Kuna faida kubwa kwenye mfumo wa tiketi mtandao kwa ukataji tiketi kuliko hasara zake

Kama utaratibu huu Ni mzuri na wenye faida kede kede; MBONA WAMILIKI WA MABASI HAWAUPENDI???
Sawa sawa na kusema mwanamke Ni mzuri wakati hajaolewa Wala Hana mchumba.
Wafanyabiashara wengi wa bongo ukiwabana/ukitaka uweke mambo wazi lazima wawe mbogo
 
Badala ya kuongeza ajira nyie mnazipunguza,
Makanjanja wa stand wakalime,wakajifunze ufundi,biashara nk.Huu mfumo utasaidia kuondoa wimbi la wazururaji pale stand.
Wapiga Debe hawana wanalofanya stand zaidi ya kelele na ghasia.
Kwa taarifa yako mfumo utaongeza ajira.Watu watajisajili kama mawakaka huko mitaani kama tunavyofanya malipo ya shule au ya serikali.Mawakala e- money watajiongezea kipato kwa hio ajira itapanuka katika mfumo rasmi usiokuwa na fujo.
Mfumo huu utawasaidia sana watu wavijijini.
Teknolojia haijawahi kukosea.
Naunga mkono hoja ya mdau kuwa serikali itapata mapato halisi ikisimama kidete hadi daladala zitoe risiti ya EFD mi ntawazonga makondakta wasiotoa risiti mpaka kwa trafiki.Trafiki wawe macho magari yasioyotoa efd.
Ziwekwe namba maalumu za kuripoti gari isiyotoa risiti on the spot.
Lazima tukubali kuhama(Paradigm shift).Yani sekta kubwa ya usafirishaji iendelee kuendeshwa kiholela, unakubaliana na hilo kisa mpiga Debe?
Waafrika tukubali kupokea mabadiriko kwa ustawi wa nchi, sio kila kitu kupinga kisa JIWE yupo madarakani.
Nchi isiendelee kisa kundi dogo la watu watakosa ulaji usio halali, mbona watumishi hewa walitoka na sasa tumesahau maisha yanaendelea.
 
Akihitaji kusafiri atajua tu hamna linaloshindikana.......kila kitu kina mwanzo ingekua hivyo hata hizi mpesa tungetupilia mbali mwanzoni maana watu wengi walikua hawana uelewa
Hao mashangazi ndio wakwanza kuomba salio m-pesa,Tigo nk.Ila kununua tiketi ndio watashindwa eti?
 
Kama utaratibu huu Ni mzuri na wenye faida kede kede; MBONA WAMILIKI WA MABASI HAWAUPENDI???
Sawa sawa na kusema mwanamke Ni mzuri wakati hajaolewa Wala Hana mchumba.
Kwani hata wafanyabiashara Wabongo walizipenda mashine za EFD ⁉️
 
Kwani hata wafanyabiashara Wabongo walizipenda mashine za EFD ⁉️
Tofautisha efd na tiketi ya bus.
Efd mashine haina faida yoyote kwa mfanyabiashara na hata akiona Kuna uwezekano asiitoe hatoi.
Hii ya tiketi si mlisema Ina faida kwa WAMILIKI? Mbona hawaipendi?
Anyway nadhani inatokea Kongwa. I rest my case.
 

Mfumo use kwenye DATA BILA MALIPO (FREE BASICS) kutawezesha kukata tikiti muda wowote bila kugharamia App, ukimuomba mwenye simujanja itabidi umnunulie bando ya kupakua App.
 
Tiketi iwe kwa free basics. Na pia iwe kwa ussd. Yaani unapiga namba mfano *150*99# kisha unachagua mkoa unaotoka, kisha unachagua mkoa unaoelekea kisha unachagua basi kisha unachagua nauli halafu unalipa.
Hili wazo lingenitajirisha ila ndio hivyo sina mtaji wala connection.

Kitu kirahisi
 
Mfumo use kwenye DATA BILA MALIPO (FREE BASICS) kutawezesha kukata tikiti muda wowote bila kugharamia App, ukimuomba mwenye simujanja itabidi umnunulie bando ya kupakua App.
3. KWA ABIRIA
Huyu anafaidika zaidi na mfumo huu:
(a) Unamwepusha kuibiwa. (Kupewa tiketi ya basi ambalo halipo)

(b) Unampunguzia usumbufu wa kuzongwa zongwa wakati wa kwenda kukata tiketi

(c) Unamwondolea usumbufu wa kugonganishwa siti

(d) Unamwondolea adha ya kulanguliwa tiketi kwa kulipa nauli sahihi

(e) Anaweza kununua tiketi toka alipo na kufanya malipo kwa Pesa taslimu, mifumo ya simu (M-PESA, T-PESA, Tigo-Pesa, airtel money, nk), benki, au kulipa kwa kadi

(f) Kumwondolea gharama za kusafiri kwenda kukata tiketi. Mfano kutoka Tegeta kwenda Ubungo kukata tiketi kwa ajili ya kusafiri kesho yake.

(g) Uhuru wa kuchagua basi alitakalo
 
Back
Top Bottom