Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,454
- 872,084
Raha ya post ipate wachangiaji... Kwakuwa tunaiandikia jamii na jamii iki react iwe positively ama negatively lakini ikasema chochote inakupa mwanga fulani kutokana na kile ulichoandika....
Tuna post nyingi nzuri tu lakini unakuta zimechangiwa na watu wasiozidi kumi... Inavunja moyo kweli... Unajiuliza shida iko wapi hapa?
Nikwambie kitu mchangiaji wa kwanza huwa ni muhimu sana Joseverest[emoji3] [emoji3] [emoji3]!!!, kuna watu automatically akianza na post yako atavuta wengine wengi si kwa kile alichochangia la hasha bali kwa positive energy aliyo nayo[emoji144] [emoji144] [emoji144]
Kuna ID ikishaingia tu kwenye mada yako... POLE SANA.... [emoji23] [emoji23] [emoji23] Zinaitwa killer ID'S... inakuja kuua post mazima, inaleta negative energy ambayo huififisha na kuinyongelea mbali mada yako na huo ndio unakuwa mwisho wa kuchangiwa!
Tafadhali nakusihi usije kuanza kupekenyua mada zenye wachangiaji wachache na kuanza kuangalia wa kwanza kuchangia na wa mwisho.... Utazusha mgogoro usio na sababu