Kijana usidharau vijiwe vya kahawa kuna madini mengi sana pale

rajiih

JF-Expert Member
Apr 4, 2019
477
714
Wana Jf kwa mara nyingine tena mwezi huu wa Pili nmeamua kuanzisha Threads hii ya kuhusu vijiwe vya KAHAWA kwa sababu ambazo zina faida nyingi kuliko hasara.

Kwa muda sasa nilijiapiza kuzoea katika ya vijiwe vya kahawa ambavyo vitakua Jirani yangu au hata nikiwa katika safari ya ugeni ambao itanihitaji Mwenyeji ili kupafahamu zaidi eneo husika, Na hizi ni baadhi ya niliyogundua katika vijiwe hivi.

1. Kila mtu wa sekta zote anaweza kuwa mahali hapa nikimaanisha WATU WA SERIKALI, WALALA HOI na watu wa KIBINAFSI hii ni zaidi ya Faida maana hapa kila mtu akiguswa katika sekta yake anao Muda wa kuelezea kilichokua sawa na kisicho kuwa sawa kwa wakati mmoja na nyinyi mkabaki mnamsikiliza kwa uzuri kabisa.

2. Ukiachana na uongo wa vijiwe hivi vya Kahawa pia kuna Faida muhimu sana ya kujifunza kama kijana Msomi na Kiongozi wa baadae nayo ni KUJIAMINI katika kile unachokizungumza wakati huo, Haijalishi ni cha Uongo au Kina ukweli ndani yake wana Jf sio masihara kuijenga hoja na kuitetea kwa wakati mmoja nadhani wengi tunafahamu hili na limekua tatizo kwa walio wengii tu kiasi kuleta shida katika Kazi zao.

3. Kuna baadhi ya taarifa Nyeti iwe za Nchi au Viongozi wa Nchi na hata makampuni ya kibinafsi huwa zinaanza kuvuja huku katika vijiwe hivi na mara nyingi vinakuja kutokea kweli au zinakua ni taarifa za ukweli hata kama zitatoka kwa kucheleweshwa ila kama mwanachama wa vijiwe hivi unakua ushatambua kitambo tu.

4. Wana Jf yako mengi sana katika vijiwe hivi ukitaka wabobezi wa biashara yeyote unayotaka kuifanya kwa mtaji wako huo huo ambao umekua ukikusumbua kichwa kwamba utaanzaje bhasi usipate shida we tembelea katika vijiwe hivi muhimu tu usiwe na haraka katika jambo lako linalokutatiza utafika tu wasaa wa kuzungumzia biashara nawe hapo hapo utapata upenyo wa kuomba ushauri japo huwezi kujidirect kabisa unaweza tumia hata Mtu fulani au mtu wako wa karibu kama ndio muhusika wa hiko anachotaka kwenda kukifanya.

5. Faida ya sehemu ngeni kwako hapa nikimaanisha hata Mikoani huko Mkuu usipate shida we tenga muda wako tu wa kutembelea vijiwe vya Kahawa hapa utapata taarifa zote ziwe za kijiji na hata viongozi ambao hawawajibiki ipasavyo katika majukumu yao hivyo kama utakua umeenda kwa ajili ya jambo fulani itakuwa rahisi kujua au kupata msaada wa haraka zaidi ambao utakuweka salama zaidi[ia utakua umeokoa muda wako.

AKILI YA KUAMBIWA ONGEZEA NA YAKO.....
Nawasilisha.
 
Ni kweli kwa kiasi kikubwa lakini inategemea na aina ya watu waliopo katika vijiwe hivyo...kama vijana ni wengi panakuwa pa hovyo

Ninachopenda katika vijiwe hivyo ni vile ambapo watu hawadharauliani na kama wakitoleana maneno ya dharau ni kwa utani tu

Kingine sio watu wote waliopo kwny hivyo vijiwe ni Walala hoi na Wasiosoma, Wapo wasomi, wenye maarifa mengi na Wenye pesa huko....so usijaribu kuwadharau kama huwajui...unaweza kujifunza mengi kutoka kwao
 
Jamiiforum ni kama kijiwe tu ,chai kahawa na vitafuno tunapata apa apa.
1705053263379.jpg
 
ni sahihi kabisa, ni vile wengi hatujui ila ni bora kukaa kwenye kijiwe cha kahawa kuliko kwenda baa, bichi, au kukaa nyumbani.
pia garama utakazo tumia kwenye kijiwe cha kahawa ni ndogo sana kulika na sehemu nyingine, pia hakuna kishawishi chochote kinachoweza kujitokeza kwenye kijiwe cha kahawa.

changamoto ni kwa wenzetu wanawake, kwa upande wao hamna vijiwe rafiki kwa kama sisi.
 
Back
Top Bottom