Kuna jambo haliko sawa. Top ya matajiri katika nchi kuwa wa rangi moja tu

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,243
Reaction score
90,303
Sio kwa ubaya lakini sio hali ya kawaida katika nchi ambayo wengi ni Wabantu, Waniloti na Wakushi matajiri top kabisa katika nchi kuwa ni Wahindi, Waarabu na Waburushi/Wapersia na wao kuwa ndio walioshikilia sehemu kubwa ya uchumi na sekta muhimu za uchumi.

Inaweza isizingatiwe kwa sasa lakini huko mbele mbele italeta shida.
 
Waasia walianza mapema. Wahindi waliletwa na waingereza kujenga reli, na wengine wakaja kufungua biashara za kuhudumia walioletwa.

Hao waajemi na waarabu ndo wa kitambo kabisa enzi za usultani.

Swali ninalojiuliza ni kwamba imekuwaje hawajaathiriwa na sera za ujamaa za Nyerere?
 
Hao uliowataja kuwa matajiri wako busy kufanya biashara na kufungua viwanda. Nyinyi mko busy kuiba kodi zenu na kupeleka benki za nje,kununua vijumba Dubai,kununua majumba ya mabilionini masaki huku mkishindana kununua G wagon za bilioni muwakoge masikini mitaani. Stupid.
 
Hawa watu wana tabia ya kuficha ukwasi wao huko Canada, naamini hata nyakati za JN pesa zao nyingi zilikuwa nje ya nchi.
 
Waasia walianza mapema. Wahindi waliletwa na waingereza kujenga reli, na wengine wakaja kufungua biashara za kuhudumia walioletwa.

Hao waajemi na waarabu ndo wa kitambo kabisa enzi za usultani.

Swali ninalojiuliza ni kwamba imekuwaje hawajaathiriwa na sera za ujamaa za Nyerere?
Ndo ujue kuwa uchawa na kujipendekeza upo tangu enzi za mchonga!
 
Sio kwa ubaya lakini sio hali ya kawaida katika nchi ambayo wengi ni Wabantu, Waniloti na Wakushi matajiri top kabisa katika nchi kuwa ni Wahindi, Waarabu na Waburushi/Wapersia na wao kuwa ndio walioshikilia sehemu kubwa ya uchumi na sekta muhimu za uchumi.

Inaweza isizingatiwe kwa sasa lakini huko mbele mbele italeta shida.
Hao watu historically ni matajiri, aliyeijenga Dar Sultani wa Zanzibar ndio Aliwaleta mostly toka Gujarati India na Balochistan, wapo Tanzania specific kwa ajili ya kufanya biashara na ndio walipa Kodi wakubwa, wanafund kwa kiasi kikubwa Bajeti yetu.

AT same time kuna matajiri kibao local, hapa Kariakoo kuna wakinga wananunua Maghorofa Hadi Bilioni 10 nenda kaangalie Biashara zao hata VAT hawana.

Ukiona maraisi wote kuanzia Nyerere Hadi someone controversial like Magufuli hataki kuwagusa wanajua Hali ya Nchi na Umuhimu wao.

Unaweza ukaamua kuwa mbaguzi na kutaka wasimiliki Mali ama ukaona mchango wao na Ku appreciate.
 
Katika jicho la kawaida ni sawa na kusema uchumi umeshikiliwa na wageni(let's call a spade chepe tu)

Hawa jamaa hata kukitokea machafuko they fly abroad, Canada nk. So ni kama uchumk wetu umeshikiliwa na wageni tu.
Mzungu anaondoka baadhi ya mashamba wahindi wengi ndo wakashika usukani kuyaendesha
Kamwe kwa utamaduni tulionao weusi ni Ngumu sana kuja kuwa juu yao.
 
Hao uliowataja kuwa matajiri wako busy kufanya biashara na kufungua viwanda. Nyinyi mko busy kuiba kodi zenu na kupeleka benki za nje,kununua vijumba Dubai,kununua majumba ya mabilionini masaki huku mkishindana kununua G wagon za bilioni muwakoge masikini mitaani. Stupid.
Escrow, BAE System, EPA, Richmond n.k kote huko wamekuwepo.

Halafu hivi unafikiri kuna mswahili anaweza kwenda kuficha pesa alizokwapua nje au kununua assets huko bila wao kumchorea ramani??
 
Waasia walianza mapema. Wahindi waliletwa na waingereza kujenga reli, na wengine wakaja kufungua biashara za kuhudumia walioletwa.

Hao waajemi na waarabu ndo wa kitambo kabisa enzi za usultani.

Swali ninalojiuliza ni kwamba imekuwaje hawajaathiriwa na sera za ujamaa za Nyerere?
Wahindi waliojenga reli sio hawa Matajiri wa Tanzania. Kama hufahamu waziri mkuu wa Sultani Karne ya 19 aliitwa Tharia topan alikua ni Ismailia toka Gujarati India, Sultan alikua Hana ukwasi kama hawa wahindi, aliwapa mazingira mazuri ya Biashara ili wahamie Znz wakati huo.

Sultani aliponunua kijiji cha uvuvi hapa Dar akawaweka hao wahindi, kina Aga khan wakaitwa ndio wakaijenga Dar, Aga khan alikua na pesa Sana yeye akafanywa ndio msimamizi wa Mali zote wakati huo.

Hawa wahindi wote walikua na Root moja wakagawanyika, Ismailia na mabohora, hawa Ismailia kiongozi wao zilienda Sana na Nyerere wakapewa vyeo vikubwa Sana serikali ya Nyerere na mpaka Leo wengi Wana vyeo nyeti na ni wasomi wakubwa. Diamond jubilee ni alama Yao kubwa na chai aliyonipa Mzee wangu ni kwamba walipofungua Hilo Jengo walidonate almasi nyingi Sana kwa Nyerere.

Upande wa pili mabohora hazikuenda na Nyerere, hawa jamaa hela zao huwa wanampelekea shehe wao Quba, kulizuka ugomvi mkubwa baina Yao na Nyerere na baadhi ya Mabohora kuwasaliti wenzao.

Pia waajemi Wana predate Waarabu na Asilimia kubwa ya wabantu hapa pwani, watu pekee ambao ni wa Mwanzo kabla ya wa Ajemi ni kushite tribes kama warangi, wairaqw etc kuna studies siku hizi zinaonesha makabila ya pwani kama wamakonde, Wazaramo etc DNA zao mpaka Asilimia 50 ni za ki Ajemi, waajemi wamekuja zaidi ya miaka 1000 iliopita na waarabu kama miaka 500 iliopita.
 
Escrow, BAE System, EPA, Richmond n.k kote huko wamekuwepo.

Halafu hivi unafikiri kuna mswahili anaweza kwenda kuficha pesa alizokwapua nje au kununua assets huko bila wao kumchorea ramani??
Nilichokiandika hapo ukisoma kwa undani nimeonesha MENTALITY yao na yetu.
Wao walikuwepo EPA etc na sisi tukaingia. Unajua wao walianza kupiga EPA kabla ya ndugu zetu? Sasa mlipoingia nyinyi mlivyoonja tu EPA mkaanza kuleta magari kwa ndege mara mnunue nyumba za 30m kwa 500m. Ni ulimbukeni unstucost.
 
Hao watu historically ni matajiri, aliyeijenga Dar Sultani wa Zanzibar ndio Aliwaleta mostly toka Gujarati India na Balochistan, wapo Tanzania specific kwa ajili ya kufanya biashara na ndio walipa Kodi wakubwa, wanafund kwa kiasi kikubwa Bajeti yetu.

AT same time kuna matajiri kibao local, hapa Kariakoo kuna wakinga wananunua Maghorofa Hadi Bilioni 10 nenda kaangalie Biashara zao hata VAT hawana.

Ukiona maraisi wote kuanzia Nyerere Hadi someone controversial like Magufuli hataki kuwagusa wanajua Hali ya Nchi na Umuhimu wao.

Unaweza ukaamua kuwa mbaguzi na kutaka wasimiliki Mali ama ukaona mchango wao na Ku appreciate.
Tunamshukuru sana Sultan kutuanzishia Dar es Salaam kutoka kituo cha biashara ya Utumwa wa babu zetu na Pembe za ndovu wetu.
 
Sio kwa ubaya lakini sio hali ya kawaida katika nchi ambayo wengi ni Wabantu, Waniloti na Wakushi matajiri top kabisa katika nchi kuwa ni Wahindi, Waarabu na Waburushi/Wapersia na wao kuwa ndio walioshikilia sehemu kubwa ya uchumi na sekta muhimu za uchumi.

Inaweza isizingatiwe kwa sasa lakini huko mbele mbele italeta shida.
Matajiri au Madalali !?
 
Wahindi waliojenga reli sio hawa Matajiri wa Tanzania. Kama hufahamu waziri mkuu wa Sultani Karne ya 19 aliitwa Tharia topan alikua ni Ismailia toka Gujarati India, Sultan alikua Hana ukwasi kama hawa wahindi, aliwapa mazingira mazuri ya Biashara ili wahamie Znz wakati huo.

Sultani aliponunua kijiji cha uvuvi hapa Dar akawaweka hao wahindi, kina Aga khan wakaitwa ndio wakaijenga Dar, Aga khan alikua na pesa Sana yeye akafanywa ndio msimamizi wa Mali zote wakati huo.

Hawa wahindi wote walikua na Root moja wakagawanyika, Ismailia na mabohora, hawa Ismailia kiongozi wao zilienda Sana na Nyerere wakapewa vyeo vikubwa Sana serikali ya Nyerere na mpaka Leo wengi Wana vyeo nyeti na ni wasomi wakubwa. Diamond jubilee ni alama Yao kubwa na chai aliyonipa Mzee wangu ni kwamba walipofungua Hilo Jengo walidonate almasi nyingi Sana kwa Nyerere.

Upande wa pili mabohora hazikuenda na Nyerere, hawa jamaa hela zao huwa wanampelekea shehe wao Quba, kulizuka ugomvi mkubwa baina Yao na Nyerere na baadhi ya Mabohora kuwasaliti wenzao.

Pia waajemi Wana predate Waarabu na Asilimia kubwa ya wabantu hapa pwani, watu pekee ambao ni wa Mwanzo kabla ya wa Ajemi ni kushite tribes kama warangi, wairaqw etc kuna studies siku hizi zinaonesha makabila ya pwani kama wamakonde, Wazaramo etc DNA zao mpaka Asilimia 50 ni za ki Ajemi, waajemi wamekuja zaidi ya miaka 1000 iliopita na waarabu kama miaka 500 iliopita.
Mkuu nasikia hawa watu wote wenye jina la "Shiraz" ni wazawa wa waajemi ambao walikuwa wakiuza watumwa Zanzibar. Ni kweli?
 
Tunamshukuru sana Sultan kutuanzishia Dar es Salaam kutoka kituo cha biashara ya Utumwa wa babu zetu na Pembe za ndovu wetu.
Dar inaanzishwa biashara ya utumwa imeshakomeshwa na Sultan alikua kiongozi wa biashara, hata Jeshi alikua Hana, yeye alikua kama "connection" ya Swahili elites, viongozi wote wa pwani walikua ni waswahili wenyewe. The so called makabila makubwa East Africa walikua ni partner wa Sultan.

Sultan aliweza kuingia mkataba na nchi kubwa kama USA kwamba Anything they need Africa wananunua kupitia kwake, haikua Empire ya mchezo mchezo.
 
Unaweza kuwa dalali tajiri.
Wakati mwingine nahisi kuwa hutumika kama sura ya kibiashara, huku kukiwa na uwezekano wa kuwa na uhusiano wa karibu wa kimaslahi na baadhi ya wanasiasa wa CCM.
 
Mkuu nasikia hawa watu wote wenye jina la "Shiraz" ni wazawa wa waajemi ambao walikuwa wakiuza watumwa Zanzibar. Ni kweli?
Yap, Shirazi wanatoka Iran, na hata Iran MTU mweusi kutoka Zanzibar alikua anashobokewa kama Royality, MTU mwenye pesa na status kubwa.

Kuna Historia kubwa Sana sababu watu wanataka kudemonise utawala wa Zanzibar wa Sultan inafichwa.

309.-Bwana-Heri.png

Picha halisi ya Swahili Elites aka Shirazi traders.
 
Back
Top Bottom