Kuna la kujifunza hapa kuhusu heshima

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Mwanamke mmoja aliyekuwa anaitwa Nancy alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha kusambaza na kusaga nyama.

20231231_140046.jpg

Siku moja, baada ya kumaliza ratiba yake ya kazi, aliingia kwenye chumba cha baridi (friji) cha nyama ili kukagua kitu, lakini kwa bahati mbaya, mlango ulijifunga na akakwama ndani bila msaada.

Ingawa aliita kwa nguvu na kupiga mlango kwa nguvu zake zote, kilio chake kilisikika bila kusikilizwa kwani hakuna aliyeweza kumsikia.

Wafanyakazi wengi walikuwa tayari wameondoka, na nje ya chumba cha baridi, ilikuwa haiwezekani kusikia wala kuona kilichokuwa kinaendelea ndani.

Baada ya saa tano kupita, akiwa karibu kufa na amekata tamaa, hatimaye mlinzi wa kiwanda anafika na kufungua mlango.

Nanvy alinusurika kwa miujiza siku hiyo.

Alimuuliza mlinzi ilikuwaje akaja kufungua mlango, jambo ambalo halikuwa kawaida yake kufanya maama sio sehemu yake ya kazi.

Mlizi alieleza: "Nimefanya kazi kwenye kiwanda hiki kwa miaka 35, wafanyakazi wengi wanakuja na kuondoka kila siku, lakini wewe ni mmoja wa wachache wanaonigia na kunisalimia "Habari" asubuhi na kusema "Kwaheri" usiku unapoondoka baada ya kazi. Wengi ujifanya kama hawanioni.

Leo, ulipoingia kazi kama kawaida yako ulinisalimia "Habari", lakini jioni baada ya saa za kazi, niligundua kwa kushangazwa kwamba sikusikia "Kwaheri tutaonana kesho" kutoka kwako. Hivyo, niliamua kukutafuta kila mahali.

Ili nipate salamu yangu "Habari" na "Kwaheri", kwa sababu zinanikumbusha kuwa mimi ni mtu.

Kwa kutokusikia kwako kuaga leo, nilijua kuna kitu kilikuwa kimeenda hovyo. Ndio maana nilikuwa nikikutafuta kila mahali."

Kuwa mnyenyekevu, penda na heshimu wale wanaokuzunguka kamwe huwezi kujua kesho itakuletea nini.

Mwisho 😎

C & P FROM X
 
Hii ni stori maarufu sana.

Heshima ni muhimu ila siku za hivi karibuni anaeheshimiwa ni mwenye kitu tu.
Na hii hadi watoto wadogo wameirithi. Dogo anakutreat vile anaona wakubwa zake wanakutreat.

Kama baba/mama yake anakujigu hovyo, jua hata yeye atakujihu hovyo haijalishi umri wako.
 
Kabisa Mkuu wangu.
 
TUMSIFU YESU KRISTO... NI KWELI KABISA HAUPUNGUKIWI NA CHOCHOTE UKIWA NA UNYENYEKEVU NA HESHIMA

ZEKARIA 9:9
 
Mwanamke mmoja aliyekuwa anaitwa Nancy alikuwa anafanya kazi kwenye kiwanda cha kusambaza na kusaga nyama.

View attachment 2858452

Siku moja, baada ya kumaliza ratiba yake ya kazi, aliingia kwenye chumba cha baridi (friji) cha nyama ili kukagua kitu, lakini kwa bahati mbaya, mlango ulijifunga na akakwama ndani bila msaada.

Ingawa aliita kwa nguvu na kupiga mlango kwa nguvu zake zote, kilio chake kilisikika bila kusikilizwa kwani hakuna aliyeweza kumsikia.

Wafanyakazi wengi walikuwa tayari wameondoka, na nje ya chumba cha baridi, ilikuwa haiwezekani kusikia wala kuona kilichokuwa kinaendelea ndani.

Baada ya saa tano kupita, akiwa karibu kufa na amekata tamaa, hatimaye mlinzi wa kiwanda anafika na kufungua mlango.

Nanvy alinusurika kwa miujiza siku hiyo.

Alimuuliza mlinzi ilikuwaje akaja kufungua mlango, jambo ambalo halikuwa kawaida yake kufanya maama sio sehemu yake ya kazi.

Mlizi alieleza: "Nimefanya kazi kwenye kiwanda hiki kwa miaka 35, wafanyakazi wengi wanakuja na kuondoka kila siku, lakini wewe ni mmoja wa wachache wanaonigia na kunisalimia "Habari" asubuhi na kusema "Kwaheri" usiku unapoondoka baada ya kazi. Wengi ujifanya kama hawanioni.

Leo, ulipoingia kazi kama kawaida yako ulinisalimia "Habari", lakini jioni baada ya saa za kazi, niligundua kwa kushangazwa kwamba sikusikia "Kwaheri tutaonana kesho" kutoka kwako. Hivyo, niliamua kukutafuta kila mahali.

Ili nipate salamu yangu "Habari" na "Kwaheri", kwa sababu zinanikumbusha kuwa mimi ni mtu.

Kwa kutokusikia kwako kuaga leo, nilijua kuna kitu kilikuwa kimeenda hovyo. Ndio maana nilikuwa nikikutafuta kila mahali."

Kuwa mnyenyekevu, penda na heshimu wale wanaokuzunguka kamwe huwezi kujua kesho itakuletea nini.

Mwisho 😎

C & P FROM X
Sio mara zote heshima hulipwa kwa heshima.

Mimi kuna wafanya usafi na walinzi baadhi wa sehemu ninapofanyia kazi,nawasilimia wananiangalia kama hawanioni vile.

Chukulia hiyo hali ni wewe,ungejisikiaje?

Kwa sasa imebidi na mimi nawapita tu,yaani mtu hata namsemesha hanijibu wakati anasikia kila kitu.
 
Back
Top Bottom