mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 821
- 1,343
Kwa hali ilivyo imenifanya kufikiria mengi sana,nimeanza kufikiria upande wa utawala/uongozi nikagundua kua uongozi/utawala ni karama ambayo mtu huzaliwa nayo na unajijua kama ni kiongozi au sio kiongozi kwa kujiangalia wewe na familia yako hapo ulipo , je unafamilia iliyona furaha na amani? je migogoro ya kifamilia au ya ndoa ndani ya nyumba yako au mahusiano yako unaitatua vipi ? je una ndoa iliyothabiti ya mfano wa kuigwa ? Kama ndoa yako inachechemea iko taabani halafu system au mfumo wa nchi au mfumo wa kazi unayofanya inakulazimisha kuendelea kuibeba hiyo ndoa au familia au mahusiano lakini kwa upeo wako umeshindwa basi wewe sio Kiongozi katafute msaada kwa wanadiplomasi waliobobea katika masuala ya mahusiano au masuala ya ndoa.....HUFAI KUA KIONGOZI
Nikaja kufikiria upande wa Kiuchumi,kwa hali ya nchi ilivyo sasa hivi kiongozi au mtawala inabidi angalau awe na upeo wa kufanya biashara ya aina yoyote au awe na uwezo wa kumiliki pesa na kuzifanyia maamuzi sahihi ili zijizalishe na kuongezeka,kiongozi mzuri ni yule anaeweza kusimamia matumizi ya pesa,kama familia yako au ndoa yako au mahusiano yako kila mnapopata pesa mnashindwa kuitumia vizuri na mwisho wa siku inaleta ugomvi mkubwa mahali ulipo wewe hufai kua kiongozi,na ukiangalia sehemu nyingi ambazo zimeshinda watawala wengi au viongozi wengi shida kubwa ni matumizi mabaya ya pesa yaliyopelekea uchumu kuyumba vibaya na kujikuta nchi au familia au mahusiano mnaangukia pua.
Kama huna vyote ue tayari kujifunza kwa watu ambao tayari wao wamefanikiwa kwa nyanja walipo usiwe mkorofi na kukataa kila unachoshauriwa eti kwa sababu labda anaekushauri ni mdogo kwako au ana mamlaka madogo kuliko wewe hivyo unaona kama anakuaibisha,you are wrong !!!!
Sasa ndugu mwana JF we angalia hizo sifa hapo juu kama kiongozi wako hana hata moja hakufai,mimi nimewasilisha hizo kwa mawazo yangu karibuni mchangie....!