Hoja ni kwamba, mfumo wa mali kauli unatumika sana kwenye masoko yetu; sasa kinachofuata hapo ni uaminifu wa yule aliyeachiwa mali kwa mali kauli!!
Na hili tatizo linachangiwa na mambo makuu mawili:-
1. Madalali hawapo regulated,
2. Majority kama sio wote wanategemea kumlipa mwenye mzigo baada ya mzigo kuuzwa kwa sababu hawana mitaji! Wengi wanachoweza kufanya in advance ni ku-clear madeni ya Seller... kwa mfano, kama unadaiwa na transporter, dalali atakachofanya ni ku-clear deni la transporter, kisha mnamalizana juu kwa juu!
Kutokana na hilo, wakati mwingine unakuta dalali wala sio nia yake kukutapeli bali unakuta umemuachia mzigo na bishara imegoma kutegemea na hali ya soko!!!
Kitakachofuata hapo, ni full calendar... au kama alivyojibiwa dogo kwamba "kama vipi, njoo uchukue mzigo wako"!!
Wakati mwingine, na ni kawaida sana kukuta kweli dalali bado mzigo anao!!!