Kumsusa Kikwete, CHADEMA wamevuna mahindi au Mabua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumsusa Kikwete, CHADEMA wamevuna mahindi au Mabua?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sikonge, Jan 22, 2012.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,489
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  By FaizaFoxy [​IMG]
  Kususa inkwisha? mlipoteza muda mrefu sana kwa siasa za kususa susa, naona mmejifunza kuwa kususa inatumika kuwa "disadvantage" kwenu.
  [​IMG]

  Nimekuwa najiuliza, hivi ukivamiwa na nchi fulani ya jirani au hata ya mbali, je kuna haja ya kusimama na kuitetea nchi yako? Hili swali ndiyo limenipa msukumo wa kuandika haya machache hapa.

  German ikiongozwa na Adolf Hitler, walianza mchakato wa kuzishambulia nchi za jirani na lengo hasa likiwa kujipanua kiuchumi. Walijizatiti kivita na walipokuwa tayari, walianza mchakamchaka wa kuzichukua nchi moja baada ya nyingine. Nchi nyingi kama Waholanzi, Wapolish, Wafaransa, Warusi waliwapinga na hiyo ikapelekea nchi hizo kupigwa vibaya sana na kuharibiwa.
  Mji kama Warsaw, waliuvunja zaidi ya asilimia 90. Russia walikuwa wakivunja kila kitu na kwa Moscow, Warusi waliamua na wao wenyewe kuuchoma mji wa Moscow na Wageruman walipokuwa wakifika, hawakuwa na maji, chakula wala sehemu ya kujisetiri.

  Vita kali sana ilipiganwa huko Volgograd (zamani ikiitwa Stalingrad - http://en.wikipedia.org/wiki/Battle_of_Stalingrad ) na vita ilipoisha, kulikuwa na uharibifu mkubwa sana. Katika matukio ya kusikitisha, ni kikosi cha Warusi, askari 10,000 ambao walipelekwa kushambulia Wageruman na wote wakafa. Mengine mtu unaweza kusoma mwenyewe kuhusu vita na hilo si muhimu hapa.

  Upande mwingine, kuna nchi ambazo wao walimkaribisha Hitler kwa mikono miwili ingawa kwa shigo upande na kumpa funguo na mji mkuu wao na hiyo ilipelekea nchi hizo zisipigwe hata risasi moja wakati wa vita ya pili ya dunia. Moja ya nchi hizo ni Czech na ukiona mji mkuu wao uitwao PRAGUE, utagundua tofauti yake na nchi nyingi. Pale kuna majengo ambayo mengine hata yana zaidi ya miaka 1,000. Old town ya Prague kwa ujumla ni kipande kizuri cha historia.

  Hapa swali langu ndiyo linaanza, je kulikuwa na haja ya nchi kumpinga Hitler? Je walifanikiwa nini zaidi ya kusababisha nchi zao kuharibiwa tu na silaha kali za Hitler? Je hao waliokubali nchi zao kuchukuliwa kirahisi, leo wamefaidika vipi?

  Nafikiri hapa jibu litategemea mtu umeamua kukalia kiti katika upande upi. Wengine wanaona kuwa nchi zilizomgomea Hitler, walao baada ya vita ya pili ya dunia, walianza kuipanga miji yao upya hasa ukichukulia kuwa, miaka ya zamani, mitaa ilikuwa myembamba sana na vitu kama mabomba ya maji, umeme, simu, gas nk ilikuwa kwenye mpangilio wa ovyo kutokana na mitaa kuwa myembamba sana na hatari kwa afya ya binadamu.
  Kwa wale waliokataa vita, wamebaki na historia yao na huku dunia nzima ikienda kuangalia jinsi zamani nchi za Ulaya zamani zilivyokuwa.

  Hata kwa Tanzania, kuna makabila yaliwakubali na kuwapokea Wakoloni bila upingamizi. Wanyamwezi, Wahehe, Wangoni, nk waliamua kula nao sahani moja na kufanya maisha ya jamaa kuwa magumu walau kwa siku za mwanzo. Hapa napo unarudi kwenye lilelile swali, je kulikuwa na haja ya kuwagomea na matokeo yake yakawa kifo cha Isike, Mkwawa, Kinjeketile Ngwale na wananchi wengi sana ambao kulikuwa hakuna haja/kulikuwa na haja?

  Tukirudi kwenye kesi yetu hapa ambayo imeumiza sana watu kichwa, Chadema kulikuwa na haja ya kumsusia (PROTEST) Kikwete pale Bungeni? Kulikuwa na haja ya Dr. Slaa kutokufika sehemu ya kuapishwa Kikwete pale uwanjani?

  Kwangu mie, miaka ya zamani ningelijibu kuwa ilikuwa ni ushamba wa hali ya juu. Utamsusiaje mtu ambaye kesho yake unaenda kwake kumuona? Hiii hali iliendelea kuwepo kichwani kwangu hadi wakati wa vita kati ya Iraq na Iran (Israel vs Palestine) ambapo kila wakati nilikuwa nashangaa jambo moja kuwa kila wakisema wiki lijalo, watakaa mezani kujadili kusimamisha vita, basi vita ilikuwa inazidi kuwa kali sana. Zinapigwa utafikiri wamesema mwisho wa dunia unakaribia.
  Nilimuuliza kaka yangu nini kinasababisha hii kitu na yeye akanijibu kwa kiingereza "Bargaining power at the mediation table."

  Sina uhakika kwa kiasi gani, Nguvu ya CHADEMA na Dr. Slaa kwa CCM na hata kwa IKULU kwa sasa imekuwa kiasi gani au kupungua kwa kitendo chao cha kumsusia Kikwete na tume yake ya Uchaguzi. Je kama wasingelifanya hivyo, CCM ambayo hata kwenye kampeni zao hawakuwa na ajenda ya katiba mpya, wangelianzisha mchakato huu?

  Labda kuna vijimaswali kadhaa inabidi kujiuza na haswa watu kama Lady FF (ingawa nafikiri atakuwa anafahamu hata zaidi yetu wengi humu ndani ya JF) kuwa, msuso wa CHADEMA, umeipa Bargaining Power kiasi gani hapa Tanzania against CCM/Ikulu/Serikali ya TZ?

  MAONI YANGU: Kuna dalili kubwa kuwa, kususa kwa CHADEMA kumeleta mchakato wa katiba mpya. Sidhani kama CCM wangelianzisha kitu kama hiki bila ya kusukumwa kutoka nje kama Newton's law of motion inavyosema "a body will remain at rest or will continue to move at a constant velocity, unless an external force is applied. "
  Ni mtu ambaye hafikiri sana na hajui au anajua ila anajifanya hajui (FF) ndiye atakuja na maelezo kuwa CCM wenyewe wameamua tu kubadilisha katiba na Rais mwenye kaamua tu kwa HURUMA yake kuonana na Chadema.

  AGAIN, remember "a body will remain at rest or will continue to move at a constant velocity, unless an external force is applied. " Ukiona VINAELEA, VIMEUNDWA.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,489
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  By Dr.W.Slaa [​IMG]
  WanaJF,

  Nawashukuru wote wanaofuatilia thread hii. Nawaomba kwa mara nyingine muwe na amani. Nawahakikishia hakuna wala hakutakuwa na usaliti. Chadema iko makini sana. Tunasukumwa na uzalendo na nia njema kwa Taifa letu.

  Aidha kama alivyosema MMJ, tumekuwa tukisukuma mabadiliko makubwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kabla Rais hajateua Tume ya kukusanya maoni. Tulieleza wazi kuwa vinginevyo hatutashiriki mchakato wa kukusanya maoni.

  Ni dhahiri busara ya kawaida inataka tupate progress ya majadiliano hayo hayo na utekelezaji wake. Katiba nzuri ndio afya na uhai wa Taifa hata kama si ufunguo wa matatizo yote yanayotusibu leo. Wakati mwafaka utakapofika tutatoa Taarifa kwa umma.

  Msiwe na hofu mtuamini.

   
 3. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 60
  H ah ha ha h sio chadema waliosusa, hata sisi wananchi tusio cdm. By the way bado hatujui safari hii ni cdm au kikwete alimwalika mwenzake. Looser ni Jk tu na serikali yake maana uhai wa serikali ni watu na kama watu hawaitaki serikali unategemea nini. Majibu unayo
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,799
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hivi ulivyompigia kura kikwete na ccm umevuna mahindi au mabua?
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,950
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 180
  Safari ni ndefu lazima tutafika. Dawa ni kumweka Jk kwapani
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Kwa mtazamo kwa haraka haraka ningefikiria na kutoa hitimisho kama mleta mada alivyofanya. Ila nikifanya upembuzi zaidi naona hatua zilizofanywa na Chadema zimezaa matunda mazuri hadi kufikia leo kukutana Ikulu kwa kile Kikwete kutekeleza Sera na Ilani ya Chadema.

  CCM haikuwa na ilani ya Katiba mpya, kwa vyo vyote hatua za Chadema zimemsumbua kichwa Kikwete hadi ndani ya siku 100 za mwanzo ambazo Chadema walipanga kufanya mchakacho wa Katiba mpya Rais Kikwete amelazimika kutekeleza.

  Kwa asiyejua mbinu za kisiasa anaweza kutoa hitimisho la jibu lako, ila kwa wapembuzi watajiuliza iweje CCM itekeleze ilani ya uchaguzi wa Chadema badala ya ilani yao ya CCM?
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chama cha kwanza kuwa na sera ya Katiba mpya ni CCM, CDM au CUF? Manake naona humu tunaongea bila kumbukumbu. Turejee Katiba za Vyama hivi ili tuwe sahihi pale tunapoamua kuongelea jambo fulani.
   
 8. M

  Makupa JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Cdm kususa wamejifunza kutoka cuf na mtaona baadae kitakachofuata baada ya hawa viongozi kukanyaga ikulu, kwani maalimu.Seif si alianzaje
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145

  Katika Uchaguzi Mkuu mwaka juzi CCM haikuwa na ilani ya Katiba mpya isipokuwa Chadema ulikuwa ni wimbo ulioshehehi Katiba mpya na hata walipomgomea Kikwete kule Dodoma madai yalikuwa ni kushinikiza upatikanajiwa Katiba mpya.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 12,966
  Likes Received: 889
  Trophy Points: 280
  Tuna safari ndefu sana ya kwenda. kama tukienda hivi, kuna watu wengi tutaachana nyuma tusijue cha kufanya. Bila uzalendo kazi ipo kubwa mbele yetu
   
 11. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Kususa ni njia mojawapo ya kujiexpress nadhani ata wewe uliepost kwa namna moja au nyingine unasusa anapokua na dissatsification ili kufikisha ujumbe....CDM hawakulupuki thas y ata jamaa wa magamba kasoma mchezo na kua mpole ili nchi itawalike.....so nampongeza JK na viongozi wa CDM kwani KJ akiacha ushambenga wa uCCM nadhani nchi itaenda sawa..jamani cku hizi kuna facial transp..... huyo jamaa nyuma ya JK ananitisha wakati wa picha wawe wanamtoa yani...........
   
 12. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,942
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  In any ways Kikwete anacheza kwenye parameters za CDM ambazo ni Katiba mpya haya mengine ya sijui wamekwenda ikulu sijui nani kamwalika mwingine nani kasusa hayana maana yeyote.
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,054
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  We are on the road towards political maturity!
   
 14. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,339
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  I cant wait to see my President Dr. Slaa akitinga magogoni na kuanza mara moja kazi ya kuwakamata wahujumi uchumi, kufilisi mali zao na kuwaseka lupango, pamoja na kufumua mikataba yote ya kipumbavu walioingia Magamba kwenye madini na ardhi ili kulinda hadhi ya Mtanzania
   
 15. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,095
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280

  you bet
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Swali lako ni irrelevant kwa situation ya sasa na hatua tuliyo fikia hakika .
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,489
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu, uwe unasoma makala kwanza basi kabla hujaanza kukurupuka. Anyway, uchaguzi uliopita wala kura sikupiga kwa sababu ambayo ipo nje ya uwezo wangu na hata kama ningelipiga wengi hapa wanajua ningelimchagua nani.
   
 18. N

  Nyamizi JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 1,376
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hebu rudia kumsoma vizuri mleta mada,unadhani ni kwa nini katolea mfano wa Newton's law of motion? Nadhani hujamwelewa vinginevyo naona kama uko pamoja nae.
   
 19. N

  Nyamizi JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 1,376
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hajui kama wewe ulikuwa ni mtu wa kwanza hapa JF kuweka signature yako ya kumuomba Dr.Slaa akubali kugombea Urais hata kabla ya CDM haijamteua?
   
 20. d

  dada jane JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera jk hongera cdm. Watakaowabeza wasameheni bure kwani wanatakiwa wakombolewe fikra zao.
   
Loading...