Tusichanganye lack of sense of humor, intro na ukauzu.
Ukauzu ni lifestyle fulani iliyopandishwa umaarufu na uwepo wa makundi kama Walume ndago, TMK Wanaume, TMK majita na East Coast Team. Kwa kuwaona East Coast wakishua TMK Wanaume wakajiundia personality ya ukauzu ambayo ni haijali kama haijaoga wiki nzima, haijali kama mavazi ni machafu na kua tayari kwa ugomvi.
Mtu alikua anajitamba yeye ni kauzu zaidi ya dagaa akimaanisha haoni aibu wala hahofii macho ya watu kwa atakachotaka kukufanyia au kwa jinsi alivyo.
Watu hawa walikua na kausemi ka "Mi gangstar" ukimuuliza mbona shati chafu jibu lake "Mi gangstar nimhofie nani? Mwenzako mi kauzu"
Anyway, haya makundi kufifia kulienda sambamba na hilo neno kauzu na personality yake. Nina uhakika hamna ambaye hili neno limekatiza akilini mwake mpaka alivyoliona hapa na hata ulivyolisoma cha kwanza kukumbusha ni dagaa na siyo personality.