Kumwambia Babako kuwa Unampenda

Kumwambia Babako kuwa Unampenda

Duuuh mi mwenyewe hadi nazeeka sijawahi kumtamkia baba wala mama hilo neno aisee
 
Kiongozi hata sijui, labda malezi...wakati mwingine nahisi neno lipo kike sana...

Nimekusoma mkuu ....

Malezi yanatufanya wakati mwingine tuone kufanya mambo ambayo ni ya kawaida kama sio kawaida!
 
Hii inategemea na makuzi,kama umezaliwa kwenye ile familia ambayo mtoto anavaa nusu uchi anatoka bafun na kanga iliyolowa kisha anaweza pita mbele ya baba ake aliyejifunga taulo pekee au kavaa bukta tumbo likiwa wazi,kimsingi ni kawaida kumuambia mzazi wako nakupenda huku umerembua macho na kiss la mdomo juu,vice versa kwa watt wa kiume kwa mama zao,..ila kama umezaliwa katika jamii
ile ya kuwa baba ako ni baada ya Mungu hapa dunia,na ukajua kuwa wazazi wako wanakupenda kwa vitendo ndio maana upo hapo ulipo na ukajua kuwa kuna umri ukifika lazima uheshimu mwili wako na akili zako zifikirie sawa sawa siyo kama wale watto wa lutu waliofanya mapenz na baba yao(chukulia picha ya jamii ile nzima) basi kumuambia mzazi wako wa jinsia tofaut na ww kuwa unampenda lazima tuanze kusema umeanza kuwa na laana ya kina lutu.
 
Angekuwepo ningemwambia mara nyingi tu kuwa nampenda bahati mbaya aliondoka mapema sana hata sijajua maana wala kusema nakupenda
 
Katika vitu ambavyo huwa najutia mpaka kesho ni kutokumwambia baba nakupenda mpaka umauti ulipomfika.Wadogo zangu walikuwa wanamwambia sana lakini mie najifanyisha komando ili asinione kuwa nampenda wakati rohoni mwangu hakuna mtu nilikuwa nampenda na nitampenda kama marehemu baba yangu.Kwa hiyo msisite kuwaambia wazazi wenu kuwa mnawapenda
 
kwani kupenda ni nini? my son amekuzwa akinambia mama nakupenda na kunichum kila mara. sasa kuna shida gani mtoto kumwambia mzaziwe nakupenda. basi kama waona soo kusema baba nakupenda sema wazazi wangu nawapenda. hizi akili za kuwaza maneno ingine mbaya mbaya wachaa.
 
kuna siku fulani babangu alinipigia na tuliongea naye tu kwa upoa alafu alimaliza na "i love you" yaani nilishtuka mzeeiya ata sikua na kitu cha kusema. sikumjibu, wala kusema tu "ooh ok bassi baadaye"...

jameni sijui nilimtusi au nini lakini sikupenda kwangu! hizo ni za utisho mzee...
 
Tamaduni tofauti.

Kiafrika afrika kwetu huko upendo wa familia unaonyeshwa kimatendo zaidi.

Kuna matendo mengine yakifanywa tunaona hakuna haja ya kusema nakupenda.

Kuna washua wa rika fulani hata mkewe hawezi kumwambia anampenda.

Hizi habari za dunia ya utandawazi zaidi.
 
Ni kweli kabisa aisee sisi tuliozaliwa kwenye mazingira ambayo mkiamka asubuhi kila mtu anatawanyika....baba na mama wanaweka majembe begani...watoto mnatafuta maji yako wapi daftari ziko wapi then mnatimua mbio hadi kufika shule iliko dk arobaini zimekatika......jioni ukirudi ni mtafutano mara kutafuta kuni,sijui kuchota maji....muda wa kuambiana I love u mtapata wapi..!! Ila kuna wale wenzetu unaamka asubuhi umetayarishiwa kila kitu,unapata breakfast mama yuko pembeni yako baada ya hapo anakusindikiza barabarani kupanda school bus.....mtakosaje kuambiana maneno matamu matamu kama hayo......
 
Hii inategemea na makuzi,kama umezaliwa kwenye ile familia ambayo mtoto anavaa nusu uchi anatoka bafun na kanga iliyolowa kisha anaweza pita mbele ya baba ake aliyejifunga taulo pekee au kavaa bukta tumbo likiwa wazi,kimsingi ni kawaida kumuambia mzazi wako nakupenda huku umerembua macho na kiss la mdomo juu,vice versa kwa watt wa kiume kwa mama zao,..ila kama umezaliwa katika jamii
ile ya kuwa baba ako ni baada ya Mungu hapa dunia,na ukajua kuwa wazazi wako wanakupenda kwa vitendo ndio maana upo hapo ulipo na ukajua kuwa kuna umri ukifika lazima uheshimu mwili wako na akili zako zifikirie sawa sawa siyo kama wale watto wa lutu waliofanya mapenz na baba yao(chukulia picha ya jamii ile nzima) basi kumuambia mzazi wako wa jinsia tofaut na ww kuwa unampenda lazima tuanze kusema umeanza kuwa na laana ya kina lutu.
Inawezekana unalosema lina mantiki...kiafrika na makuzi yetu huko vijijini nitaanzaje kumwambia "daddy I love you" khaaaaaa! Yani hata Sijui ataelewaje mzee yule..atahisi hana mtoto wa kiume tena..teh!
 
Back
Top Bottom