Kuna mpasuko mkubwa mno ndani ya CCM kutokana na wamachinga wanavyotendewa

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Ni suala la muda tu.

Kuna sintofahamu kubwa mno ndani ya CCM baina yao na mbaya zaidi ni mpasuko uhusuyo Kanda na namna ambavyo machinga wanavyotendwa.

Ikumbukwe, asilimia kubwa ya wabunge wa CCM hawapendezwi mno na namna zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yao ya sasa linavyofanyika lakini hawataki kuonyesha misimamo yao hiyo kwa kuhofia kushughulikiwa.

Pamoja na hayo, suala la Kanda fulani kutotendewa haki katika mazingira fulani ya kiutawala nalo ni moja ya sababu ya mpasuko huo.

Ni suala la muda kishindo cha mpasuko huo waja.
 
Haya mambo yapo kila wakati. Wakati wa awamu ya 5 pia kuna ambao hawakupendezwa na jinsi serikali ilivyowakumbatia wamachinga. Kuna waliosema wazi wazi kwamba serikali inajiundia bomu na muda wa kulipuka ukifika hakuna anayeweza kuzuia.

Amekuja kiongozi mwingine anayejeribu kunyoosha na kusahihisha mambo japo kachelewa lakini wanajitokeza watu na ku- challenge. Kuhusu mambo ya ukanda, hayo ndiyo ya kawaida kabisa. Kiongozi asipotoka katika makabila fulani basi jamii hizo kwa sababu mbali mbali huona kuwa zimesahaulika, cha muhimu na chenye manufaa ni kuwa mambo haya yote ni kwa faida ya nchi yetu.

Aliyetaka kuwasaidia wamachinga alifanya kwa lengo zuri pamoja na mapungufu yake yote. Anayerekebisha ufanyaji wa biashara za kimachinga naye anafanya kwa manufaa ya nchi yetu. La muhimu kwa watanzania tujifunze kusikiliza kwa makini maelekezo ya viongozi, tumekuwa hodari wa kulaumu na kukosoa kila jammbo
 
Ungesema kuna mnyukano wa wabunge waliopitishwa na hawakushinda kura za maoni ungeeleweka.

Machinga:
Machinga ni mchuuzi anaetembeza biashara akiwa amezishika, hawa wanaojenga mabanda ya chuma juu ya mitaro na kuziba njia ni wafanyabiashara.

Kiufupi machinga walidekezwa sana,

Wakaaminishwa ni wanyonge,

Akajinasibu ni mtetezi wa wanyonyonge.

Kumbe mnyonge au maskini ni mtu mjinga,

Maskini hununulika

Mungu hampendi maskini,

Alie nacho ataongezewa na asie nacho hata kile kidogo atanyang'anywa.
 
asilimia kubwa ya wabunge wa CCM hawapendezwi mno na namna zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yao ya sasa linavyofanyika lakini hawataki kuonyesha misimamo yao hiyo kwa kuhofia kushughulikiwa.
usitegemee lolote jipya toka kwa wabunge wa CCM, kila mtu ni kufa lwake.
 
Hakuna mpasuko wala mnyukano. Kwanza wewe hata kwenye kamati kuu ya CCM haupo wala hauna wadhifa uko. Wewe utakuwa mmiliki wa kibanda cha mbao kilichokuwa juu ya mtaro wa maji pembezoni mwa barabara. Hapa unajaribu kutia taharuki. Leo hii wabunge wa CCM wawe na uchungu na raia? Imeanza lini
 
Ungesema kuna mnyukano wa wabunge waliopitishwa na hawakushinda kura za maoni ungeeleweka.
Machinga:
Machinga ni mchuuzi anaetembeza biashara akiwa amezishika,,, hawa wanaojenga mabanda ya chuma juu ya mitaro na kuziba njia ni wafanyabiashara.
Kiufupi machinga walidekezwa sana,
Wakaaminishwa ni wanyonge,
Akajinasibu ni mtetezi wa wanyonyonge.

Kumbe mnyonge au maskini ni mtu mjinga,
Maskini hununulika
Mungu hampendi maskini,
Alie nacho ataongezewa na asie nacho hata kile kidogo atanyang'anywa.
Alienacho ataongezewa na asie kuanacho hata kile kidogo anachodhaniwa kua nacho atanyang'anywa...
 
Ni suala la muda tu.

Kuna sintofahamu kubwa mno ndani ya CCM baina yao na mbaya zaidi ni mpasuko uhusuyo Kanda na namna ambavyo machinga wanavyotendwa.

Ikumbukwe, asilimia kubwa ya wabunge wa CCM hawapendezwi mno na namna zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yao ya sasa linavyofanyika lakini hawataki kuonyesha misimamo yao hiyo kwa kuhofia kushughulikiwa.

Pamoja na hayo, suala la Kanda fulani kutotendewa haki katika mazingira fulani ya kiutawala nalo ni moja ya sababu ya mpasuko huo.

Ni suala la muda kishindo cha mpasuko huo waja.
Maccm hata wangeuana wote kwangu mimi poa tu kwani ni zaidi ya ibilisi
 
Ni suala la muda tu.

Kuna sintofahamu kubwa mno ndani ya CCM baina yao na mbaya zaidi ni mpasuko uhusuyo Kanda na namna ambavyo machinga wanavyotendwa.

Ikumbukwe, asilimia kubwa ya wabunge wa CCM hawapendezwi mno na namna zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yao ya sasa linavyofanyika lakini hawataki kuonyesha misimamo yao hiyo kwa kuhofia kushughulikiwa.

Pamoja na hayo, suala la Kanda fulani kutotendewa haki katika mazingira fulani ya kiutawala nalo ni moja ya sababu ya mpasuko huo.

Ni suala la muda kishindo cha mpasuko huo waja.
huo ni unafki wa kiwango cha lami peleka ujinga wako kule bavicha
 
Ni suala la muda tu.

Kuna sintofahamu kubwa mno ndani ya CCM baina yao na mbaya zaidi ni mpasuko uhusuyo Kanda na namna ambavyo machinga wanavyotendwa.

Ikumbukwe, asilimia kubwa ya wabunge wa CCM hawapendezwi mno na namna zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yao ya sasa linavyofanyika lakini hawataki kuonyesha misimamo yao hiyo kwa kuhofia kushughulikiwa.

Pamoja na hayo, suala la Kanda fulani kutotendewa haki katika mazingira fulani ya kiutawala nalo ni moja ya sababu ya mpasuko huo.

Ni suala la muda kishindo cha mpasuko huo waja.
Kanda ndio kitu gani?! Inaamana mtu anapokosea tunaangalia kanda au tunaangalia sheria inasemaje?!

Hebu tusiwe na mijadala ya upotoshaji na kukosa hoja zenye logic.

Ni nani anafurahia uchafu wa mabanda na mrundikano wa mabanda maeneo ya mijini.

Machinga sio ajira rasmi ni kujitafutia kimagumashi ila sio ajira ya kudumu wala halali tukifuata sheria kali zaidi.
 
Kila mtu ana haki ya kujitafutia riziki kwa njia halali hivyo ni jukumu la serikali kuwatafutia machinga maeneo sahihi ya kufanyia shughuli zao sio wanasubiri hadi uchaguzi unapokaribia ndio wanaanza kuwathamini. Huo ni unafiki.
 
Ni suala la muda tu.

Kuna sintofahamu kubwa mno ndani ya CCM baina yao na mbaya zaidi ni mpasuko uhusuyo Kanda na namna ambavyo machinga wanavyotendwa.

Ikumbukwe, asilimia kubwa ya wabunge wa CCM hawapendezwi mno na namna zoezi la kuwaondoa machinga katika maeneo yao ya sasa linavyofanyika lakini hawataki kuonyesha misimamo yao hiyo kwa kuhofia kushughulikiwa.

Pamoja na hayo, suala la Kanda fulani kutotendewa haki katika mazingira fulani ya kiutawala nalo ni moja ya sababu ya mpasuko huo.

Ni suala la muda kishindo cha mpasuko huo waja.
Pale lumbumba CCM hawtaki raia apaki gari lake Machinga auze so huo mpasuko upi tena? walifanya figisu hadi msomali alifunga hotel yake iliyokuwa inajaza watu na magari hadi lumumba wakafunga barabara wakaibomoa kisha wakapiga stop kujenga hadi msomali akahamisha biashara yake ndio barabara ikajengwa lami.. Machinga tatizo lao hata wao kwa wao wanasemana kuwa ilikuwa too much so wacha kwanza wapungue haswa wenye uwezo wao na wale waliofunga maduka yao wawe machinga kisha watatruhusiwa kwa utambuzi rasmi sio mtu anakuwa tajiri and then anaendelea kuwa Machinga no no no... na umachinga sio kujenga mabanda machafu machafu eneo lolote tu la wazi hadi kwenye maduka ya wanaolipa kodi
 
Back
Top Bottom