Kuna la kujifunza hapa kuhusu kuiga mambo

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Impact-of-Artificial-Intelligence-in-this-Changing-Railway-Industry.jpg


Katika kituo cha treni, kulikiwa na wahasibu watatu kila mmoja alinunua tiketi yake. Lakini waliwaona mainjinia watatu wakinunua tiketi moja tu.

Ikabidi mmoja wa wahasibu awaulize, "Nyie mpo watatu mtasafirije kwa tiketi moja tu?",

"Subiria utajionea mwenyewe", anajibu mmoja wa mainjinia.

Muda unafika na wote wanapanda treni. Wahasibu watatu wanaenda kukaa kwenye viti vyao, lakini mainjinia wote watatu wanaingia ndani ya choo na kufunga mlango.

Muda mfupi baada ya treni kuondoka, kondakta anaanza kupita kukusanya tiketi.

Anagonga mlango wa choo na kusema, "Tiketi tafadhali".

Mlango unafunguka kidogo na mkono mmoja unatoka umeshika tiketi mkononi. Kondakta anachukua na kuendelea kukusanya tiketi zake.

Wahasibu walipoona hivyo nao walikubaliana kuwa ni wazo la zuri sana. Baada ya mkutano kuisha, wanaamua kuwaiga mainjinia na kununua tiketi moja kwenye safari yao ya kurudi ili kuokoa pesa.

Wanafika kituoni, wananunua tiketi moja tu. Kitu kilichowashangaza zaidi safari hii, mainjinia hawakununua tiketi kabisa.

Mmoja wa wahasibu anauliza, "Mtasafiri vipi bila tiketi yoyote?"

"Subiria utajionea mwenyewe", mmoja wa mainjinia anajibu.

Kisha wote wanapopanda treni, wahasibu watatu wanaingia kwenye choo kimoja na mainjinia watatu wanaingia kwenye choo kingine kilicho karibu. Treni inaondoka.

Muda mfupi baada ya kuondoka, moja wa mainjinia anatoka chooni na kuelekea kwenye choo ambacho wahasibu wamejificha.

Anagonga mlango na kusema, "Tiketi tafadhali".

Mwisho.
 
Back
Top Bottom