Kuna mambo huwezi kujifunza ukubwani

Kuna mambo huwezi kujifunza ukubwani

kwa leo napenda kuzungumzia swala la kizazi cha leo kukosa maadili ,sio kwamba ni kuiga ni jinsi watoto wanavolelewa kwenye familia watoto wa siku hizi wanafanyiwa kila kitu na beki tatu,haishangazi mtoto yupo chuo kikuu hata kupika hajui kila kitu anafanya beki tatu.

Nakumbuka mimi nilianza kupika nikiwa darasa la pili,wakati huo nilikuwa naenda shuleni saa tano ,nilikuwa na miaka nane nilikuwa mchana kabla ya kuondoka lazima nipike ugali ,nioshe vyombo,nifagie nje ,nideki nyumba jmosi nayo tunafua nguo za kushindia zile

Nzuri za kanisani au kwendea mtoko,hosptal alikuwa anafua mama au dada wakubwa.
kwa sasa hivi mtoto wa miaka nane hata chakula analishwa atii.kuna mtoto wa sister niliachwa nae sister alienda kusoma alikuwa darasa la tatu tena genious tu class anakuwa wakwanza ila ilikuwa inabidi nimuogeshe maana hata kuoga ilikuwa shida.
watoto wa siku hizi wakubwa tu washavunja na ungo hata kupika chai tu ni kazi hawajui maana kwao kila kitu ni beki tatu.

Ubaya ni kwamba kuna vitu ni vigumu sana kujifunza ukubwani mojawapo ni mapishi japo kuna shule za mapishi nyingi tu ila kama hujazoea jiko hata ujifunze vipi hutoweza kupika chakula kizuri.

Ukitaka ujue mapishi lazima uwe muhenga wa jikoni.kuna vitrick vingi sana ambavo unajifunza kwa uzoefu na sio darasani tuanze kuwatrain watoto wetu ni kwa manufaa yao
Miss Natafuta katika ubora wako.... Ni kweli kabisa
 
Wote kwa pamoja... wife kila awapo na wasaa lazima anionjeshe ladha adhimu ya mikono yake... Good thing anajua akinipikia hata asiponiambia lazima apate sifa zake kwani najua hata kwa harufu.. Yupi mwanamke asiyependa sifa ya mumewe???? Unalo jibu miss.. Mabinti bado wadogo ila sina hofu na baadae yao kwani mimi mwenyewe fundi hivyo wasipoiga kwa mama watanikuta mimi japo mara moja moja...

Sent using Jamii Forums mobile app
hata kama ni wadogo unawaambia hata watwange vitunguu swaumu mkuu.
 
Sio kujua kupika wengine wanapolala ni shida. Bora mtu usijue kupika, uwe msafi jamn mtu unaingia kwa mtu hodi unapokelewa na jungu la ugal liko mlangon yote ni malez mabaya

Wamama wa zaman walikuwa bora, kwa kupata elimu bora ya nyumban Kutoka kwa wazaz wao.
mtu anapika ugali hata mwiko haoshi
 
Elimu haina mwisho. Mimi binafsi nilikuwa sifanyi kazi yoyote nyumbani, nimetoka nyumbani sijui kupika wala kufua, ila nilijifunza mbele kwa mbele sasa hivi unaweza kufikiri nimesomea upishi.
[emoji102] [emoji101] mmh
 
karibu muhenga mwenzangu wa jikoni najua ukiingia tu jikoni chungu kinajiivisha chenyewe
Mie namshukuru sana mama yangu, namuombea apumzike kwa amani, alinifundisha kupika hasa ugali. Ilikuwa nikipika ugali una kasoro anakwambia kasoro hiyo imetokana na nini wakati hata hakuwepo wakati ninasonga, mfano alikuwa anajua kasoro ambazo zimesababishwa na kuanza kupika ugali kwa moto hafifu halafu baadae ndio nikaongeza moto, ugali ambao uji wake ulikuwa mzito sana, ugali ambao nimesonga halafu nilivyoona umekuwa mgumu nikaongeza maji ya baridi na mengineyo mengi. Kipindi kile nilikuwa nachukia sana anavyonipelekesha lakini leo naona faida yake,
Hata nikila kwa mama lishe kama ugali una kasoro nawaambia huu ugali wenu sio mzuri na hii ni kutokana na sababu hii.......
Mwisho tuwafundishe watoto wetu kazi zote za ndani kuanzia kupika, usafi na mengineyo, tena hii ifanyike kwa watoto wa jinsi zote.
Vijana wa kiume ambao hawajui kupika wala kufua wanapata tatizo la kuoa haraka hata kama hajasimama vema ili tu apate mtu wa kufanyia hayo
 
hata kama ni wadogo unawaambia hata watwange vitunguu swaumu mkuu.
Noted mkuu, sema hii sayansi na teke linalokujia mambo mengi yanafanywa na vimashine...ila wana ushiriki mzuri wa idara hiyo na hata kufua na mengine... Utashangaa baadhi ya wazazi wanalaumu hili kundi limekuwa hovyo bila kufikiri wao ndio ovyo zaidi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo watu wa pwani tunasemwa Sana, ila acha kwenye maswala ya nyumban tunajua kujiongeza. Mtu aliyechezwa huwezi kuta mjinga mjinga Ndio maana sikuhiz watu wanapiga hela tu kuwafunda whatsapp vya Uongo na kweli mabinti wengi hawajui majukumu ya mwanamke nyumban, kupangilia mda, usafi, kupika, hekima, heshima wakat elimu hii unatakiwa upatiwee Bureee. Asante mama kwa kunifundisha.
 
Mie namshukuru sana mama yangu, namuombea apumzike kwa amani, alinifundisha kupika hasa ugali. Ilikuwa nikipika ugali una kasoro anakwambia kasoro hiyo imetokana na nini wakati hata hakuwepo wakati ninasonga, mfano alikuwa anajua kasoro ambazo zimesababishwa na kuanza kupika ugali kwa moto hafifu halafu baadae ndio nikaongeza moto, ugali ambao uji wake ulikuwa mzito sana, ugali ambao nimesonga halafu nilivyoona umekuwa mgumu nikaongeza maji ya baridi na mengineyo mengi. Kipindi kile nilikuwa nachukia sana anavyonipelekesha lakini leo naona faida yake,
Hata nikila kwa mama lishe kama ugali una kasoro nawaambia huu ugali wenu sio mzuri na hii ni kutokana na sababu hii.......
Mwisho tuwafundishe watoto wetu kazi zote za ndani kuanzia kupika, usafi na mengineyo, tena hii ifanyike kwa watoto wa jinsi zote.
Vijana wa kiume ambao hawajui kupika wala kufua wanapata tatizo la kuoa haraka hata kama hajasimama vema ili tu apate mtu wa kufanyia hayo
ahahaa shogangu na wewe ulikuwa hujiongezi unaongeza tena maji baridi kwenye ugali? aahaaa ulikuwa unatokaje na harufu ya ubichi? mimi nilifundishwa na ile style ya kurusha ugali ukutani kucheki kama umeiva .weee yaani hadi nimalize kusonga ugali robo nzima ipo ukutani huko ahaaa
ila pole sana kwa kumpoteza mama yetu.Mwenyenzi Mungu ampe mapumziko mema peponi amen!
 
Muhimu ukubali kujifunza. Tena ukijifunza ukubwani unakuwa huru zaidi kujaribu vitu mbalimbali.
hatukatai kujifunza dear ila haiwi nzuri kama ukijifunza utotoni.halafu wewe ni wa kiume bwana kuna tofauti
 
Japo watu wa pwani tunasemwa Sana, ila acha kwenye maswala ya nyumban tunajua kujiongeza. Mtu aliyechezwa huwezi kuta mjinga mjinga Ndio maana sikuhiz watu wanapiga hela tu kuwafunda whatsapp vya Uongo na kweli mabinti wengi hawajui majukumu ya mwanamke nyumban, kupangilia mda, usafi, kupika, hekima, heshima wakat elimu hii unatakiwa upatiwee Bureee. Asante mama kwa kunifundisha.
pwani wenzetu mpo juu hadi kugegedana mnafundishwa natamani ningezaliwa pwani maana kitandani sijui lolote
 
ahahaa shogangu na wewe ulikuwa hujiongezi unaongeza tena maji baridi kwenye ugali? aahaaa ulikuwa unatokaje na harufu ya ubichi? mimi nilifundishwa na ile style ya kurusha ugali ukutani kucheki kama umeiva .weee yaani hadi nimalize kusonga ugali robo nzima ipo ukutani huko ahaaa
ila pole sana kwa kumpoteza mama yetu.Mwenyenzi Mungu ampe mapumziko mema peponi amen!
haahahaha, mie nilikuwa mvivu, nilikuwa sipendi kufanya kazi hivyo akawa anakomaa na mimi.
Hiyo ya kurusha ugali ukutani bibi yangu alikuwa ana i discourage yaani akiona tu umerusha anakufinya, halafu hata ya kusonga ugali halafu ugonga surufia ,kuuuuuuuuuuuuuuutu, kuutttttttttttttttttttuuuuuu na yenyewe alikuwa anatukaza, anasema usonge ugali kwa staha sio ugomvi.
Ahsante mwaya kumuombea mama yangu dua njema.
 
Mi niliambiwa samaki mkunje angali mbichi nikabisha kumbe akikauka ukimkunja tu anavunjika hapo huu msemo una maana sana
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom