Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,279
92,344
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
 
Uzuri wake ni kuwa usipotoa si kosa la jinai.
Ukishaingia mfumo wa jumuia lazima utowe pesa ya kuwa mkatoliki kila mwezi.

Pili harambee za kipuuzi na sadaka nyingi kwenye ibada inaondoa system ya kikatoliki ambayo tulizoea ibada ya misa ya jumapili ni lisaa limoja na nusu tu na ikizidi kwa special case ni masaa mawili tu, sasa kwa huu upumbavu ulioanza ibada inakwenda mpaka masaa matatu, misa ya kwanza mnaingia saa 12 asubuhi mnatoka saa mbili na kitu.
 
Toa ndugu toa ndugu..ulichonacho..halafu unataka usitoe hilo kanisa litapelekaje injili..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje wahudumu..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje bills tofauti kama umeme na maji...unataka usitoe hilo kanisa litafanyeje logistics mbali mbali...unataka usitoe maintaince na repairs ya vifaa na miundombinu mbalimbali utatoa wewe.??

Acha kulalamika sana kama huna hela kaa kutulia

Uzuri hujalazimishwa..ila mkristo wa kweli hawezi kuona kama ni wizi mana hayo ndio mahitaji muhimu ya kuendesha taasisi.

Kingine kutoa ni upendo..kiwango itachojaliwa kutoa kinatosha sana.

Kama unaona hufiti nenda huko ambako hawatoi sadaka..hakuna aliyekushikiria unabaki kanisani.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom