Power to the People
JF-Expert Member
- Jul 11, 2007
- 1,198
- 900
Jana, mume wa rafiki yangu amemuua mtoto wake bila kukusudia akiwa anageuza gari lake atoke kweda kazini. Sipati picha maumivu walio nayo wazazi hasa baba wa mtoto kwa kusababisha kifo cha mwanaye. Nina hakika siwezi kuufikiria wala kuelezea uchungu walio nao sasa hivi.
Ajali nyingi za watoto hutokea nyumbani kwa sababu muda mwingi watoto hawa huwa nyumbani. Sisi kama wazazi tuna jukumu kubwa sana kuhakikisha nyumba zetu ni salama kwa ajili ya watoto wetu. Hebu chunguza nyumba yako, kama iko salama ili kujiepusha na machungu yatokanayo na kusababisha kifo cha watoto wetu wa kuwazaa. Angalia jikoni, bafuni, nje ya nyumba, unahifadhi vipi ndoo za maji, unahifadhi vipi vifaa na kemikali za usafi, drawers zina stoppers au hufunguka mpaka mwisho, socket za umeme zimekaa vizuri au zimelegea. Mambo ya kuangalia ni mengi sana.
Tukumbushane hapa mikakati ya kuchukua kuwaepusha watoto wetu na ajali na vifo vinavyoweza kuzuilika.