Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA

Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA

Bavicha noma mkuu, Tumebadilisha mbinu hatufanyi matangazo tunamkimbiza mwizi kimyakimya.Wakati wao wanalipana kwa kupost uharo mitandaoni sisi tupo field tunakamata mwizi meeeeni
 
Mkuu, mi naona ni kama BAVICHA ya sasa imepoa sana, si kama ile ya Heche, sijui wewe unaipima vipi Mkuu!

BAVICHA ya sasa si jeshi la mtu mmoja bali ni jeshi kubwa lililotapakaa kila kona.Mikoa na wilaya wanapiga kazi usiku na mchana na hawamtegemei m/kiti tu kama zamani.
 
NAOMBA NIWEKE WAZI KUWA SIWEKI POSTI HII ILI KUVURUGA UMOJA HUU,WALA SINA NIA YA KUFARAKANISHA VIONGOZI,NIA YANGU NI KUANZISHA MJADALA MPANA ILI KUUSAIDIA UMOJA WETU UENDANE KASI INAYO TAKIWA.

Baraza la vijana wa chadema kwa sasa linaonekana limefubaa,ni thahiri uongozi uliopo unashindwa kubuni mambo,hauna kasi iliyokuwepo hapo awali alipokuwepo Mh,Heche, uongozi ni kama unafanya mambo kwa kushuliwa na baadae una lala tena.niwazi mwenyekiti wetu amzidiwa mbinu au hana mbinu za kuchangamsha baraza.

Wana bavicha niwazi sasa tunahitaji mbinu mbadala,au plan B, baraza linahitajika kuamka na uongozi ukubali kuanzisha kikosi kazi maalum kitakachokuwa ndani ya bavicha kwaajili ya kazi hiyo,mwenyekiti abaki ofisini kusimamia harakati hizo kwasababu hata kwenye operesheni alizoshiriki ameonyesha kutomudu mikiki mikiki na badalayake amakuwa akimezwa na waliomzunguka na kutoonekana kabisa,amekuwa kama anauoga flani.

Tunahitaji kikosi kitakacho changamsha baraza letu hata ikiwezekana waliogombea nafasi ya mwenyekiti na kushindwa basi,wapewe uwanja maalum wa kuendesha siasa ndani ya bavicha ili baraza lichangamke na kurudisha msisimko uliokuwepo awali.

kwamuda ambao mwenyikiti amekuwepo umetosha kumpima na kujua ni mtu wa aina gani,uwezowake jukwaani tumesha ufahamu,huvyo hatupaswi kuendelea kupoteza muda wakati uchaguzi unakaribua.

NI WAKATI WA KUCHUKUA HATUA SASA KWA USTAWI WA UMOJA WETU

Mwisho wa siku na wewe utaitwa msaliti
 
Back
Top Bottom