Kumsusa Kikwete, CHADEMA wamevuna mahindi au Mabua?

..wamevuna mahindi kwasababu nadhani kitendo kile ndicho kilichopelekea kuanzishwa kwa mchakato wa katiba mpya.

..hata kutoka bungeni wakati wa mjadala wa mswada wa katiba nadhani walifanya vizuri. Raisi asipowasiliza CDM na NCCR anaweza kusababisha katiba mpya ikaonekana ni katiba ya CCM badala ya Watanzania wote bila kujali itikadi zao.
 
Kwa mtazamo kwa haraka haraka ningefikiria na kutoa hitimisho kama mleta mada alivyofanya. Ila nikifanya upembuzi zaidi naona hatua zilizofanywa na Chadema zimezaa matunda mazuri hadi kufikia leo kukutana Ikulu kwa kile Kikwete kutekeleza Sera na Ilani ya Chadema.

CCM haikuwa na ilani ya Katiba mpya, kwa vyo vyote hatua za Chadema zimemsumbua kichwa Kikwete hadi ndani ya siku 100 za mwanzo ambazo Chadema walipanga kufanya mchakacho wa Katiba mpya Rais Kikwete amelazimika kutekeleza.

Kwa asiyejua mbinu za kisiasa anaweza kutoa hitimisho la jibu lako, ila kwa wapembuzi watajiuliza iweje CCM itekeleze ilani ya uchaguzi wa Chadema badala ya ilani yao ya CCM?

kumbe kuna muda una mawazo mazuri kweli ndugu yangu! big up sana
 
wamevuna mayai, si umesikia sasa marekebisho yaja? Hivi ulidhani Slaa angenda ikulu kunywa juice?
 
Back
Top Bottom