nyota ya mafanikio unamaanisha nini?
Yaani mtu anikatae afu anilaani? Hakuna kitu kama laana, ni uthubutu tu.
Bora kutunza baba mlezi aliyejali.
Ipo siku ataelewa umuhimu wa babaye
habarini wana mmu,
kuna habari nimeisoma mahali nikaona si vibaya nikiwashirikisha ambayo imenifanya nijiulize kweli KUNA KOSA LISILOSAMEHEKA? kuna mwimbaji maarufu wa bongo flava ambae ana pesa na hata amemnunulia mama yake gari la 38 M na pia anatumia mamilioni ya pesa kwenye starehe ili hali baba yake anaumwa mguu kwa muda mrefu bila msaada wowote ikiwa ni sh milioni 1 tu ndio inayoitajika kumtibu.
Kipindi cha nyuma kidogo mwimbaji huyu aliwai kusema kuwa baba yake alimkana,na mama yake ndie aliyeangaika nae toka mdogo kwa kila kitu.
Ingawa mwenye kuhuku ni Mungu lakini kwa hisia zako hivi alifanyalo huyu mwimbaji ni sahihi au si sahihi?
Ni hayo tu,nawatakia week-end njema.
NB: kwa ambao mmeshavurugwa na foleni,kazi,stress e.t.c msi comment
inawezekana kweli huo msemo ndio uko unafanya kazi labda angemuomba msamaha mwanae
lin;
Mtu mzima ukiisha jikuta unamchukia mzazi wako yeyote kati ya Babako au Mamako, weye ni taa.hira tu. Hata ungevuma mpaka kwenye upepo.
Kumbuka waswahili walisemaga; Utavuna ulichopanda. Kweli babake anavuna alichopanda lakini mtoto huyo huyo atajavuna na yeye anachokipanda kwani hakuna mwanaye atakaye mjali???
AAche kuyakumbuka mavi ya kale. Achukulie hilo kama ngazi kwake na amkaribishe babake kwake aje ale mema aliyoyafanya mamake. Mjinga ka huyo aweza kwenda kumjali baba wa kambo kuliko. Pole sana mbaba unayetaabika leo wala usimlaani mwanao
Mzazi ni Mungu wa pili. Akilaani hamna anayeweza kurekebisha hiyo laana
Kongosho,
Najua utakataa tu kwa kuwa kuna kukataa lakini babako alivyo ndivyo nawe utakuwa. Huo ndio uumbaji na Mungu hajakosea hapo. Nawe utawa[uuza wanao, hata kama utajitahidi vipi, mtoto akizubaa tu umemtema. Ndivyo ilivyo, hivyo mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
Laana ipo na itadumu daima, hutafanikiwa. Mwone huyo mtu waliye msema humu, mwangalie kidogo tu utaona mambo yake yatakavyo samaratika kiaina.
Sijaona mahala uliposema kuwa baba karudisha roho yake na sasa kamkubali mwanae.
nimeshawahi kusikia kijana akisema "atanitafuta tu akikua".
Sina moyo na wanaotelekeza watoto.
atajiju.
Mkuu unajua uchungu wa kukanwa na mzazi?
Kinacho tokea hapo ni Mungu kumuadhibu huyo mzee na si Dimond kuonekana kuwa hajali.Unaanzaje kusikitika kwa mtu ambaye hakuwahi kukujali wala kutaka kukusikia hata siku moja
Domoooooo
Kusamehe ni moyo wa mtu, inategemea pia aliimia au madhara aliyopata kwa kukanwa na babae pia hvyhvy kwa ***** aliumia kiasi hadi ashindwe kumshawishi mwanae amsamehe babake, pengine ndie alisababisha wakakulia maisha waliokua nayo. UNAPOSKIA MALIPO HAPAHAPA DUNIANI NDIO HAYO. naungana nae kwa maamuzi yake.
Ni kweli, we earn forgiveness.
Inawezekana wala hajamkubali na kakimbilia kwenye vyombo vya habari.