Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,331
- 14,259
Hiyo ni kwa Wajinga tu.isingekuwa hofu ya kifo,jehanamu na kutokuzikwa na kanisa,watu wengi wangeshazipiga chini hizi dini
Hiyo ni kwa Wajinga tu.isingekuwa hofu ya kifo,jehanamu na kutokuzikwa na kanisa,watu wengi wangeshazipiga chini hizi dini
Ttz sio kutoa au kubeba tatizo unapanga sadakaUnaendaje kanisani na buku 5 mkuu? Wakati baa mnaingia na laki beba kuanzia hamsini ukiona unahoji mambo ya sadaka jua umekufa kiroho toa ulichonacho huna tulia Mungu anakuona matumiz ya sadaka hayatuhusu imarisha uhusiano wako na Mungu kwa kutoa
Eeh, moyo wangu ukiwa hauna kinyongo juu yao basi nitaenda. Unafiki siwezi. Nitapata dhambi mara mbili bure.Nashukuru sana dada kwa kunielewa.
Ndg. Nasri; Hata ss Wakristo mwanzoni ilikuwa hivyo i.e. Tulipokea misaada ya Kifedha na Mali kutoka Ulaya lakini kadri muda ulivyokwenda ndio tuko hapa sasa.Wakati unatusifia Waislamu, sisi huku wenyewe tunatamani tungekuwa na moyo wa kutoa sadaka kama wenu.
Sisi ni changamoto watu wazito kutoa sadaka, madrasa na misikiti mingi inahitaji ukarabati na shule pia. Ila watu wetu wazito mno wa kutoa sadaka. Sadaka mpaka zitokee kwa waarabu ndio madrasa zijengwe
Lkn fuata huo ushauri wa Bwana wetu Yesu Kristo.Eeh, moyo wangu ukiwa hauna kinyongo juu yao basi nitaenda. Unafiki siwezi. Nitapata dhambi mara mbili bure.
Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Mh ingekuwa hivyo basi pia wachamungu wa kweli wangekuwa wengi lakini tunaona watu wanadini ila bado wanafanya na mambo yenye kusababisha kwenda motoni.isingekuwa hofu ya kifo,jehanamu na kutokuzikwa na kanisa,watu wengi wangeshazipiga chini hizi dini
Nitafanya. Ila unafiki nimekataa ndugu yanguLkn fuata huo ushauri wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Unafiki sio mzuri,hata Maandiko Matakatifu yanakataza.Fuata ushauri wa Bwana wetu Yesu Kristo .
Pole sanaSiku moja nimemtembelea mzee wangu nilipofika akaniambia anadaiwa elfu hamsini kanisani kwa ajili ya harambee.Akanieleza kuwa kila jumuiya imepangiwa kiasi flani cha fedha ambazo zimegawanywa kwa kila nyumba.Mzee wang anakaribia miaka 80..Na alinieleza kuwa siku ya harambee kila familia wanakuwa wanasomwa kanisani mnapita mbele kwenda kukabidhi hicho kiasi cha fedha na kama huna lazima utoe sababu za maana hapo na linakuwa deni mpaka ulilipe. Mambo yamekuwa magumu mno siku hizi.
You have a brain and you use it.Uzuri wake ni kuwa usipotoa si kosa la jinai.
Kama hujui mimi nilikuwq mnistrant mpiga chetezo ila hawa RC wamekuwa wazinguzi sana wahitaji unachanga tena na wakati sadaka ya pili ilikuwa ni kwenda kuwaona wahitaji in short hawa ma padre nao wamestuka wana familia tunalisha familia zaoUlishawahi kuona post zangu kuhusu kulilalamikia Kanisa Katoliki juu ya taratibu zake??.Mimi ni Mkristo Mkatoliki niliyekomaa kweli kweli,kisiki Cha mpingu kitoke nyuma.
Hiyo pesa ya kuwa mkatoliki ndo naiyona leo. Sijui itakua parokia gani hiyo. Kuhusu michango kwa uzoefu wangu mdogo nilionao. Ni hivi mfano mimi kabla sijahamia kwangu parokia mbili zote nilizowai sali zilikua hazina michango mingi kwakweli. Sasa kimbembe huku nilikojamia ndo kwanza tunajenga kanisa, aisee kuna michango jamani. Ila hii michango mimi huwa hainipi tabu kwasababu natoa nilichojaliwa .Ukishaingia mfumo wa jumuia lazima utowe pesa ya kuwa mkatoliki kila mwezi.
Pili harambee za kipuuzi na sadaka nyingi kwenye ibada inaondoa system ya kikatoliki ambayo tulizoea ibada ya misa ya jumapili ni lisaa limoja na nusu tu na ikizidi kwa special case ni masaa mawili tu, sasa kwa huu upumbavu ulioanza ibada inakwenda mpaka masaa matatu, misa ya kwanza mnaingia saa 12 asubuhi mnatoka saa mbili na kitu.
Uwepo na wachamungu wengi hakutokani na Hofu ya Kifo,Jehanum au kutokuzikwa na kanisa bali ni kutokana na watu walioamini na kuiishi Imani yao kwa vitendo. Kwa kifupi ni kwamba Kifo ni LAZIMA uwe ni mcha Mungu au asiye mcha Mungu. Jehanum ipo tu haijalishi ww ni mcha Mungu au la. La msingi ni Je, ww umejiandaa kwenda sehemu gani? i.e Matendo yako yanakuelekeza au Umechagua kwa hiari yako kwenda wapi? Mbinguni au Jehanum? Kuwa na Dini sio Tiketi Kigezo cha kwenda mbinguni. Kuzikwa na kanisa hakumfanyi mtu aende mbinguni. Kwa mantiki hiyo wapo watu (Roho zao) watakaohesabiwa Haki (watakaokwenda mbinguni) kutokana na matendo yao mema waliyotenda katika kipindi cha Uhai wao hapa Duniani na wapo watu (Roho zao) watakaohukumiwa kuingia Jehanum kutokana na matendo waliyotenda.Mh ingekuwa hivyo basi pia wachamungu wa kweli wangekuwa wengi lakini tunaona watu wanadini ila bado wanafanya na mambo yenye kusababisha kwenda motoni.
Hilo unalizungumziaje?
Wamekaza macho wanasubiria kuona nani anainua kichwaView attachment 2182986
Christian Revenue Authority