Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 401
Wandugu,
Katika vituko ambavyo wengi wetu huwa tunavishuhudia nchi hii ni pale rais wetu anapopata uenyekiti wa mojawapo ya jumuiya za ushirikiano na nchi zingine za Afrika. Kwa mfano, katika jumuiya ya afrika mashariki viongozi wetu wamejiwekea utaratibu wa kubadilishana uenyekiti wa jumuiya kila inapofika muda fulani. Utaratibu huo hauendeshwi kwa kura yoyote. It's just automatic kwamba kama kipindi kilichopita m/kiti alikuwa X basi safari hii anakuwa Y.
Sasa kilichotushangaza wengine na zaidi sana suala hili limejitokeza zaidi wakati wa uongozi wa jk, ni namna na kiwango cha pongezi zilivyotolewa wakati alipopata uenyekiti wa jumuiya ya afrika mashariki. Ilifika mahali baadhi ya wabunge wa ccm wakisimama bungeni wakati wa kuchangia hoja, wanaanza kwanza na pongezi kwa rais wakimsifu kwa kupata uenyekiti ndipo baadaye wanaendelea na hoja zao.
Jamani hii ina mantiki kweli, au ni propaganda tu??? Ninachotaka kieleweke hapa, siyo kwamba napinga rais wetu asipongezwe bali ni kiwango cha kupongeza. Nilidhani muda zaidi ungetumika (kama ni lazima kufanya hivyo) kumwombea na kumtakia mafanikio mema kwa nafasi aliyopata badala ya kumpongeza kwa kupata uenyekiti.