Kuna "kakikundi" ambako Rais Magufuli alikuwa nako pale TANROADS na anakatukuza sana, kulikoni?

Acha uongo na kuongea usiyoyajua.

Alfayo kidata alikua katibu mkuu ardhi enzi ya JK mpaka JPM anaingia madarakani.

Kijazi alikua katibu mkuu ujenzi kabla yakupewa ubalozi. Kijazi alipewa ubalozi na JK sio Magu.

Inatia kinyaa sana kuongea usiyoyajua.
John Kijazi Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Katibu Mkuu (W) Ujenzi wakati wa Mkapa.
Uteuzi wa katibu mkuu Wizara sio discretion ya Waziri isipokuwa Mhe. Rais.

Alfayo Kidata imeelezwa vyema alikuwa Katibu mkuu (W) Ardhi wakati wa JK.
Ukifuatilia site hii yaonesha Kidada kawepo toka enzi za JK kama Naibu Katibu Mkuu Tamisemi then akawa Katibu wa Wizara Ardhi.


JK aliwahi kumchukua aliewahi kuwa Katibu Mkuu wizara ya mambo ya nje Philemon Luhanjo wakati wa Mkapa JL akiwa Waziri na kumpa kuwa katibu Mkuu Kiongozi.

So far, kama Kichere alifanya vyema Tanroad mpaka kuwa Chief Internal Auditor sidhani kwa kuwa Tanroad inampa demerits za kuaminiwa kuwa CAG.

Mwisho Wakati wa JK ulikuwepo uvumi sina hakika kama ni kweli; "wanamtandao" wengi walipata nafasi serikalini.

Nataka kuamini kwamba duniani kote watu hufanya kazi na watu wanaowaamini na wakujua wako loyal kwao hasa nyakati ambazo hujuma na kutoaminiana kupo.

Bravo mlioteuliwa. Ni mategemeo mtatimiza majukumu kwa utumushi uliotukuka.

CDM wakati mmoja Baba mkwe alimwachia mkwewe Ukatibu Mkuu then baadae uenyekiti.
Ndesamburo nae akampa mwanae Ubunge viti maalum.

Lissu nae akampa dada yake pande viti maalum.

Boss mmoja CDM nae akampa "goma" lake ubunge viti maalum.

The moral of the story; mara kwa mara watu hufanya kazi na watu wanao waamini na walio loyal kwao.

Kuna wakati wa Mwl. JKN Shirika la Bima (NIC) lilijaa kabila fulani kwa kuwa boss alikuwa wa kabila lile.
Wakati huo huo wa Mwl. ATC nayo ilijaa watu wa kabila fulani. Na makabila yote yaho mawili hayakuwa ya mkoa wa Mara.

Tanzania yetu ndo hii
 
Haka ni kakikundi ka watu ambako Rais Magufuli alikuwa nako pale Tanroads na amekuwa akikatukuza sana. Imefika hatua hata wakitumbuliwa huku wanapelekwa kule. Aidha wengine nimeona wakipewa hata utukufu usio wa kawaida.

1. Mhandisi John Kijazi.
Huyu alikuwa pale ujenzi kama boss na Rais Magufuli alipoukwaa urais tu akamtoa kwenye ubalozi muda mfupi baada tu ya kudumu hapo sasa yupo naye ikulu kama katibu mkuu kiongozi. Hawa walikuwa maswahiba wakubwa pale ujenzi

2. John Mfugale.
Huyu ni mtendaji mkuu wa Tanroads ambaye jina lake limepewa hadhi na Rais Magufuli kuwa jina la daraja la juu la TAZARA. Hii ni ya kwanza kufanywa na mkuu wa nchi yetu na ni ya aina yake. Bila shaka akitoka pale Tanroads anaweza kuukwaa ubalozi.

3. Alphayo Kidata.
Huyu naye aliwahi kupita pale Tanroads. Rais Magufuli akamteua kuwa kamishina mkuu wa TRA, akamrudisha kwenye ubalozi akamvua hadhi ya ubalozi na wengi tulitarajia kitakachofuata ni mashitaka dhidi yake ila sasa ni RAS.

4. Charles Kicheere.
Huyu naye alikuwa na Rais Magufuli pale Tanroads akateuliwa kuwa kamishina wa TRA, akatumbuliwa na sasa ameteuliwa kuwa CAG baada ya kutokea huko kwenye u RAS.

Aidha nimeona leo wahandisi wawili wakiukwaa ubalozi na u RAS na hawa pia wamezungua zunguka kwenye vyeo na walikuwa pale Tanroads na Rais Magufuli.

Naona kuna kitu wanazunguka naye nacho na hawa hawatumbuliki bali wanahamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kulikoni? Hii kweli ni sahihi?
Zimwi likujualo
 
Waendelee kumfichia ufisadi wake wajiandae kuswekwa ndani kwa kesi za uhujumu na utakatishaji pesa
 
Nadhani twakumbuka JK alitoka na January Wizara ya mambo ya Nje akamchukua kama katibu wake binafsi.

Baada ya kugombea ubunge akapewa Unaibu Waziri na Katibu wa Mambo ya Nje CCM kwa nafasi yake pia mjumbe kamati kuu.

Trump amemfanya mkwewe kuwa Deputy Chief of Staff.

John F Kennedy alimteua mdogo wake kuwa AG Marekani.

Rais wa Argentina Néstor Kirchner 2003-2007 alimuachia mkewe Cristina Fernández de Kirchner Urais wa nchi na alidumu 2007-2015.
Kwa sasa madam Cristina ni makamu wa Rais Mteule.

Haya mambo ya kufahamiana sio dhambi. Yapogo. Cha msingi anaowateua wanaweza ku-deliver
 
Kama kiongozi mkuu katika nafasi fulani anaweza tu kujichukulia watu kwa sababu anawafahamu au amewahi kufanya nao kazi; sio vyema. Kuna vetting na kuna ofisi ya serikali maalum kwa vetting na PSSO imeeleza pia taratibu za teuzi. Kuna ofisi inagharamiwa kwa kodi zetu kufanya vetting. Kwanini Sasa tujichotee tunaowafahamu tu?
 
Kwani huko walikokuwa wizara ya ujenzi ni Wizara yake binafsi Magufuli.. si walikuwa humohumo ndani ya utumishi wa serikali.?
Hakuna utaratibu kama huu duniani. Ipo siku watateuliwa wanafamilia ndugu utaona sawa.

Hii nchi ni ya watanzania,hata kama unao ndugu,jamaa na marafiki wenye sifa hupaswi kuwateua maana utendaji pia unawafanya wananchi kuweka mashaka juu yao.

Wanawezakosea kiufundi tu ama bahati mbaya lakini wakahukumiwa kwa ushirika tu.
 
Hii ni Tabia ya mtu dhaifu yani hata kama anaemuamini (kwa mtazamo wake) ana haribu kila ofisi anayompangia yeye hawezi kuona mbadala wake. Hiki ni kilema cha mhe.rais wetu
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata upotevu wa pesa
Hoja za msingi kama hizi ambazo huwezi kujadili kwa hoja muwe mnapita kimya mipasho siyo mahala pake hapa.
 
Hii ni Tabia ya mtu dhaifu yani hata kama anaemuamini (kwa mtazamo wake) ana haribu kila ofisi anayompangia yeye hawezi kuona mbadala wake. Hiki ni kilema cha mhe.rais wetu
Kwani wao chadema wakaguzi wao wana elimu gani na wakina nani? Au ni komu?
 
Back
Top Bottom