Kuna Haja ya Kumpongeza kwa Nguvu & Bidii Zote Rais kwa Kupata Uenyekiti wa Mzunguko?

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
401
Wandugu,
Katika vituko ambavyo wengi wetu huwa tunavishuhudia nchi hii ni pale rais wetu anapopata uenyekiti wa mojawapo ya jumuiya za ushirikiano na nchi zingine za Afrika. Kwa mfano, katika jumuiya ya afrika mashariki viongozi wetu wamejiwekea utaratibu wa kubadilishana uenyekiti wa jumuiya kila inapofika muda fulani. Utaratibu huo hauendeshwi kwa kura yoyote. It's just automatic kwamba kama kipindi kilichopita m/kiti alikuwa X basi safari hii anakuwa Y.

Sasa kilichotushangaza wengine na zaidi sana suala hili limejitokeza zaidi wakati wa uongozi wa jk, ni namna na kiwango cha pongezi zilivyotolewa wakati alipopata uenyekiti wa jumuiya ya afrika mashariki. Ilifika mahali baadhi ya wabunge wa ccm wakisimama bungeni wakati wa kuchangia hoja, wanaanza kwanza na pongezi kwa rais wakimsifu kwa kupata uenyekiti ndipo baadaye wanaendelea na hoja zao.

Jamani hii ina mantiki kweli, au ni propaganda tu??? Ninachotaka kieleweke hapa, siyo kwamba napinga rais wetu asipongezwe bali ni kiwango cha kupongeza. Nilidhani muda zaidi ungetumika (kama ni lazima kufanya hivyo) kumwombea na kumtakia mafanikio mema kwa nafasi aliyopata badala ya kumpongeza kwa kupata uenyekiti.
 
sasa kama anakomalia title ya udokta wa heshima unategemea nini? Huyu jamaa, jk, ni mpenda sifa sana! Na hao ccm ni wanafiki sana, wanashangilia hata pasipo stahili, shame on them!
 
Rejea kisa cha Nyerere juu ya almasi ya kweli na almasi ya kuchongwa.
 
Sijawahi kumsikia Rais anayeitwa na kufurahia kuitwa DR wakati hakusomea. Marais wengi Duniani wamekwishawahi kupewa shahada hizo za kutunukiwa lakini husikii wakiitwa Dr. Nani amewahi kumsikia Mzee Mandela akiitwa DR Nelson Mandela? Ili kukidhi furaha ya Rais wetu ya kusifiwa napendekeza aitwe PROFESSOR FIELD MARSHAL CARDINAL MUFT MKUU SIR JAKAYA MRISHO KIKWETE.
 
Nadhani inategemea zaidi iwapo watu wamekusoma unapenda nini. Kwa mtazamo wangu Rais anapenda kusifiwa hata kama sifa hizo hazina msingi wala maana.
Kwa mfano alipongezwa saaaana:
- kuwa rais wa kwanza afrika kuonana na Obama (so what?)
- kuwa mwenyekiti wa AU
- kupewa udokta
- kupinga filamu ya darwin nightmare iliyoonyesha wananchi wanakula masalia ya samaki mwanza.

Mkapa pamoja na madhaifu yake hakupenda sifa zisizo na maana, ni katika utawala wake aliondoa picha ya rais kwenye pesa yetu vinginevyo sasa hivi "msimbazi" ingekuwa na sura ya JK na smile lake.
Kwa sasa tuvumilie tu huo usanii hadi 2015
 
Jamani hakuna "time machine" ya kusogeza muda huu uishe haraka? Maana sitarajii mabadiliko yoyote chini ya JK!
 
Wandugu,
Katika vituko ambavyo wengi wetu huwa tunavishuhudia nchi hii ni pale rais wetu anapopata uenyekiti wa mojawapo ya jumuiya za ushirikiano na nchi zingine za Afrika. Kwa mfano, katika jumuiya ya afrika mashariki viongozi wetu wamejiwekea utaratibu wa kubadilishana uenyekiti wa jumuiya kila inapofika muda fulani. Utaratibu huo hauendeshwi kwa kura yoyote. It's just automatic kwamba kama kipindi kilichopita m/kiti alikuwa X basi safari hii anakuwa Y.

Sasa kilichotushangaza wengine na zaidi sana suala hili limejitokeza zaidi wakati wa uongozi wa jk, ni namna na kiwango cha pongezi zilivyotolewa wakati alipopata uenyekiti wa jumuiya ya afrika mashariki. Ilifika mahali baadhi ya wabunge wa ccm wakisimama bungeni wakati wa kuchangia hoja, wanaanza kwanza na pongezi kwa rais wakimsifu kwa kupata uenyekiti ndipo baadaye wanaendelea na hoja zao.

Jamani hii ina mantiki kweli, au ni propaganda tu??? Ninachotaka kieleweke hapa, siyo kwamba napinga rais wetu asipongezwe bali ni kiwango cha kupongeza. Nilidhani muda zaidi ungetumika (kama ni lazima kufanya hivyo) kumwombea na kumtakia mafanikio mema kwa nafasi aliyopata badala ya kumpongeza kwa kupata uenyekiti.
Kwa mujibu wa wahe. wabunge bunge ni sehemu TUKUFU na utukufu huo hautoki sehemu nyingine bali ni ndani ya mipaka ya TZ hii, (i.e by definition wao mtukufu ni Rais wa JMT) hivyo kama vile wewe ufikavyo kwenye nyumba ya ibada na kumrudishia sifa na utukufu Muumba wako bila kushurutishwa , vivyo hivyo wahe. wabunge hurujikuta wamerudisha sifa na utukufu kwa mwenye nchi wanayoitumikia bila shuruti - Lol
 
Ili kukidhi furaha ya Rais wetu ya kusifiwa napendekeza aitwe PROFESSOR FIELD MARSHAL CARDINAL MUFT MKUU SIR JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Hehe,, ila usishangae akipewa hizi tittle zote bado atataka kuongezea na nyingine hata ambazo hazipo. Mpenda sifa huwa haridhiki kaka...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom