Kuna mtu anataka kunitapeli naomba msaada

Ki accounts huyo uliyemkopesha tunamuita "Bad debt "...kwenye vitabu tuna treat kama expense ...yaani inapunguza gross profit..akija kukulipa tuta treat kama "Recoverable bad debt" tuta add na gross profit ...asipokulipa... tutamuweka kwenye "Provision for Doubtful debts" kwa asilimia zetu...na at the end of the year(tunapofunga books of the accounts) tunaenda kumpunguza kwenye Debtors( Accounts Receivable) ...mchezo unakuwa umeisha ...hope umenielewa mkuu...
Mkuu adi debtor aje kuwa bad debtor au deni liwe bad debt kuna conditions lazini zikidhi ndo tutasema deni limekuwa bad debt.....kwa situation ya huyo jamaa bado kuwa bad debt.

Huyo ni debtor sema inabidi apo aweke % za provision for doubtful debts , Mana apo kuna uwezekano asilipwe deni lote coz hiyo amount ya mkopo ni kubwa mno ukilinganisha na situation waliokopesheana.

Mkuu pambana mi naamini ukikaza sura pesa yako utapata japo nahisi kupata zote si rahisi kihvyo.

Ila sku nyengine usifanye huo mchezo (don't put all your eggs in one bucket) na usiwaamini watu ktk biashara...apo ungechukua ata laki 4 ufanye hyo biashara,nyengine (laki 2) ungewekeza Kwenye kuuza ata pipi na karanga... nyengine (laki 2) ungeiweka bank kama akiba itakayo baki ndo pocket money kilinda mfuko na tumbo.
 
Mimi ni kijana niliye maliza masomo yangu mwaka huu, kipindi nikiwa chuo nilikuwa najiwekea akiba kutoka kwenye boom langu ili nikimaliza basi niwe na mtaji ili nianze kufanya biashara, nimefanikisha kuwa namtaji .TZS.1000000/= tarehe 2.9.2020 nilienda wilaya ya simanjiro (manyara)kijiji cha kimotoroki kufata samaki aina ya kambale nili nunua samaki 2000 walio gharimu Tzs. 900000 hapo kuanzia manunuzi hadi kuwabanika kwa moto, niliwasafirisha hadi dodoma kwenye soko la chang'ombe ambapo niliwasiliana na boss ambaye alisema anachukua mzigo wote ananipa pesa yangu siku hiyo hiyo.

Tulifungua samaki akahesabu akapata samaki 1385 kati ya samaki 2000 kutokna na usafiri hao wengine walivunjika hivyo hawakuhesabiwa hiyo ilikuwa tarehe 18/9/2020 , kwa samaki 1835 ilitakiwa anipe TZS. 900250 ila aliomba pesa yangu atanitumia baada ya siku tatu,basi kiungwana nikakubali mimi nikaondoka nikijua pesa ata nitumia hadi sasa hajanitumia pesa na nikimtafuta simu hapokei Wala sms hajibu, Leo nimemtafuta kapokea kaniambia niende dodoma nikafate samaki wangu.

Baada ya kumsumbua sana kuhusu pesa yangu, naomba msaada wenu wa mawazo mimi ni mtoto wamvuvi tena mvuvi wa hali ya chini na mama anafanya uchuuzi wa samaki ila mala nyingi matapeli kama hawa wanatufanyia hivi tukipeleka mizigo sokoni

Dah pole sana, ila mtu haumjui wala nin unamuachia mzigo wote. Biashara ni kutake risk lakini hii imezid Broo
 
Kusoma kwako kwote mpaka level ya degree hujawahi kusikia kua

"usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja"

Mbona hyo ni general rule kila mjasiriamali na mfanya biashara anaijua we ulisahauje ukaenda kununua mzigo wa laki tisa out of milion apo hata hujui mzunguko wa biashara upoje

Pole sana there are more to come, be SMART.
 
Mkuu adi debtor aje kuwa bad debtor au deni liwe bad debt kuna conditions lazini zikidhi ndo tutasema deni limekuwa bad debt.....kwa situation ya huyo jamaa bado kuwa bad debt.

Huyo ni debtor sema inabidi apo aweke % za provision for doubtful debts , Mana apo kuna uwezekano asilipwe deni lote coz hiyo amount ya mkopo ni kubwa mno ukilinganisha na situation waliokopesheana.

Mkuu pambana mi naamini ukikaza sura pesa yako utapata japo nahisi kupata zote si rahisi kihvyo.

Ila sku nyengine usifanye huo mchezo (don't put all your eggs in one bucket) na usiwaamini watu ktk biashara...apo ungechukua ata laki 4 ufanye hyo biashara,nyengine (laki 2) ungewekeza Kwenye kuuza ata pipi na karanga... nyengine (laki 2) ungeiweka bank kama akiba itakayo baki ndo pocket money kilinda mfuko na tumbo.
Ukiwa na milioni...fanya biashara ya laki...principles of business...sio wewe umekopa 5m bank yote unatumbukiza kwenye biashara....ukikopa benki mill 10 hakikisha wewe na 40mill zako ...principles of business...
 
Chikolombe njo nkupeleke kwa mganga tunamtoa magamba mwili mzima kama hao samaki aliodhulumu.

Mganga achukui pesa mpaka umuhakikishie jamaa katoka magamba mpaka kwenye macho.
 
Dah! pole sana mkuu ila kwa mwenendo huo ni rahisi sana kudhurumiwa kirahisi labda muwe mliandikishana vinginevyo ni maumivu tu.
 
Hivi una miaka mingapi mpendwa maana naona bado akili ya kitoto unakusumbua

Hiyo hela huipati ng'oo 😂
 
Huko chuoni dogo unasome ujinga gani kwanza umenunua samaki pcs 2000 umeshindwa kuzitunza vizuri umefikisha pcs 1300tu na bado hizo samaki umekwenda kumkabidhi tapeli

Ningekuwa Mimi ndio baba yako ungenirudishia pesa za karo sio kwa utopolo wa kiwango hicho
 
Mshushe busha tu.
Yaani hiyo pesa yako bora unge bet au ungehonga mtoto mzuri umtafune kwa mwaka mzima.
 
Nenda mahakaman kafungue kes ya madai, jamaa anakutingishia kiberiti ukijidai mtu wa kanisa umeumia , dunia hi unatakiwa uwe na roho mbaya kwa mtu anae kufanyia ubaya

Hii dunia haipo kwaajili ya watu wenye mioyo mizuri
 
Mimi ni kijana niliye maliza masomo yangu mwaka huu, kipindi nikiwa chuo nilikuwa najiwekea akiba kutoka kwenye boom langu ili nikimaliza basi niwe na mtaji ili nianze kufanya biashara, nimefanikisha kuwa namtaji .TZS.1000000/= tarehe 2.9.2020 nilienda wilaya ya Simanjiro (Manyara)kijiji cha Kimotoroki kufata samaki aina ya kambale nilinunua samaki 2000 walio gharimu Tzs. 900000 hapo kuanzia manunuzi hadi kuwabanika kwa moto, niliwasafirisha hadi Dodoma kwenye soko la Chang'ombe ambapo niliwasiliana na boss ambaye alisema anachukua mzigo wote ananipa pesa yangu siku hiyo hiyo.

Tulifungua samaki akahesabu akapata samaki 1385 kati ya samaki 2000 kutokna na usafiri hao wengine walivunjika hivyo hawakuhesabiwa hiyo ilikuwa tarehe 18/9/2020 , kwa samaki 1835 ilitakiwa anipe TZS. 900250 ila aliomba pesa yangu atanitumia baada ya siku tatu,basi kiungwana nikakubali mimi nikaondoka nikijua pesa ata nitumia hadi sasa hajanitumia pesa na nikimtafuta simu hapokei Wala sms hajibu, Leo nimemtafuta kapokea kaniambia niende Dodoma nikafate samaki wangu.

Baada ya kumsumbua sana kuhusu pesa yangu, naomba msaada wenu wa mawazo mimi ni mtoto wa mvuvi tena mvuvi wa hali ya chini na mama anafanya uchuuzi wa samaki ila mara nyingi matapeli kama hawa wanatufanyia hivi tukipeleka mizigo sokoni
Kuna mtaalam mmoja aliwahi kusema "kasi ya kiongozi wa wahuni ndio kasi ya wahuni wenyewe", dogo next time respect your money! Otherwise utaishia kuwa km huyo mwamba kwenye avatar yako
 
Halafu we bhana ungekuwa wife wangu tungezaa maparoko watupu waliojazwa upako huko huko!!

Kilichoniumiza zaidi sio risk ya kutapeliwa bali ni kuona kijana mdogo aliyeamua kujinyima akiwa chuo ili asiadhirike akirudi mtaani, anatokea mshenzi mmoja anataka kumdhulumu haki haki!

Sie wengine ilikuwa tukipata boom hata stimu za kukaa darasani zinakatika lakini dogo yeye kaamua kujiwekea akiba!!!

We are twins, ndio maana tulipendana toka mwanzo humu! Hahah nakusalimu kipenzi.

Kiukweli kijana kanisikitisha sana ni vile tu sina chakumsaidia.
 
Vijana wengi siku hizi mnaenda vyuoni kwa sababu vyuo vina nafasi.
Kuna mtaalam mmoja aliwahi kusema "kasi ya kiongozi wa wahuni ndio kasi ya wahuni wenyewe", dogo next time respect your money! Otherwise utaishia kuwa km huyo mwamba kwenye avatar yako
Huko chuoni dogo unasome ujinga gani kwanza umenunua samaki pcs 2000 umeshindwa kuzitunza vizuri umefikisha pcs 1300tu na bado hizo samaki umekwenda kumkabidhi tapeli

Ningekuwa Mimi ndio baba yako ungenirudishia pesa za karo sio kwa utopolo wa kiwango hicho
Nyote nyinyi inaonesha hamjawahi kuuza hata pipi kwahiyo nyamazeni kwa sababu hakuna mnachojua!!

Alichofanya dogo kwa kiasi kikubwa ndicho kinachofanyika, kwahiyo acheni kumkejeli wakati hamjui lolote!! BIashara za aina hii zinaenda kwa "mali kauli"!
 
Hao ndio maadui wa maendeleo, hakika umedhulumiwa, hakuna sababu ya kwenda huko , mwombee dua afe tu.

Mloge afie huko

Pole.
Sasa akifa si atakufa na mtaji wake... halafu baada ya hapo arudi kijiweni, au?!

Lakini bora umeona tatizo kuliko wale wanaomkejeli wakati dogo kama huyu alitakiwa kupongezwa! Watu boom wanapigia pombe tu lakini yeye akawa ana-save ili baada ya kumaliza chuo awe na pa kuanzia!!
 
We are twins, ndio maana tulipendana toka mwanzo humu! Hahah nakusalimu kipenzi.

Kiukweli kijana kanisikitisha sana ni vile tu sina chakumsaidia.
Mie niko poa best, ya huyo kijana we acha tu!!

Hawa wanaomkejeli natamani kuwapiga makofi... mbaya zaidi wanamkejeli kwa kitu wasichokijua manake wangekuwa wanafahamu biashara za jumla masokoni zinaendeshwaje wala wasingekuwa wanamkejeli!!
 
Back
Top Bottom