Kumsusa Kikwete, CHADEMA wamevuna mahindi au Mabua?

Hahaha, Ilumbuye Nyamizi, kwanza heri ya mwaka mpya 2012.

Kijana atakuwa mgeni huyu na haangalii hata mwandishi kajiunga lini na ana Post ngapi.

Nakumbuka kampeni ya kumuomba Dr. Slaa agombee Urais ilianza kama utani na wengi wakikejeli. Matokeo yake yameifanya Tanzania ibadilike kwa speed kubwa sana na kupata mwamko mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kutokea.

Hajui kama wewe ulikuwa ni mtu wa kwanza hapa JF kuweka signature yako ya kumuomba Dr.Slaa akubali kugombea Urais hata kabla ya CDM haijamteua?
 
kuna jambo ambalo bado akili za hawa jamaa hazijakaa sawa kuelewa walicho fanya Chadema ni kuonyesha kwa vitendo kuto kukubaliana na mfumo ulio waweka waliopo madarakani

kwa kususa huko matunda mazuri tunayaona awali walipinga kufanyika mabadiliko makubwa ya katiba refer Kombani na Werema pia walisema Chadema ni wachochezi na wapenda vurugu leo nini kinacho endelea

FF penda sana uwe mtu anaye simamia maneno yake kwa manufaa ya wengi kwa muda na asiye mchochezi Hivi Chadema wangegoma moja kwa moja wagevuna mabua au mahindi kwa faida ya nani Uchochezi hauna kwa leo

quote_icon.png
By Dr.W.Slaa
FaizaFoxy,
Si vema kupotosha wala kuingiza ushabiki katika mambo mazito. Tuko kwenye process na kinachoendelea kisitazamwe as an isolated incidence. Process hii ilianzia na wabunge wa Chadema kususia Bunge. Ni vema mtu akatafakari kwa kina kuelewa vizuri mchakato unaoendelea. Umakini, kutafakari na kuchukua hatua ndio njia pekee ya kufikia malengo makuu ya kuliokoa Taifa letu.
 
Kuna siku niliona gari linauzwa na wameandika kuwa wamefanya punguzo la Euro 20,000.

Nikaanza kujiuliza kama hilo ni punguzo, je bei ya gari ikoje?

Mwenye macho haambiwi tazama kuhusu mafanikio ya Chadema/Dr. Slaa.
Loser anaeogelea katika awamu ya pili? ana wabunge zaidi yako, hata nusu yake hujafikia, ana madiwani zaidi yako hata nusu yake hujafikia, alisema "Mie ndio Rais" mtarudi, kauli yake imetimia.
 
i have been a leader, this has been necessary statements i have been following:

1. A good GENERAL is the one with ultimatums..... unatakiwa unapoenda front uwe na njia mbadala iwapo unayoitumia inaelekea kufail.......

2. rigirity + rigidity = breakage...... do not be too rigid other issues we are dealing with are like glass- - - - brittle!

kudos dr slaa, kudos chadema, kudos kikwete
 
Mkuu, Dr. Slaa aliandika vizuri sana. FF anaelewa zaidi ya watu wengi sana hapa JF ila kwa makusudi kabisa anapotosha ukweli.
kuna jambo ambalo bado akili za hawa jamaa hazijakaa sawa kuelewa walicho fanya Chadema ni kuonyesha kwa vitendo kuto kukubaliana na mfumo ulio waweka waliopo madarakani

kwa kususa huko matunda mazuri tunayaona awali walipinga kufanyika mabadiliko makubwa ya katiba refer Kombani na Werema pia walisema Chadema ni wachochezi na wapenda vurugu leo nini kinacho endelea

FF penda sana uwe mtu anaye simamia maneno yake kwa manufaa ya wengi kwa muda na asiye mchochezi Hivi Chadema wangegoma moja kwa moja wagevuna mabua au mahindi kwa faida ya nani Uchochezi hauna kwa leo
 
You choose your future President now but I for sure wait for the ballot to speak.
 
Hajui kama wewe ulikuwa ni mtu wa kwanza hapa JF kuweka signature yako ya kumuomba Dr.Slaa akubali kugombea Urais hata kabla ya CDM haijamteua?

Nadharia ya falsafa ya mtoa mada nimeipata vizuri sana tu ndio maana nimehitimisha kwa kusema kwa mtazamo wa haraka ningefikiri kama hoja aliyotoa, lakini kwa vile nimefanya upembuzi zaidi ndio maana nimetofautia na hoja hiyo kwa maana yamtoa mada kutojua malengo ya Chadema kumwadhibu Kikwete kwa kutoshiriki alipofungua kikao cha bunge, na tarumbeta ile imelia hadi maiikioni mwake bila kikomo hadi kuridhia mchakacho wa katiba mpya ndani ya siku 100 zilizokusudiwa na Chadema ajenda ambayo CCM katika kampeni zake haikuwa na ilani hiyo.

Katika ushindani wa kiitikadi unapoamua kutekeleza ilani ya mwingine ambaye hashiki dola na kutelekeza ilani yako uliyoivalia njuga maana yake ilani yako ilikuwa ni usanii usiotekelezeka na kubaini ya uliowabeza ndiyo yenye mantiki ya utekelezaka.

Nkumba na Sikonge hata hawajawahi kukutana. Si nimeandika hapo juu kuwa uchaguzi wa mwaka 2010 hata sikushiriki? Sasa ingelikuwaje Nkumba awe mbunge na asishiriki uchaguzi?

Infact, familia yetu ni wapinzani wa waziwazi wa Nkumba and Nkumba knows it. Wee unaona Nkumba angelisimama na kumpigia debe Dr. Slaa agombee Urais kwa ticket ya Chadema? Nkumba yupo busy kuichangia sikinde pesa za kununulia Kinanda :)
Sikonge? Au wewe ni nkumba nn?
 
Wakati naandika, nilijitahidi kujiweka katikati na mwisho kabisa ndiyo nikaweka maoni yangu.

Bado sikutaka kujaiminisha kwa asilimia 100 kama wewe kwa sababu sikuwepo chunguni. Hapa duniani nimeshaanza kujiaminisha kuwa kama ukisikia mtu kafa na kazikwa na hukuona mwili wake akiwa maiti, basi usiwe na uhakika kuwa kweli kafa na kuzikwa.

Kususa kulikuwa na ubaya na uzuri wake. Ingelikuwa heri kama Siasa za Tanzania zisingeliruhusu tufikie huko kwenye kususiana na kugomeana/migomo na maandamano. Ila maadam tumefikia hapo, itakuwa makosa kusema kususa kubaya au kuzuri kwa asilimia 100 na nafikiri hata Dr. Slaa atakubaliana na mie.

Ila la muhimu ni kuangalia kwa asilimia ngapi kususa ni kubaya au kuzuri. Mie hapo ndiyo ninamalizia kwa kusema kususa kwa asilimia kubwa kumeleta mazuri. Kwa ufupi ndiyo hayo Sister Nyamizi alimalizia kwa kusema TUPO PAMOJA.
Nadharia ya falsafa ya mtoa mada nimeipata vizuri sana tu ndio maana nimehitimisha kwa kusema kwa mtazamo wa haraka ningefikiri kama hoja aliyotoa, lakini kwa vile nimefanya upembuzi zaidi ndio maana nimetofautia na hoja hiyo kwa maana yamtoa mada kutojua malengo ya Chadema kumwadhibu Kikwete kwa kutoshiriki alipofungua kikao cha bunge, na tarumbeta ile imelia hadi maiikioni mwake bila kikomo hadi kuridhia mchakacho wa katiba mpya ndani ya siku 100 zilizokusudiwa na Chadema ajenda ambayo CCM katika kampeni zake haikuwa na ilani hiyo.

Katika ushindani wa kiitikadi unapoamua kutekeleza ilani ya mwingine ambaye hashiki dola na kutelekeza ilani yako uliyoivalia njuga maana yake ilani yako ilikuwa ni usanii usiotekelezeka na kubaini ya uliowabeza ndiyo yenye mantiki ya utekelezaka.

Taarab la nguvu na sisi watu wa bara kwa kweli inakuwa ngumu kulicheza.

Kama Mungu ni mtoa uhai, kwa nini Dr. Slaa asubiri hadi mwaka 2015? Pana wakati WANCHEKESHA weye! Nenda Nigeria uulize....

Ahh, unatumia nguvu sana kumchora mtu ambaye hayupo. Ngoja ije katiba ya Tanzania na hapo ndiyo utaona kama Watanzania kweli wanamtaka Rais gani. Rais wa NEC atakufa pamoja na likatibu lenu la sasa hivi.

Rais gani anatangazwa na NEC basi kashinda? Wangeliweza hata kukutangaza wewe kuwa mshindi na hakuna ambaye angelibisha.

Slaa,

Nini kinachopotoshwa? nyinyi, wewe hususan ukiwa kiongozi ndiye uliyeongoza maandamano haramu yaliyopelekea watu kufa, wewe kama kiongozi umeshadidia kususa, kuanzia bungeni mpaka mitaani. Hapo ni kipi kinachopotoshwa?

Leo hii, wewe mwenyewe umeona kuwa kususa na maandamano sio tija, ni matatizo tu, ndiyo chama chakao kikaamuwa kumuomba Rais, wako na wetu sote, muonane nae. Kwa uungwana kabisa, Kikwete kakubali kuwaona, jee, mmepoteza nini?

Bado unataka kutuaminisha kuwa kumuona Rais na kujadili mambo muhimu (kama kweli yana umuhim) sio "isolated case"? Hapo ndipo nnapokuona kuwa unaongea kingine na kutenda kingine. Na hiyo inadhihirisha kuwa hata kwenda kwako kumuona kwenye hii unayosema sio "isolated case" si kwa matakwa yako, vipi? ilikuwa ni amri kutoka kwa Mwenyekiti.

Usemi wako wa mwisho hauashirii wema hata kidogo, kuliokoa hili taifa kutoka kwenye nini? Ikiwa Urais, ni demokrasia na kila mtu apendae anapiga kura. Sasa leo utuokoe kwenye nini? wengine tunaona siasa zako za maandamano na vurugu ni kututia kwenye janga na maafa, leo unaongea kutuokoa? Labda unachotaka ni kujiokoa mwenyewe (ambacho pia huwezi) kwa uchu wako wa madaraka lakini usituaminishe kuwa unataka "kuokoa taifa hili". Kikwete ndio "Chaguo la Mungu" na ndio chaguo letu tuliompigia kura, wewe rafiki inabidi ungoje 2015 (kama bado Mungu atakupa uhai, maana ni yeye tu muokoaji wetu sote) ujaribu tena bahati yako.

Kauli za mtu huashiria upeo wake, na hapa kwenye hizi kauli zako chache, na nyingi za uchochezi na siasa majitaka nilizokwisha zisikia, nasikitika sana kukuambia kuwa hufai kuwa kiongozi wa wote, labda baadhi tu ya Watanzania.

Utapoacha siasa za uchochezi na kuingia mitaani na kuanza kuingia Ikulu na kufanya kiukweli kuwa siasa sio "isolated case" kama maana ya neno siasa hapo ntakuona kuwa u mtu makini na unayeitakia mema nchi hii, kwa sasa na kwa kauli hizo tunataka tuone maandamano na kususa kuwa ni "isolated case" nakuona ni bado sana.
 
Wakati naandika, nilijitahidi kujiweka katikati na mwisho kabisa ndiyo nikaweka maoni yangu.

Bado sikutaka kujaiminisha kwa asilimia 100 kama wewe kwa sababu sikuwepo chunguni. Hapa duniani nimeshaanza kujiaminisha kuwa kama ukisikia mtu kafa na kazikwa na hukuona mwili wake akiwa maiti, basi usiwe na uhakika kuwa kweli kafa na kuzikwa.

Kususa kulikuwa na ubaya na uzuri wake. Ingelikuwa heri kama Siasa za Tanzania zisingeliruhusu tufikie huko kwenye kususiana na kugomeana/migomo na maandamano. Ila maadam tumefikia hapo, itakuwa makosa kusema kususa kubaya au kuzuri kwa asilimia 100 na nafikiri hata Dr. Slaa atakubaliana na mie.

Ila la muhimu ni kuangalia kwa asilimia ngapi kususa ni kubaya au kuzuri. Mie hapo ndiyo ninamalizia kwa kusema kususa kwa asilimia kubwa kumeleta mazuri. Kwa ufupi ndiyo hayo Sister Nyamizi alimalizia kwa kusema TUPO PAMOJA.

Tunakwenda sambamba mdau Sikonge, ni mada inayojadiliwa na hoja tutoazo kwa watu makini hufikia kwenye point ya kuafikiana katika jambo moja la msingi, asiyekubali kufikia majumuisho yenye kuhitimisha hoja ana tatizo.
Tumekubaliana katika hoja yetu. Thanks Sikonge

jk anajua power ya docta slaa
na ndo m2 pekee anae
isumbua ccm, 2endelee kumsapoti
docta slaa.
 
Waliposusa hawakuvuna chochote zaidi ya aibu na vifo kwa baadhi ya wafuasi wao, in the samw way walipokufa wafuasi wa CUF 2001 the diffence being namba of people killed!

Chadema hawajawi kukataliwa kuonana na rais kabla ya kususa kwao; kwa hiyo hakuna hoja yoyote kwamba wasingesusa wasingeweza kuonana na JK, JK haogopi wapinzani wa kisiasa ..he is above that..

Wanachotaka kwenye mchakato wa katiba wameshindwa kukitetea kwenye forum sahihi (bunge) hivyo kutunyima fursa adhimu sisi wananchi kufahamu hoja zao, in fact wameboa sana..

Wamepeleka mapendekezo yao kwa rais (yaliwekwa hapa JF) ni mapendekezo ya kijinga sana ambayo yanazungumzia NAFASI ya wajumbe wa chadema kwenye tume..inawezekana hilo ndilo wanachofuatilia kwasasa...

Kwa ufupi agenda ya chadema kuhusu katiba haiko wazi hasa wanataka nini, (hidden agenda); maana wangekuwa wawazi wangetumia bunge la jamhuri na kila mtu angewasikia; kuna haja ya kuwafuatilia walioko nyuma ya chadema wana interest zipi kwa taifa letu??
 
Ikiwa sera ya katiba mpya ni hoja basi CUF walikuwa nayo muda mrefu kabla ya magwanda hawajaifiria na hata rasimu waliitowa.

Tatizo ni pale unapolilia katiba mpya inapotekelezwa unasusa baada ya muda unaomba kwenda kunana na Rais, yote ni kutafuta sababu za kusema "si mnaona, tumetaka kuonana nae kakataa", lakini Kikwete ni makini na ana uzoefu wa diplomasi kuliko mwanachedema yeyote au hata wakijumuika pamoja. Kawazima utaaamu kabisa, sasa watacheza ngoma aitakayo yeye, wakipenda wasipende Kikwete ndio Rais wao na hawana mwingine wa kumlilia shida zao.
Ajira yako ni mashaka makubwa, upo kama daktari anayewakataza watu kuvuta bange na sigara kwa sababu ya madhara kiafya lakini yeye mwenyewe anavuta mtindo mmoja!
 
Ikiwa sera ya katiba mpya ni hoja basi CUF walikuwa nayo muda mrefu kabla ya magwanda hawajaifiria na hata rasimu waliitowa.

Tatizo ni pale unapolilia katiba mpya inapotekelezwa unasusa baada ya muda unaomba kwenda kunana na Rais, yote ni kutafuta sababu za kusema "si mnaona, tumetaka kuonana nae kakataa", lakini Kikwete ni makini na ana uzoefu wa diplomasi kuliko mwanachedema yeyote au hata wakijumuika pamoja. Kawazima utaaamu kabisa, sasa watacheza ngoma aitakayo yeye, wakipenda wasipende Kikwete ndio Rais wao na hawana mwingine wa kumlilia shida zao.

Inasikitisha sana kama chama kinachotawala kina lundo la wanachama na viongozi wenye upeo na mtazamo kama wa FF, ritz 1, ms, Rejao, wssira, kombani, na vilaza wengine wengi, basi umasikini utazidi kudidimiza hii nchi.
 
H ah ha ha h sio chadema waliosusa, hata sisi wananchi tusio cdm. By the way bado hatujui safari hii ni cdm au kikwete alimwalika mwenzake. Looser ni Jk tu na serikali yake maana uhai wa serikali ni watu na kama watu hawaitaki serikali unategemea nini. Majibu unayo

Kwani ni lini tutampindua jamaa?
 
H ah ha ha h sio chadema waliosusa, hata sisi wananchi tusio cdm. By the way bado hatujui safari hii ni cdm au kikwete alimwalika mwenzake. Looser ni Jk tu na serikali yake maana uhai wa serikali ni watu na kama watu hawaitaki serikali unategemea nini. Majibu unayo

Kwani ni lini tutamwondoa jamaa?!
 
Back
Top Bottom