G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Haka ni kakikundi ka watu ambako Rais Magufuli alikuwa nako pale Tanroads na amekuwa akikatukuza sana. Imefika hatua hata wakitumbuliwa huku wanapelekwa kule. Aidha wengine nimeona wakipewa hata utukufu usio wa kawaida.
1. Mhandisi John Kijazi.
Huyu alikuwa pale ujenzi kama boss na Rais Magufuli alipoukwaa urais tu akamtoa kwenye ubalozi muda mfupi baada tu ya kudumu hapo sasa yupo naye ikulu kama katibu mkuu kiongozi. Hawa walikuwa maswahiba wakubwa pale ujenzi
2. John Mfugale.
Huyu ni mtendaji mkuu wa Tanroads ambaye jina lake limepewa hadhi na Rais Magufuli kuwa jina la daraja la juu la TAZARA. Hii ni ya kwanza kufanywa na mkuu wa nchi yetu na ni ya aina yake. Bila shaka akitoka pale Tanroads anaweza kuukwaa ubalozi.
3. Alphayo Kidata.
Huyu naye aliwahi kupita pale Tanroads. Rais Magufuli akamteua kuwa kamishina mkuu wa TRA, akamrudisha kwenye ubalozi akamvua hadhi ya ubalozi na wengi tulitarajia kitakachofuata ni mashitaka dhidi yake ila sasa ni RAS.
4. Charles Kicheere.
Huyu naye alikuwa na Rais Magufuli pale Tanroads akateuliwa kuwa kamishina wa TRA, akatumbuliwa na sasa ameteuliwa kuwa CAG baada ya kutokea huko kwenye u RAS.
Aidha nimeona leo wahandisi wawili wakiukwaa ubalozi na u RAS na hawa pia wamezungua zunguka kwenye vyeo na walikuwa pale Tanroads na Rais Magufuli.
Naona kuna kitu wanazunguka naye nacho na hawa hawatumbuliki bali wanahamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kulikoni? Hii kweli ni sahihi?