Kumuita mtu aliyeudakia tu uongozi Mama wa Taifa ni kutudharau Watanzania wenye akili kubwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,034
Halafu mnavyozidi Kumchoresha bila kujua ni hapa mnapomfananisha Kimafanikio na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere huku mkijua hana hata Miaka Minne (4) Uongozini wakati aliyeitwa Baba wa Taifa alikaa Miaka 23 Uongozini na Kuutengenezea Heshima Kubwa Kimataifa Tanzania yetu hii.

Mama wa Taifa ambalo kwa sasa linapitia Mgawo wa Umeme wakati nchi ina Utajiri mkubwa wa Vyanzo vya Nishati?

Mama wa Taifa wakati Wananchi wanateseka na Hali Ngumu ya Maisha huku Fedha za Kuchezea kuwapa Simba, Yanga na Taifa Stars zipo?

Mama wa Taifa ambalo lina Utajiri mkubwa wa Rasilimali za Kutosha za Kuiletea nchi Maendeleo lakini tunangojea Wazungu, Wachina na Wajapani waje Kutujengea Vyoo Mashuleni na Kutufundisha Watanzania jinsi ya Kunawa Mikono kwa Maji Safi na Salama?

Sasa naanza Kuamini maneno ya Rais wangu Mpendwa na Shujaa Paul Kagame wa Rwanda pale mwaka 2013 Mkutanoni Ethiopia tena kwa Kumdharau kabisa alipomuambia Kiongozi Mmoja wa wakati huo (sasa nimemsahau Jina) kuwa ni Mpumbavu, anaongoza Maiti na kumwambia ampe tu Bandari yake Moja na ndani ya Mwaka Mmoja (huyo Kiongozi na Wananchi wake) hawatoomba tena Misaada Ulaya, Marekani na Asia.

Hovyo kabisa......!!
 
sie wakatoliki tunajua mama wa taifa ni bikira Maria na taifa limekabidhiwa kwa huyo mama kwa ulinzi.........kwa mkatoliki kumuita Samia mama wa taifa ni kejeli
Na haitokuja kutokea GENTAMYCINE nikamuita Rais Samia Mama wa Taifa. Acha aitwe hivyo na Fools ( Morons ) na Sycophants ( Flaterers ) waliomzunguka na wanaomdanganya Kutwa.
 
Kwa lipi aitwe mama wa Taifa?!

Huyu ni mama wa kausha damu (mikopo).
 
Back
Top Bottom