Kuna kila dalili CHADEMA na Sukuma Gang wameunda umoja wa siri dhidi ya Serikali. Umoja wenu uwe na hoja za msingi zenye mashiko

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Friends and Enemies,

Ngoma ambayo mwenyekiti wa kudumu wa chadema Freeman Mbowe aliianzisha wiki kadhaa zilizopita ndiyo kiini hasa Cha taharuki ya tunachokiona kinaendelea Kwa sasa.

Either nichukue nafas yangu kumpongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa kufanya clarifications za kina kuwa hakuna bandari yoyote ndan ya nchi hii itayouzwa na hakuna suala la Wala ajenda ya ukanda,udini na upigaji kama vile ambavyo Mbowe na SUKUMA GANG wanavyoshadadia,

Majaliwa kama mtendaji Mkuu wa serikali amesisitiza kuwa mwananchi ana Haki ya kutoa maoni, ana Haki ya kuwa na hofu, ana Haki ya kushauri na kutoa mapendekezo wapi paboreshwe, lakin siyo sawa kuja na kashfa na kauli za kejeli na uzushi Kwa serikali na Hususan Kwa Rais kama vile ambavyo Mbowe na SUKUMA GANG wanavyoshadadia kuwa Kuna uzanzibar na ukanda.

Nasema SUKUMA GANG na Chadema wameungana katika hili kwani ulifuatilia waziwazi mijadala inayoendelea hivi sasa mitandaoni na vijiweni inaonesha wazi wazi kuwa hawa watu walikuwa wanatafuta ajenda ya kuwaunganisha pamoja na sasa wameipata hii ya bandari.

Kitu tunachotaka kuwaeleza ni kwamba pale bandarini wezi na vibaka wameweka Mizizi mirefu sana na wamekuwa kama corona Kila wakitafutiwa dawa Wana mutate na kuwa virus wapya na kuendelea kuiba na kulitia hasara Taifa hili.

Kuja kwa mwekezaji mpya wa kumreplace TICTS ni njia Bora ya kusambaratisha Moja Kwa Moja vimelea hivyo vya Rushwa,wizi na utendaji hafifu wa bandari.

Chadema na SUKUMA GANG hata mkiungana basi tafuteni hoja za msingi na zenye mashiko, acheni kupotosha wananchi na kutengeneza taharuki,kumbukeni maendeleo hata huyo JPM mnaemkumbuka hivi sasa alishaambiwa kuwa hayana chama.
 
Chadema ni upinzani kibogoyo wakiitwa ikulu wanaunga juhudi mkono
inabidi kiundwe chama kipya cha upinzan ila kwa chadema miaka million 10 ccm ataendelea kung'ang'ania madaraka
 
Raisi ana kila kitu unashindwa kufanya mageuzi mpaka uwape waarabu mpaka na kitovu chako cha uchumi bure.

Una jeshi, TISS, polish, makada hao wote wameshindwa mpaka mwarabu ndio ataweza?
 
Ndiyo mtoea maoni sasa,pale kwenye kasoro parekebishwe na kwenye kuboresha parekebishwe,

Milango iko wazi na ndiyo maana mkawekwa wazi Kwa mkataba ule kupelekwa Kwa wawakilishi wenu bungeni.
Hao Wawakilishi watapata lini nafasi ya kurekebisha wakati nafasi Yao ilishaisha?
 
Tabla lasa, raisi anakila kitu unashindwa kufanya mageuzi mpaka uwape waarabu mpaka na kitovu chako cha uchumi bure, unajeshi, tiss, polish, makada hao wote wameshindwa mpaka mwarabu ndio ataweza!?

Mwarabu siyo mara ya kwanza na Wala Tanzania siyo nchi ya kwanza kuweka uwekezeji katika masuala hayo ya bandari,tatizo lenu ni nini?

Au mkitaka apewe muisrael Taifa teule? Hana pesa sasa kama anayo aje apewe ili mfurahi
 
Katika mameno yote ya PM hakuna jibu hata moja juu ya maswali yanayoulizwa juu ya mkataba
 
Back
Top Bottom