Kuna mambo mengi sana tusiyofahamu kama wanadamu

Kuna mambo mengi sana tusiyofahamu kama wanadamu

Mayu umeandika vizur kuhusu IMANI na FACTS(Uhalisia).
Nisijikite huku.

Mm nina amini Uchawi upo.
Na hapa nataka niliongelee kwa kufikiria kwamba Mungu na Shetani hawapo.

Uchawi ni maarifa ya kitaalam ambayo baadhi ya binadamu hutumia kufanya jambo baya au zuri.
Kwa kutumia aina ya mimea au bidhaa nyingne kwenye kufanikisha jambo ambalo ni gumu kufanyika kwa hali ya kawaida.

Ni jambo la asili. Na kwakuwa chanzo chake bado watu hatufaham vizur bas ndio maana tunahusisha na Mungu.
(Maana vitu vyote vyenye nguvu ya asili ambayo bado hatufaham tunasema ni Nguvu ya Mungu).

Uchawi unaweza kuwa Hasi au chanya.
Mtu akilogwa na kudhurika tunasema ni uchawi. Ila tunasahau kuwa hata mtu akienda kwa mganga na kupewa dawa za mitishamba kukigwa na huo uchawi na mambi mengine kuwa ni Uchawi pia.

Uchawi ulikuwepo hata zaman sana kabla ya Yesu na Mtume.

Hadithi zinasema Mussa alishindana na Wachawi wa Farao.

Ukiangalia kwa muktadha huu. Basi bila shaka Uchawi upo.
Maana uchawi sio kulogwa tu.
Mkuu ni sahihi kabisa ulivyokiri UNAAMINI

HAKUNA namna yoyote unaweza KUTHIBITISHA uchawi upo zaidi ya hadithi za kuhisi au kusikia kwa wengine
Kama watu wanajifunza na wanajua huo uchawi iweje ushindwe kuthibitika?
Unajifunzaje kitu hakithibitiki?

Piga selfie leo jioni uko kwenu Namtumbo watu wakuhuhudie kisha paa naungo wako mafichoni kisha ibukia USA kapige selfie uko na Roma mkatoliki........ Simple tu

Mitishamba sio UCHAWI ni Sayansi mkuu.
Nikikupa mti wenye sumu ukadhurika au mizizi yenye ingredients zinazoua wadudu wa Malari ukapona huo sio uchawi ni pure science
 
Fact umeongelea katika very narrow sense. Fact inaweza kuwa social fact, hii inapatikana pale ambapo imani yetu remained unchallenged any more... yani pale ambapo hakuna pingamizi juu ya ile imani yetu. Hapo ndipo tunaamini kuwa hiki kitu ni kweli na kipo. Uchawi ni spriritual realism na sio empirical evidenced

Shida ya Spiritual, hazina standard ya kuonekana kuwa kweli kwenye vigezo vya empiricism yani sense through observe, feeling, smell or hearing. Kwa muktadha huo sasa mambo ya spirit ikiwemo uchawi inabaki kuwa personal. Yani kukubali upo mpaka ukutane nao. So kuwepo kwa uchawi sio tena universal truth. Lakin kuna dhana nyingi sana znaelezea sayansi hii ya uchawi(occult), unajimu au elimu nyota (astrology) na utabiri (palmistry).
Mkuu FACT ni mambo unayoyafanya kila siku kwenye kuendesha maisha yako.
Fact ni lojiki/sayansi.
Hakuna supernatural yoyote inayoendesha maisha yetu kama ilivyo kwa viumbe wengine.
Wewe na nyani au Simba au samaki baharini hatuna tofauti yoyote kwenye kutumia FACT kuendesha maisha yetu....... Tunacho wazidi ni kwamba sisi tuna maarifa makubwa zaidi yao.

Haya mambo ya supernatural ni mambo ambayo binadamu kayatengenezea nadharia kwasababu ya udadisi wake tu..... HAYAPO
 
Je unadhani ni kwanini uchawi una exist pia kwanini nchi nyingi za Africa zenye maendeleo duni hazijaweza kutumia uchawi kutatua changamoto zilizopo?
Mkuu ukisoma historia enzi hizo Ulaya imani za uchawi zilikua kubwa mno Afrika tunasingizia tu

Lakini sasa wenzetu walikwisha kubaini kitambo hizo ni porojo tu na wamejikita kwenye SAYANSI, wapo wachache ambao bado wana fantasize hizo ngonjera lakini sisi Afrika bado watu wanaziamini.
 
Cha kushangaza sayansi haiamini uchawi ila inakubali na kutumia hypnosis na hypnotherapy, inamini brainwaves frequency kwenye relaxation, wakati hivyo vitu na uchawi vina ukaribu mkubwa mno kwa kuwa vyote vinatumia frequency, wachawi wanatumia maneno yao maalum (chants), wanatumia nyimbo na ngoma ambavyo vyote ni aina ya frequency, wanasayansi wanachagua wao aina gani ya frequency kisha wanaipa title ya facts na nyingine zinakuwa spiritual
Mkuu proof is everything

Ukiwaambia wanasayansi wa prove matokeo ya hizo frequency zinavyofanya kazi wata kupa UTHIBITISHO pasi na shaka ya zaida

Waambie sasa hao wachawi wakupe huo uthibitisho uone kama utapewa zaidi ya ngonjera na mikingamo kibao
 
Kuna one issue ambayo mpaka sasa najiuliza kuna baadhi ya actions ambazo wengi wetu tunashuhudia hata hapa. For example, kuna watu wanaweza kutabiri kitu exactly as it happens, bila hata kujua details(manabii na hata zamani walikuwepo), sometimes even mentioning names or specific events za future. But based on science, some people explain this as time travelling or something similar.

The same applies kwenye uponyaji for instance, tukichukua wagonjwa 100 kutoka Muhimbili Hospital, tukawapeleka kwenye baadhi ya makanisa fulani you'll find that kuna asilimia ya watu watakaopona kwa Imani sudenly , even doctors can’t explain it. Na vipimo vinaonyesha wagonjwa hao ni wazima kabisa.

So my question ni kwamba, why shouldn’t we trust in religion or prayers if such things have been proven to work, or is it just that science hasn’t yet found an explanation for them?

Since Imani ni proven to some people, why not calling it facts. Maana ya fact ni kitu Cha kweli sio Cha kudhaniwa mtu kapona it's a factual thing.
Mkuu tatizo lako unasumbuliwa na IMANI
Na changamoto kubwa ya imani ni kwamba haitaki matumizi sahihi ya akili

Kwanza UNAAMINI hekaya za kale za vitabu vinaitwa eti vya Mungu, huko ndio unatumia rejea kwamba kuna watu walitabiri vitu vikatokea kama vilivyo?

Pili UNAAMINI uchawi na majini kwamba akina Shekh Yahaya wakisema mwaka huu atakufa mtu maarufu na akafa kweli unaona utabiri umetimia?
Hivi kweli mwaka mzima wasife watu mashuhuru duniani kote?

Au mtume na nabii fulani akitabiri Yanga atakua bingwa Tz au Psg Ufaransa unaona maajabu kweli?

Hebu nipe utabiri ulio kushangaza kabisa ukaona huu kweli kiboko

Mkuu kama kweli huwa UNAAMINI wale wanaotoa ushuhuda kwenye makanisa Live kwenye tv kwamba wamepona basi una safari ndefu sana kwenye huu utumwa wa kikoloni tulioletewa na waliokuja kupora mali zetu na kutufanya watumwa
 
Mkuu sioni chochote alicho TABIRI hapo labda unifafanulie kiingereza kinanipiga chenga 🤣

BTW huyu sio ndio alitabiri Chelsea itashinda UCL na haikushinda? Akakanusha
Huyu si ndio alotabiri Lowassa atashinda Urais na akashindwa? Akakanusha

Mara nyingi hizo zinaitwa tabiri za Tb Joshua zilikua zinatengenezewa nadharia tu kulingana na mahubiri yake ya awali.
Na tabiri alizotabiri na hazikutokea hutengeneza nadharia pia kukanusha kwamba hakumaanisha hivyo

Anacheza na akili za waaminio tu
 
Ndugu watabiri wapo wengi na hata science yenyewe inakubali kuhusu utabiri
 
Ndugu watabiri wapo wengi na hata science yenyewe inakubali kuhusu utabiri
Mkuu hata mimi huwa NATABIRI sana kwenye Betting na sometimes napatia sometimes nakosea...........Hakuna maajabu yoyote

Kwenye sayansi kuna kitu kinaitwa PROBABILITY, kwenye sayansi hàkuna utabiri wa 100% kama mnavyo AMINI watu wa IMANI kwamba mpiga ramli au nabii anaweza kutabiri 100% kwa kila anachotobiri

Ukweli ni kwamba watabiri wanatumia probability/possibility KUTABIRI jambo
 
Samahani, je Mungu yupo au hayupo?
Ni kitu gani kinakufanya usiamini?
Je, unadhanani mtu ambae ameshuhudia muujiza maishani make akiamini anakosa gani?
 
Nimekuelewa vizuri ndugu, but why does religion always seem to be connected to supernatural things? For example, mtu akisemekana kalogwa, it's considered a supernatural act na kisababishi ni uchawi so kwanini huyo mtu akiombewa, ana recover(kupona), na wengi tumeshuhudia haya?

Also, kuhusu Sheria za nchi je Hatuwezi kuishiwe peacefully and morally bila dini but under national laws and regulations? For instance, China wana many atheists yet it’s serekali yao inaweza kuwa control vizuri na pia ni nchi iliyoendelea.
Soma kitu kinaitwa "Placebo effect" pia.
 
Juzi nilikuja na mada ya "Je, uchawi upo?"

Kwa kufikiri kwa kutumia logic na mtazamo wa kisayansi, tunaweza kusema uchawi haupo, bali ni fiction hasa kutokana na story nyingi za uongo tunazozisikia kutoka kwa watu mbalimbali.

Lakini nilikaa nikajiuliza, je, kuna mambo kama mapepo? Baadhi ya watu hata ndugu zetu wanaonekana kuwa na hali hizo, na mara nyingine hujitokeza kwa kulipuka au kupoteza fahamu wanaposikia kile kinachodhaniwa kuwa ni Neno la Mungu. Je hii issue ya mapepo kama hamna nguvu ya ajabu kwanini kuwe nayo na kwanini hutokea watu wenye akili timamu kabisa?

Nikaanza pia kuwaza kuhusu mambo ya mysterious ways yanayotokea. Kuna hali ambazo watu hudai wamelogwa lakini hupata uponyaji kupitia maombi au hata kwa kutumia kinachojulikana kama ushirikina. Mimi mwenyewe nimeshuhudia watu wakipona live. Why so if we don't have such power?

Kuna pia watu wanaotabiri mambo, na viumbe vya ajabu kama kakakuona. Kwenye mtazamo wa kisayansi, wengine hudai kuwa ni suala la time travelling, lakini sayansi bado haijafanikiwa kufafanua undani zaidi wa mambo haya.

Nilipochunguza upande wa dini, nilijaribu kutafuta ukweli kupitia makanisa mbalimbali. Nikajiuliza: kwa nini katika baadhi ya makanisa watu huanguka au "kulipuka" zaidi wakati wa maombi yenye kelele na muziki mkubwa, lakini kwenye makanisa yenye maombi ya utulivu hakuna hali kama hizo? Pia kwanini itokee kijiografia isitokee kwa wachina, wahindi, wakorea, wajapani?

Kisha nikajiuliza swali kuu Kwa nini tupo duniani?
Je, kusudi la sisi kuwepo ni nini? Maana asilimia kubwa ya maisha ya mwanadamu yamezungukwa na changamoto iwe ni kilimo, biashara, umaskini, elimu, afya, au kazi nyingine zote zipo kwa lengo la kutatua changamoto fulani. Hivyo, je, tulikuja duniani kwa ajili ya kutatua changamoto tu na kuonana na matatizo, au kuna kusudi jingine kubwa zaidi ya sisi kuwa hapa?

Pia nashangaa, kwa nini Mwenyezi Mungu alimtoa kafara mwana wake wa pekee kwa ajili ya wanadamu, lakini akamwacha Shetani aendelee kuishi? Kwa nini hakumuangamiza kabisa ili vizazi vyote vikombolewe? Ni kama vile unaua watu wasio na hatia badala ya majambazi waliotenda uovu.

Na mwisho, kwa nini tunaomba kama kila kitu tayari ni mpango wa Mungu? Kama kila jambo limepangwa tangu mwanzo, kwa nini tumshawishi abadilishe alichokipanga?
Upo ili ufe
Maisha sio mchezo WA uwoga mjomba
Unataka shibe hakikisha haukombi mboga.

Religion ni Imani
Science ni Fact
 
Ukijua kutengenisha kati ya IMANI na FACT basi haya mambo hayatakupa shida sana.

Yes ni kweli binadamu hajui mambo mengi sana kuhusu huu ulimwengu, maybe tunajua 0.001% ya huu ulimwengu

Mambo tunayo yajua na tunaweza kuyathibitisha tunayaita FACT

Mambo ambayo Hatuyajui tunabuni na kutunga tunayaita IMANI

Changamoto ni pale tunapoishi kwa kutumia FACT lakini tukiamini ni IMANI inayotuwezesha

Mfano mtu anafanya kazi akipata hela anaamini ni MUNGU kampa RIZIKI
Akiumwa anaamini Shetani akitumia dawa akapona anaamini Mungu kamponya

Unazungumzia Makanisa kwasababu makuzi yako yamekufanya UAMINI dunia nzima wana makanisa na kuabudu kama unavyo abudu wewe
Ukienda China kuna watu hawajui hata kama kudini zingine zidi ya mabudha yao na wana maisha bora kabisa kuliko walokole wanaokesha makanisani Afrika na Waislam wanaoswali swala tano Somalia au Sudan

Kwa bahati mbaya sana haya mambo ya IMANI wenzetu walio endelea wameacha kuyapa kipaumbele kwenye maisha yao ya kila siku, imebaki kama tamaduni na fantasy tu za baadhi ya watu

Lakini huku kwetu dunia ya tatu IMANI ndio kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yetu
Kila kitu tunaamini Mungu atafanya tukimuomba kwa bidii

Israel wanajilinda kwa iron dome na kila silaha za hali ya juu lakini sisi tunaamini tunalindwa Mungu wa Israel.

Israel ni kame na wanageuza maji ya bahari kuwa baridi kumwagilia mashamba wakati sisi mvua ikigoma tunajazana makanisani kumuomba Mungu wa Israel atupe mvua.
Mkuu kula kitimoto na ndizi mbili nalipia
 
Mayu umeandika vizur kuhusu IMANI na FACTS(Uhalisia).
Nisijikite huku.

Mm nina amini Uchawi upo.
Na hapa nataka niliongelee kwa kufikiria kwamba Mungu na Shetani hawapo.

Uchawi ni maarifa ya kitaalam ambayo baadhi ya binadamu hutumia kufanya jambo baya au zuri.
Kwa kutumia aina ya mimea au bidhaa nyingne kwenye kufanikisha jambo ambalo ni gumu kufanyika kwa hali ya kawaida.

Ni jambo la asili. Na kwakuwa chanzo chake bado watu hatufaham vizur bas ndio maana tunahusisha na Mungu.
(Maana vitu vyote vyenye nguvu ya asili ambayo bado hatufaham tunasema ni Nguvu ya Mungu).

Uchawi unaweza kuwa Hasi au chanya.
Mtu akilogwa na kudhurika tunasema ni uchawi. Ila tunasahau kuwa hata mtu akienda kwa mganga na kupewa dawa za mitishamba kukigwa na huo uchawi na mambi mengine kuwa ni Uchawi pia.

Uchawi ulikuwepo hata zaman sana kabla ya Yesu na Mtume.

Hadithi zinasema Mussa alishindana na Wachawi wa Farao.

Ukiangalia kwa muktadha huu. Basi bila shaka Uchawi upo.
Maana uchawi sio kulogwa tu.
Uchawi ni kama Maarifa Fulani, tuko sawa? Huenda uko sahihi japo Kuna ukakasi
 
Samahani, je Mungu yupo au hayupo?
Ni kitu gani kinakufanya usiamini?
Je, unadhanani mtu ambae ameshuhudia muujiza maishani make akiamini anakosa gani?
Mkuu mimi sitaki habari ya KUAMINI........ Mimi nataka KUJUA kama Mungu yupo.
Kuna Miungu zaidi ya 1000 Duniani na kila dini inakazi ya kuaminisha Mungu wake yupo na ndio Mkuu.
Wewe kama unaweza kunifanya nimjue Mungu itakua vyema....... Sio kuniaminisha
So far nimejiridhisha HAYUPO.

Miujiza ni nini kwanza? Maana mtu wa IMANI hata akipona kwenye ajali mbaya ataita MIUJIZA...............Lakni mimi nitaona ni coincidence tu lakini kwenye imani utaita miujiza mkubwa

Be specific ni miujiza gani wewe umewahi kuona? Au umefantasize na hekaya za miujiza ya walokole eti "nilichukuliwa usiku kimazingara na wachawi tukawa tunakula nyama za watu makàburini" 🤣🤣🤣
 
ulipata majibu gani kuhusu makaniaa ya mziki mkubwa watu kuanguka mapepo na ya slow kuwa safe?
 
Mkuu ni sahihi kabisa ulivyokiri UNAAMINI

HAKUNA namna yoyote unaweza KUTHIBITISHA uchawi upo zaidi ya hadithi za kuhisi au kusikia kwa wengine
Kama watu wanajifunza na wanajua huo uchawi iweje ushindwe kuthibitika?
Unajifunzaje kitu hakithibitiki?

Piga selfie leo jioni uko kwenu Namtumbo watu wakuhuhudie kisha paa naungo wako mafichoni kisha ibukia USA kapige selfie uko na Roma mkatoliki........ Simple tu

Mitishamba sio UCHAWI ni Sayansi mkuu.
Nikikupa mti wenye sumu ukadhurika au mizizi yenye ingredients zinazoua wadudu wa Malari ukapona huo sio uchawi ni pure science
Uchawi hauthibitiki kwa sababu ya kuhitajika uthibitisho wa kisayansi kitu ambacho kwa sasa hakuna vifaa vyenye kuweza kutumika kuthibitisha uchawi katika misingi ya kisayansi. Hata meditation pia huko mwanzoni watu walipinga faida ya meditation maana hakukuwa na ushahidi wa kisayansi hadi baadaye vilipopatikana vifaa vya kisasa vilivyotumika na kuweza kupatikana ushahidi wa kisayansi juu ya faida za meditation.

Chukua mfano hiyo mitishamba ambayo imeanza kutumika kabla hata ya maendeleo katika sayansi watu walijua mmea fulani unatibu ugonjwa fulani na baadaye sayansi inakuja kuthibitisha baada ya kufanyika utafiti wa kisayansi, hivyo ndio ilivyo na hata sasa bado kuna watu hawaamini kabisa kwenye tiba za mitishamba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom