Chademakwanza
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 6,346
- 1,872
Kamanda unadhani wt wanaoSupport CDM wanaAcces yakuingia kwenye Vikao????
Kwenye kila kata Tanzania kuna Mwenyekiti na Katibu wa kata Husika kuna Matawi pia
Chadema Kwanza
Kamanda unadhani wt wanaoSupport CDM wanaAcces yakuingia kwenye Vikao????
CHADEMA ni chama cha wote lazima tuhoji utendaji wa viongozi wake huyu jamaa kalala kasinzia hafanyi harakati zozote.
naming its not fair!
Any way kiufupi hafai,ila historia inambeba.
Ya huyu kiongozi wa BAVICHA mimi siyajui na wala sitaki kuyaongelea hapa kwasababu sina uhakika na yanayosemwa kuhusu yeye lakini ningeyajua ningechangi ama kwa kumuunga mkono mleta mada au kumpinga kwa hoja.
Hata hivyo,utaratibu wa kutumia vikao vya chama kukosoa unawafaa kutumika zaidi kwa viongozi na si kwa mashabiki wengine wa kawaida na ambao ndio wapiga kura.
Kama watu wanatoa pongezi kwa viongozi na chama kupitia mitandaoni, ni kwanini basi iwe nongwa kukosoa?!Kukosoa si dhambi na kila mtu ana mawazo yake na isitoshe hakuna mtu aliekamilika.
Kumbukeni hizi ni nyakati za teknolojia kama hii mitandao ya kijamii na watu wako huru kutoa mawazo yao na pia hizi ni siasa za ushindani.
Mkiminya uhuru wa mawazo kwa mashabiki wa chama maana yake ni kuwataka watu hao wakatafute uhuru huo kwenye vyama vingine jambo ambalo si jema hata kidogo.
Mfano,msemaji wa chama ana akaunti hapa JF.Sasa akileta hoja au jambo hapa ina maana watu wasichangie wasubiri vikao vya chama?
Je,wapiga kura wa CHADEMA ni wanachama tu?
Jambo baya na hatari ni kwa viongozi kulumbana wao kwa wao hadharani na majukwaani lakini mashabiki wa kawaida tu waachwe watoe yao ya moyoni na uzuri penye ukweli uongo hujitenga hivyo alie mnafiki na mzushi mwisho wa siku ataishia kuumbuka tu.
Mtu kama ni pandikizi mwisho wa siku atajulikana tu na hapo ndio itakuwa sahihi kumpuuza na hata kumuita msaliti lakini si kama hivi mnavyofanya baadhi ya mashabiki wa CHADEMA hapa JF.
Tukumbuke hata Nyerere mwenyewe alikuwa anaikosoa CCM na viongozi wake tena hadharani kabisa na mchana kweupe.
Ushauri wako ungelikuwa mzuri sana sana na wakujenga kama ungeli uzungumzia MAHALA STAHIKI na SI JF au on PUBLICITY.
Sasa hata mimi unanipa mashaka usije kuwa ni WALEWALE na KAMA SIYO WALEWALE comeon ASAP and Correct your Post.
Haraka sana.
Kwa yeyote ambaye anaushauri kuhusu bavicha naomba afike osifi za chama mkoa au makao makuu tutamzikilia kama ni chadema kweli
Hatutavumilia double standard
NAOMBA NIWEKE WAZI KUWA SIWEKI POSTI HII ILI KUVURUGA UMOJA HUU,WALA SINA NIA YA KUFARAKANISHA VIONGOZI,NIA YANGU NI KUANZISHA MJADALA MPANA ILI KUUSAIDIA UMOJA WETU UENDANE KASI INAYO TAKIWA.
Baraza la vijana wa chadema kwa sasa linaonekana limefubaa,ni thahiri uongozi uliopo unashindwa kubuni mambo,hauna kasi iliyokuwepo hapo awali alipokuwepo Mh,Heche, uongozi ni kama unafanya mambo kwa kushuliwa na baadae una lala tena.niwazi mwenyekiti wetu amzidiwa mbinu au hana mbinu za kuchangamsha baraza.
Wana bavicha niwazi sasa tunahitaji mbinu mbadala,au plan B, baraza linahitajika kuamka na uongozi ukubali kuanzisha kikosi kazi maalum kitakachokuwa ndani ya bavicha kwaajili ya kazi hiyo,mwenyekiti abaki ofisini kusimamia harakati hizo kwasababu hata kwenye operesheni alizoshiriki ameonyesha kutomudu mikiki mikiki na badalayake amakuwa akimezwa na waliomzunguka na kutoonekana kabisa,amekuwa kama anauoga flani.
Tunahitaji kikosi kitakacho changamsha baraza letu hata ikiwezekana waliogombea nafasi ya mwenyekiti na kushindwa basi,wapewe uwanja maalum wa kuendesha siasa ndani ya bavicha ili baraza lichangamke na kurudisha msisimko uliokuwepo awali.
kwamuda ambao mwenyikiti amekuwepo umetosha kumpima na kujua ni mtu wa aina gani,uwezowake jukwaani tumesha ufahamu,huvyo hatupaswi kuendelea kupoteza muda wakati uchaguzi unakaribua.
NI WAKATI WA KUCHUKUA HATUA SASA KWA USTAWI WA UMOJA WETU
Nina imani na Chadema, nawaamini Bavicha
Mkuu, mi naona ni kama BAVICHA ya sasa imepoa sana, si kama ile ya Heche, sijui wewe unaipima vipi Mkuu!