Kuna ghorofa udom linawaka moto hivi sasa.

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Wanajamvi kuna mtu kanitonya kuwa kuna jengo ndani ya chuo kikuu cha Dodoma linawaka moto hivi sasa. Ninaendelea kufuatilia ukweli juu ya swala hili na ninaomba kama kuna mtu mwingine mwenye taarifa zaidi atujuze hapa jamvini. Naomba kuwasilisha.
 
Hamna aliyepata uhakika wa hizi taarifa mpaka mda huu???
 
yaani watu wengine badala ya kusema kama ni kweli wao wanasema majibu ya tatizo kabla ya kujua tatizo
 
[h=3]NAPE ATEMBELEA UDOM LEO, AAGIZA MAJENGO YENYE NYUFA YASHUGHULIKIWE HARAKA [/h]


CCM imewaagiza viongozi wanaohusika kwenda kukagua majengo ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ili kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la nyufa zilizoanza kuitokeza kwenye baadhi ya majengo.

Chama kimewaagiza pia viongozi hao kukagua hali ya miundombinu ya majitaka katika maadhi ma maeneo chuoni hapo ili ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inatuamisha maji kutoka katika majengo na kusababisha adha ya harufu mbaya kwa wanafunzi, walimu na wafanyakazima,m wengine chuoni hapo.

Maagizo hayo yalitolewa leo, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kutembelea chuo hicho na kagua baadhi ya majengo ambapo alishuhudia baadhi ya majengo yakiwa na nyufa.


Majengo yaliyoonyesha kuwa na nyufa ni katiba mabweni ya wanafuzi wa Shule ya Sayansi na Jamii yaliyoko Block 2 na 3 ambapo alionyeshwa na wanafunzi wanaoishi katika mabweni hayo.

"Kujengwa kwa chuo hiki ni uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, hivyo ni lazima kuuenzi uamuzi huu kwa kuhakikisha mazingira na majengo yake yanakuwa katika hali bora", alisema Nape.

Nape alionyesha kushangazwa kwake kuona majengo ambayo hayajatimiza miaka mitano tangu kujengwa kwake, kuanza kupata nyufa jambo ambalo alisema ni hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaoishi katika majengo hayo.

Mapema akizungumza na Nape, ofisini kwake, Makamu Mkuu wa UDOM Profesa, Idrisa Kikula alisema, sasa chuo hicho kina wanafunzi 20,000 ambao kati yao asilimia 50 wanalipiwa gharama zao zote za masomo na Bodi ya Mikopo.

Profesa Kikula alisema, wakati chuo hicho kina wanafunzi pia kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Msumbiji, Walimu wapo kutoka nchi za Russia, India, Kenya, Nigeria,Korea, Japan, Poland na Sweden.

 
hawa watakua chadema tuu...........
teh wapi nape?? si ulitoa tamko yakaguliwe?? haya toa tamko tena na leo
 
Wewe udsm unapajua?nenda hall 4 uone kwa nyuma jengo linaweza anguka muda wote toka nasoma 2003 bado vilevile na hawajabadilisha,subirini maafa ya udsm kuanguka kwa hall 4 na kuua

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom