Vikao vya chama vipo kwenye ngazi ya Msingi na ukipeleka maoni yanafika Taifa. Ukiwa mwanachama una wajibu wa kuhudhuria vikao vya chama! Kila mwanachama ana kikao cha kuhudhuria na niwajibu.
Chama kitapigiwa kura na wanachama, wapenzi, washabiki na wale watakaokubaliana na sera zetu. Tunaendelea kuwajengea imani watanzania kuwa sisi ndio tumaini jipya. Watakaotuelewa watatupigia Kura.
Kukosoa viongozi kwa wanachama ni kwa kufuata utaratibu, Otherwise itakuwa yale yale, Naibu Katibu mkuu anaenda kuulizia hesabu za chama kwenye Ofisi za PAC. Huo ni upuuzi!
Ya huyu kiongozi wa BAVICHA mimi siyajui na wala sitaki kuyaongelea hapa kwasababu sina uhakika na yanayosemwa kuhusu yeye lakini ningeyajua ningechangi ama kwa kumuunga mkono mleta mada au kumpinga kwa hoja.
Hata hivyo,utaratibu wa kutumia vikao vya chama kukosoa unawafaa kutumika zaidi kwa viongozi na si kwa mashabiki wengine wa kawaida na ambao ndio wapiga kura.
Kama watu wanatoa pongezi kwa viongozi na chama kupitia mitandaoni, ni kwanini basi iwe nongwa kukosoa?!Kukosoa si dhambi na kila mtu ana mawazo yake na isitoshe hakuna mtu aliekamilika.
Kumbukeni hizi ni nyakati za teknolojia kama hii mitandao ya kijamii na watu wako huru kutoa mawazo yao na pia hizi ni siasa za ushindani.
Mkiminya uhuru wa mawazo kwa mashabiki wa chama maana yake ni kuwataka watu hao wakatafute uhuru huo kwenye vyama vingine jambo ambalo si jema hata kidogo.
Mfano,msemaji wa chama ana akaunti hapa JF.Sasa akileta hoja au jambo hapa ina maana watu wasichangie wasubiri vikao vya chama?
Je,wapiga kura wa CHADEMA ni wanachama tu?
Jambo baya na hatari ni kwa viongozi kulumbana wao kwa wao hadharani na majukwaani lakini mashabiki wa kawaida tu waachwe watoe yao ya moyoni na uzuri penye ukweli uongo hujitenga hivyo alie mnafiki na mzushi mwisho wa siku ataishia kuumbuka tu.
Mtu kama ni pandikizi mwisho wa siku atajulikana tu na hapo ndio itakuwa sahihi kumpuuza na hata kumuita msaliti lakini si kama hivi mnavyofanya baadhi ya mashabiki wa CHADEMA hapa JF.
Tukumbuke hata Nyerere mwenyewe alikuwa anaikosoa CCM na viongozi wake tena hadharani kabisa na mchana kweupe.