asehHapo kwenye faida ndipo nimebaki hoi.
Siyo madalali wa Dodoma tu ila madalali popote pale Tanzania ni watu matapeli. Tanzania dalali ndiye anakuwa na nguvu na mwenye mali anakuwa kama mtumwa. Ni tofauti kabisa na nchi nyingine ambapo madalali wanakuwa waaminifu na wanyenyekevu. Nachojiuliza kila siku: Hivi kwenye biashara zetu ni lazima tutumie madalali? Kwa nini kama unasafirisha maembe usiyatafutie soko wewe mwenyewe? Wengi nadhani watajibu haiwezekani lakini mimi nasema ni uvivu wa watanzania tu kuzoea vya kunyonga. Mimi siku yoyote nitakayopingia kwenye biashara naapa sitatumia dalali. Nitatafuta soko peke yangu na bidhaa ikidoda basi inidodee mimi.Pole Sana kijana wangu, madalali wa Dodoma ni matapeli sana na ukiripoti polisi hakuna msaada maana wanajuana nao, sidhani kama utapata pesa yako hapo, siku nyingine biashara peleka popote sio Dodoma hapo wanawezana wenyewe. Kuna binti niliishi naye nyumba moja Dar mwaka juzi kaleta Maembe kayafikishia Sabasaba alitapeliwa mzigo wote wakamwambia ukitaka nenda polisi, akaenda kushita akaahidiwa atashughulikiwa kawasubiri polisi hakuwaona siku ya pili asubuhi anamwona polisi wake yupo pale kwenye Maembe kabeba anayoyataka kawekewa kwenye mfuko kaondoka alichofanya binti akazoa Maembe yake akakaa pembeni akauza ili apate nauli akajiondokea zake maana hata guest alihama akahamia kwangu, hao ndio madalali wa Dodoma. Kosa kubwa kuondoka wenzako wanakaa hapo hapo mzigo ukiuzwa anachukua pesa yake hata kama ni rejareja kila asubuhi yupo nao hata wakikutisha wewe huongei wanauza unapokea hela. Madalali wa Masoko Dodoma wanalitia aibu jiji na hawana wasimamizi wa maana