Kumshambulia Hayati Magufuli kunaweza ligawa Taifa na kupunguza nguvu ya CCM kanda ya Ziwa

Mimi naendelea kufurahia Magufuli kuitwa Fisadi, maana yake Magufuli akiitwa fisadi, basi serikari inayomfuata ifanye mambo meengi na makubwa kuliko aliyofanya Magufuli Kwa miaka yake mitano

Usambazaji umeme na bei chipa ya kuunganishia watu, ziwe Chini zaidi yake na umeme usambazwe Kwa Kasi kuliko yeye

Hospital na vituo Vya Afya, madawa na mikopo pamoja na kulipa Ada za shule msingi Hadi sekondari uongezwe kuliko yeye

Miradi kama SGR, bwawa la umeme, madaraja ya juu mfugale yawe karibu Kila jiji nchini, ndiyo, si alikuwa fisadi?? Mfanye makubwa kuliko yeye

Madege mlete angalau 50, viwanja Vya Ndege msivikarabati Tu, jengeni hata 20 hivi, stend za mabasi zienee Hadi tarafani huko

Maji vijijini, kero hii iishe na muende mbali zaidi Kwa kusambaza mabomba huko, Miradi ya maji kutoka Victoria fanyeni haraka Sana ufike Dodoma

Kwa kufanya makubwa zaidi kumshinda fisadi Magufuli kutathibitisha mkisemacho hapa, la sivyo utakuwa ni ujinga na upumbavu
Hivyo vyoote vitafanyika maana ni kutumia rasilimali za taifa tena zitafanyika Mara 2 zaidi.

Tunaye mama yetu hatuna wasiwasi
 
Unauliza kitu gani hapo??
Rejea CAG report kaka. Mifuko yote ya Wastahafu NSSSF na PSSSF imekauka Wazee wana stahafu hakuna mafao au malipo yao. Kisa? MAGUFULI KACHOTA HELA KUPELEKA SGR, BWAWA LA NYERERE, BOMBADIER, FLYOVERS, CHATO AIRPORT n.k.
Halafu jamaa alivokuwa hana AIBU utamsikia, " HII NCHI TAJIRI SANA INAWEZA KUWA DONA KANTRI...."The late JPM.
Jiwe alikuwa na balaa🤣
 
Sjajua huyu Magufuli alikuwa akitoa wapi Hizi pesa, maana zamani tuliaminishwa kwamba, pesa ni Hadi tupige magoti Kwa wazungu, ndio tufanye maendeleo,

Kwa kuwa yeye kafanya Kwa fujo na kujenga Jenga Miradi miingi Tu na Bado ameiba, basi nyinyi ambao kawachia mtaanzisha Miradi mikubwa na itajemgwa Ka Kasi kulikoni yeye,

Mkomesheni Kwa kujenga kila pahala viwanja Vya Ndege ili ijulikane Kweli alikuwa mpigaji
Hatuwezi kutumia pesa kipumbavu kujenga viwanja vya ndege wakati wananchi hawana dawa mahospitalini.huo upumbbavu uliwezekana kufanywa na mtu asiye na utu tu.
 
Kwani uraiani nako watu wanamchukia Magufuli kama ilivyo kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Twitter na Ufipa?

Bado naamini Rais Magufuli alikuwa anaungwa mkono na idadi kubwa ya watu walio wengi.

Na watu hao walituma ujumbe wao kipindi cha msiba wake.
Waliokuwa wanaomlilia huyu ni kundi la watu waliotamani matajiri wanakuwa level moja na masikini kwa jina lingine wanaitwa wanyonge.

 
Sjajua huyu Magufuli alikuwa akitoa wapi Hizi pesa, maana zamani tuliaminishwa kwamba, pesa ni Hadi tupige magoti Kwa wazungu, ndio tufanye maendeleo,

Kwa kuwa yeye kafanya Kwa fujo na kujenga Jenga Miradi miingi Tu na Bado ameiba, basi nyinyi ambao kawachia mtaanzisha Miradi mikubwa na itajemgwa Ka Kasi kulikoni yeye,

Mkomesheni Kwa kujenga kila pahala viwanja Vya Ndege ili ijulikane Kweli alikuwa mpigaji
Hatuwezi kupambana na marehemu lakini hatuwezi kuacha kusema upuuzi wa marehemu
 
Hatuwezi kutumia pesa kipumbavu kujenga viwanja vya ndege wakati wananchi hawana dawa mahospitalini.huo upumbbavu uliwezekana kufanywa na mtu asiye na utu tu.
Kwa hiyo wewe huduma za dawa ulizifuata Burundi??

Kumbe na wewe ni walewale Nyumbu?
 
Hatuwezi kupambana na marehemu lakini hatuwezi kuacha kusema upuuzi wa marehemu
Nyumbu mkubwa wewe, utahalalishaje ufisadi wake bila ya wewe kutoa huduma bora kulikoni yeye??

Utahalalishaje ufujaji wa fedha wake, Ikiwa wewe hutofanya mara tano yake,??

Ujinga mzigo
 
Nimemwangalia MB. Lusinde nimeona amejiweka katika wakati mgumu sana , muda wote alikuwa akisema Samia samia bila kutambua urais wa Mhe. Samia Suluhu huku akimuenzi Mh.magufuli kwa kutambua Urais kwa kutamka Rais Magufuli vilevile hakuishia hapo akamalizia kwa kumpongeza Bashiru na kusema mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni inamaanisha hajakubaliana na maamuzi ya Bashiru kupelekwa Bungeni.
Hivi Lusinde Class 7 naye ni MB kati ya Wabunge? Yule kwangu huwa namwona kama chizi fulani kapotea njia na kuingia Mlango wa Bunge!!!!
Lusinde ni wale walokuwa wanapongeza, kusifu, kutetea Jiwe aongezewe muda na mapambio kwa wingi kwa Mwendazake.....yule ni chizi perce!
 
Waliokuwa wanaomlilia huyu ni kundi la watu waliotamani matajiri wanakuwa level moja na masikini kwa jina lingine wanaitwa wanyonge.

Kwa hiyo wewe ni tajiri anayeshimda mitandaoni?? Mpuuzi mkubwa wewe
 
Hivi Lusinde Class 7 naye ni MB kati ya Wabunge? Yule kwangu huwa namwona kama chizi fulani kapotea njia na kuingia Mlango wa Bunge!!!!
Lusinde ni wale walokuwa wanapongeza, kusifu, kutetea Jiwe aongezewe muda na mapambio kwa wingi kwa Mwendazake.....yule ni chizi perce!
Kashindane naye umtoe bungeni, shida iko wapi, class 7 anakuwa bungeni halafu wewe msomi unakuwa unashinda mitandaoni Tu, Nani mjinga Kati yako na Lusinde ambaye yeye ni mbunge na wewe mtoa matusi mitandaoni??

Daaah!!
 
Nianze moja kwa moja kutoa maoni yangu kwa hali ya kisiasa nayoiona. Kifo cha Rais Magufuli imeacha pengo kubwa sana kwenye taifa. Kwa wale wasiopenda kusikia jina la magufuli niseme tu, Hayati alikuwa na wafuasi wengi kifo chake kimedhirisha hivyo na atakumbukwa siku zote kwa mambo mazuri aliyolifanyia taifa hili.

Niseme tu wazi si kila jambo alilolifanya hayati ni baya kwenye taifa hili. Ameacha alama kubwa sana. Licha ya kuwa na matatizo ya moyo alijitolea usiku na mchana kulipigania taifa lake.

Najua akili ni nywere na kila mtu ana zake. Watu wanaodai magufuli alikuwa fisadi unashindwa kuelewa jinsi walivyo na kumbukumbu ndogo ya aina ya ufisadi tuliyopitia kwenye taifa hili kabla ya magufuli kuingia madarakani. Kumbukeni ufisadi wa TEGETA ESCROW, EPA, BOMBA LA GAS MTWARA. Sote tunajua viongozi wa Afrika wakiiba pesa wanapeleka wapi. Wanakimbiza nchi za maghariba..kama Hayati aliiba hayo mabillioni yako wapi? Matrillion yako wapi?

Ameanzisha ujenzi wa reli kwa gharama ndogo sana uki compare na majirani zetu tena ya kutumia umeme.

Magufuli anatoka kanda yenye nguvu kiasiasa. Ukweli ni kwamba magufuli ameumiza sana watu wa kanda hiyo na taifa kwa jumla. Kitendo cha kuendelea kumshambulia kwa tuhuma ambazo watu wenye akili za kawaida kabisa wanajua zina malengo ya kisiasa nikutengeneza magawanyiko mkubwa huko mbeleni.

Kuna kitu magufuli kaacha kwenye mioyo ya watanzania. Nacho ni uzalendo. Wamejua kuhusu ukoloni mamboleo na jinsi baadhi ya viongozi wanavyotumika na nchi za magharibu kuhujumu mataifa yao either kwa ufisadi, mikataba mibovu etc.

Nimalizie kwa kusema, magufuli hakuwa malaika. Binafsi kuna mambo kadhaa niliyapinga kwenye utawala wake lakini niseme ni kiongozi mzalendo hili taifa kuwahi kupata.

Kama mnataka tuamini huo ufisadi mtueleze MAGUFULI KAFICHA HELA WAPI? Alizibeba kwenye sandarusi? Ana account ya pesa ulaya? MUNGU ATAMLIPA KIUMBE WAKE. KAKIKA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.

Mwisho kabisa kabla haujaendelea na mkakati ovu wa kumshambulia magufuli labda ujiulize. MAUAJI YA ALBINO YAKO WAPI? UFISADI MKUBWA UKO WAPI? UJAMBAZI UKO WAPI? KUKATIKA UMEME JE? AU TUMESAHAU JINSI MAJENERETA YALIVYOKUWA YANATUUMIZA MASIKIO?

Hakika MUNGU ATAMLIPA JPM kwa kutetea wanyonge na watu wasiokuwa na nguvu. Miaka 100 ijayo utakuwepo? Basi jifunze na beba mema ya hayati JPM mabaya muachie Mungu wake atamuhukumu.

Daudi alimwaga damu lakini Mungu alimkumbuka.
Unyonge alio kuwa anawasema watu ni udhalilishaji na ukandamizaji wa kifikra kuwadumaza watu ili aendelee kuwabinya. Uzalendo you upo alio iacha mioyoni mwa watu? Ni wasio waza kwa kina kama wewe unaediriki kutaja neno kama hilo. Magufuli hakuliunganisha taifa, aliligawa kikanda na kikabila. Ndio maana unadiriki kusema kanda ziwa wataumia. Alichofanikiwa ni kujenga taifa la waoga na wasioweza kuhoji. Miaka mitaani mbele angekuwa na taifa la mazezeta.
 
Kazi kukariri tu maneno!

Sukuma Gang ndo nini?
Maji ni uhai.
Screenshot_20210408-213742.jpg
 
Wasio mafisadi ndio mfanye haya maendeleo Kwa Kasi kubwa ili kudhihilisha ufisadi wa JPM, jengeni viwanja Vya Ndege kila Kona ili hoja yenu ya kumwita fisadi iwe Sawa!! La hamuwezi, basi mwacheni apumzike
Unajua shida sasa hasa siyo yeye mwenda zake, ila hawa aliowafundisha uovu. Wanataka kuendeleza uovu ule.
Wakimsikia kiongozi anyetangaza kuumiza watu wao hushangilia na kuona kama bwana wao kafufuka.


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom