Kumsamehe aliye kusaliti

Kumsamehe aliye kusaliti

Kumbe umesalitiwa,, OK ni hivi mwanaume anaposaliti mara nyingi huwa kasaliti kwa tamaa tu ila mwanamke anaposaliti mara nyingi husaliti kwa mapenzi yaani kamkubali aliyekusaliti nae kuliko wewe.. Ila dawa na adhabu tosha nikusamehe tu na kukaa kimya tena unaongeza kumjali ila usiongelee kilichotokea wengine hujiongeza na kusepa wenyewe kwakuhofia kunakitu kibaya unaplan
Sasa mkuu ukikaa kimya kwamba unakua humsemeshi au???
Maana kama mnaishi pamoja mtaishije kama mabubu mkuu??

Sasa mkuu kingne kama kamkubali zaidi hadi kakubali kusaliti kwanini asiseme mimi skutaki ili aende tu kwa jamaa aliyempenda ili wawe huru kabisa
 
Aiseeee Bro yangu moja ,, miaka ya nyuma kidogo , akitoka safari alimkuta mkewe na njemba kitandan.

Mbona aliishia kupiga mbwa risasi tu mbali na hasira na akamsamehe Demu wake ,mpaka Leo wako pamoja ..

Sema hili lishemu langu,
mwanangu ukiliona dooohhh ,lazima usisimuke mweeeee limejaaa balaaa ,paja pajaa sura sura ,jeupeeeeeeeeeeeee .

Kwa ufupi jibu LA swali lako linategemea mwenye Mali .
Kwahyo bado wako nae Paka sahivi mkuu?

Na Je vp bado anatania Ile Ile?
 
Hujui kule kapenda nini hata kama hazina unamiliki wewe atatafuta sababu umpe gawio aende kutumia na huyo mwenzako yapo tumeyaona
Daah kwel wanawake ni ngumu sana kuwaelewa wanataka nn
 
Mkuu kama umewekeza nae sana inakuaje Sasa
Fundi mzuri anajua kujenga na kubomoa.wengi wanaendelea kuwa watumwa kwa kuogopa kugawana.
Kama nimewekeza nae nachukua kianzio naanza kujenga upya.
Pesa inatafutwa na mafanikio yapo kwa mtu anayejitambua.
Unaachana nae unaenda kuanza upya
Hata kama kianzio hakipo unaweza kuanza na kufanikiwa
 
Kwahyo bado wako nae Paka sahivi mkuu?

Na Je vp bado anatania Ile Ile?
Yaap wako pamoja Mkuu namaisha yako muruaa ...( aiseee yule demu aisee kumwaacha ,alafu ukafikiria kidume mwingine ndo anayenda kula nibora ukae tuu ) .

Wako pamoja kabisaaa mpaka Leo.
Swali lako lapili sijalielewa Mkuu?.
 
Kama umeingia kwenye mahusiano naye sababu ni mzuri,hata ukimfumania utamsamehe sababu uzuri wake bado upo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu ni msomi ,hata ukimfumania utamsamehe sababu vyeti vyake bado vipo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu anapesa hata ukimfumania utamsamehe sababu pesa bado zipo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu mpo dini moja utamsamehe sababu bado mpo dini moja.

Kama umeingia kwenye mahusiano unatafuta wa kuishi naye hata ukimfumania utamsamehe sababu unachotaka ni MTU wa kuishi naye.

KAMA umeingia kwenye mahusiano unaamisi sio msaliti ,hutoweza kuendelea naye sababu ni msaliti.Na wewe hukuwa unatafuta msaliti.
he/she is not your choice
 
Kama umeingia kwenye mahusiano naye sababu ni mzuri,hata ukimfumania utamsamehe sababu uzuri wake bado upo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu ni msomi ,hata ukimfumania utamsamehe sababu vyeti vyake bado vipo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu anapesa hata ukimfumania utamsamehe sababu pesa bado zipo.

Kama umeingia kwenye mahusiano sababu mpo dini moja utamsamehe sababu bado mpo dini moja.

Kama umeingia kwenye mahusiano unatafuta wa kuishi naye hata ukimfumania utamsamehe sababu unachotaka ni MTU wa kuishi naye.

KAMA umeingia kwenye mahusiano unaamisi sio msaliti ,hutoweza kuendelea naye sababu ni msaliti.Na wewe hukuwa unatafuta msaliti.
he/she is not your choice
Daaah maneno kuntu na murua kabisa
 
Yaan bado Ana tabia Ile Ile ya kuchepuka
Hapana siku izi wako sawa nahamna kesi km izo tena .....mwanamke ukimfuma ,ukamsamehe daaahhh akirudia basi ujue huyo niwale ambazo wanatabia ya kutaste Uume tofauti tofauti....yaan yeye hapitiwi na shetani.
 
Jitoe akili tu hata kama una uhakika amekusaliti jiaminishe hawezi fanya hivo koz mnapendana..ukianza kuwaza hapa huwezi pata jibu..maumivu yake nayajua..move on
 
Habarini wana JF,

Hivi watu mlioko kwenye mahusiano ikitokea kakusaliti utamsamehe au utafanyaje? Na Je kuna watu ambao washawahi salitiwa na wakasamehe especially kama walikuwa wanawapenda sana wake zao?

Naombeni majibu wakuu
I see you with "psychological torture"....hilo no swali na maamuzi binafusi....mimi nakushauri kama utaweza kulisahau msamahe kama Huawei achana nae kila jambo liba mwisho...
 
I see you with "psychological torture"....hilo no swali na maamuzi binafusi....mimi nakushauri kama utaweza kulisahau msamahe kama Huawei achana nae kila jambo liba mwisho...
Sawa mkuu nmekuelewa na n kwel kabsa ni psychology torture hujakosea
 
Mimi huwa siangaiki natafutaga demu mwingne ili ajue kuna varieties.
NB
Hii ni wale wanawasaliti wapenz wao bila uoga na mweny Mali anajua... Kusaliti bila heshima.
WITO
Tuchepuke kwa akili mwenza wako hasijue mana maumivu yake n makali...
ONYO
Mapenz yanaua na yanasababisha shida nying sana maishani... Make sure unaposaliti kuwa makini ili kuepuka dhahama...
UZOEFU
muheshimu sana anayekujali kwa dhati ya moyo wake coz sio rahisi kupata watu wa namna hiyo...
 
Habarini wana JF,

Hivi watu mlioko kwenye mahusiano ikitokea kakusaliti utamsamehe au utafanyaje? Na Je kuna watu ambao washawahi salitiwa na wakasamehe especially kama walikuwa wanawapenda sana wake zao?

Naombeni majibu wakuu

Lazima ujifunze kusamehe kwasababu it is the right thing to do. Unasamehe kwa faida yako wewe sio kwa aliyekukosea. Unaposamehe unajiweka huru, unaondoa sumu moyoni ambayo yaweza kukudhuru siku za mbeleni. Usiposamehe maana yake unaweka visasi, majuto na hasira vitu ambavyo ni madhara kwa afya yako ya kimwili na kiakili. Usiposamehe, maana yake unaongeza tatizo kuwa kubwa wakati unaposamehe unaondoa uhasama na pia unatoa fursa kwako na kwa aliyekukosea kujifunza. Lakini muhimu zaidi hata ufanyeje, ulie, ulipize kisasi, umkomoe aliyekukosea HAIFUTI LILE KOSA LA MSINGI ALILOFANYA MWANZONI.

Kuna tofauti kati ya a) Kusamehe na b) Kuendelea na huyo aliyekukosea. Uamuzi ni wako unaweza kusamehe na kuamua kuendelea na uhusiano kama kawaida au unaweza kusamehe lakini ukaamua kusitisha uhusiano - nakusamehe lakini sitaweza kuendelea na uhusiano. Ni kosa kubwa sana kutosamehe kwasababu madhara yake ni makubwa hasa kwako wewe, maana yeye ameshafanya. Kwa kuwa unampenda mwenzako, hakuna atakayekuhukumu kwamba umesalitiwa na ukaamua kumsamehe mwenzako na kuendelea na maisha yako.

Ili uendelee na mahusiano ni muhimu kuzingatia kwamba aliyekukosea anaonekana kujutia na kutubu kosa lake, kwani unaweza kuamua kuendelea naye lakini yakatokea yale yale.

Kusamehe ni lazima kama unataka kuishi maisha marefu yenye afya
 
Habarini wana JF,

Hivi watu mlioko kwenye mahusiano ikitokea kakusaliti utamsamehe au utafanyaje? Na Je kuna watu ambao washawahi salitiwa na wakasamehe especially kama walikuwa wanawapenda sana wake zao?

Naombeni majibu wakuu
Rafiki ukweli ni huu, Mwanamke (mke) ni rafiki yako namba moja pale tu haujangundua kama kachepuka au amekusaliti lakini kama akikisaliti na ukajua kwa ushahidi au mkiachana akaenda masimbe huyo ni adui yako namba moja yaani hata akiomba msamaha huku anatoka machozi ya damu.... wengi wamesukumwa na upendo na kijifariji kuwa amebadilika lakini leo hii wamejutia na hawana sababu ya kuwaacha tena
Iko hivi mwanamke akikusaliti na ukagudua lakini akaomba msamaha na ukamsahe tena na kumrudia.. wewe utafanya kama hisani ila yeye atakuona mjinga wake kwa sababu amekusaliti na bado umemrudia anaona hauna pa kwenda
 
Ni kwel mkuu vp kwa mfano mwnamke akakussliti mara ya kwanza akakili na akaomba msamaha yakaisha alafu baada ya muda Tena karudia Yale Yale Tena vp unaweza msamehe

NB : bado anakujali na heshima iko pale pale yaan hajabadilika kitu
Mmmh... wewe endelea nae tu.
 
Mfano huyu mwnamke kadi za benk zake Zote kanpa mm yaan hata hela yake hajawah toa yy bank kila mwsho wa mwez natoa mm na Nina mjali kwa vyooooote ila ndo hvo sjui nn tatzo na Hua anaanza kulia akikutwa na kosa
Sasa mkuu kadi za benki za kwake ulizonazo na umiliki wa mapato yake ndio sababu inayokusumbua na kushindwa kutoa maamuzi au ni moyo wako na nafsi kutokana na kosa alilolitenda.Inaonekana upo interested na material things kuliko mapenzi na amani ndani ya ndoa yako. Inawezekana hii ikawa ni sababu kubwa ya mke wako kuchepuka,anakosa attention kutoka kwako. Sema na moyo wako kuhusu kumsamehe,je bado unampenda? Na mapenzi hayo uliyonayo kwake yataendelea kuwepo baada ya kumsamehe? Kama jibu ni ndio msamehe,kama ni hapana basi mwache aende kuepusha migogoro itakayotokea baada ya hili kujitokeza kati yenu. Acha kuwaza umiliki wa material things kwenye swala linalohusu hisia.
 
Back
Top Bottom