Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 6,376
- 6,720
Kwa wale waliokuwapo wakati wa awamu ya kwanza, pili,na tatu kulikuwa na utaratibu ambao naweza kuuita uwazi. Katika sehemu mojawapo ilikuwa ni kutangaza orodha ya waliokuwa wakiandamana na rais kwenye ziara zake iwe nchini au nje ya nchi.
Hii ni kwa sababu rais na watu wake hawasafiri kwa fedha zao binafsi bali kodi zetu. Hata hivyo, baada ya kuingia utawala wa awamu ya nne chini ya Jakaya Kikwete ambaye alituhumiwa kwa skandali nyingi mojawapo ikiwemo ya IPTL iliyopoteza mabilioni ya shilingi za wananchi, utaratibu huu ulizimwa tokana na rais kuanza kuandamana ima na wanafamilia yake kama ilivyo sasa au watu wenye kutia shaka hadi waganga wa kienyeji wengine hata mahawaraaaa. Ufisadi huu wa kimfumo umeendelea.
Leo Rais Samia yuko Zambia kikazi. Ujumbe wake umefanywa siri. Je kunani? Je wenye fedha yaani walipa kodi mnaridhika na ufisadi huu wa kimfumo. Je ni chawa wangapi ameandamana nao wakati maisha yakizidi kuwa magumu kwa watu wetu walio wengi kwa sasa ukiachia mbali kuwa kutangaza orodho ya ujumbe wake haupashwi kuwa siri?
Nini maoni yako
Ni wangapi wanaungana na kutaka orodha ya wanoandamana na rais iwe inatangazwa na wanaoridhika na upigaji na utumiaji mbaya wa fedha ya umma?