Habari zenu wakuu, natumaini Pasaka kwenu imekuwa vyema, kuna mdada mmoja tulikuwa tukiishi nae mtaa mmoja alikuwa mzuri shombe shombe nilitokea kumpenda sana lakini alikuwa ananiheshimu sana na binti mwenye maadili sana, nilitafuta kila mbinu ya kumuingia lakini nashindwa na sijawahi muona akizungumzia maswala ya mapenzi na sijawahi muona na mwanaume yeyote zaidi ya marafiki wa kike nao wote walikuwa ni mabinti wenye maadili sana ,kwahiyo niliangaika sana mpaka akasafiri lakini leo nimekutana nae ni mwaka wa tatu toka tupotezane Nimemuona ana mtoto mchanga katika kumuuliza maswali akadai amezalishwa na kuachwa huko alikokuwa roho imeniuma sana lakini Sina jinsi nilimpenda sana lakini udomo zege uliniponza sana ,vijana fungukeni msije mkaumia kama mimi .nawatakia sikukuu njema na Pasaka njema