Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kwa unyenyekevu na heshma kubwa, naomba kuandika kwako ewe mheshimiwa amiri jeshi mkuu, mkuu wa Nchi na Serikali kiongozi wetu mpendwa Magufuli.
Ninachokiandika kwako Mheshimiwa Rais; haimaanishi kuwa najua kukuzidi muheshimiwa, au pengine mimi nina elimu sana, la hasha! Bali najaribu kuchangia kauelewa kangu kiduchu nilikonako kama mchango wangu kwa nchi yetu hii mheshmiwa Rais wangu.
Mheshimiwa Rais; Ili taasisi yeyote (ya umma au binafsi) iweze kufanikiwa, kuna kanuni za kitaalamu na pengine za kimaumbile zinazokubalika ulimwengu mzima ambazo ni lazima zifuatwe vinginevyo lazima taasisi itashindwa kufikia malengo yake, na najua nawe hili unalielewa vyema ila ni katika kukumbushana tu mheshimiwa rais wangu. Kanuni hizo zilikuwepo, zipo na zitakuwepo tu iwe tunapenda ama hatupendi, yaani ni sawa na ambavyo ni lazima binadamu ale ili aishi vinginevyo atakufa.
Mheshmiwa rais; Ili taasisi yeyote iweze kufanikiwa, ni lazima iwe na 1.maono (vision) 2. Mpango mkakati (strategic plan) na iufuate kikamilifu, 3. Rasilimali vitu/fedha na 4. Rasilimali watu. Mkuu sio kuwa nakufundisha maana najua tayari yote haya unayajua ila nakukumbusha tu maana najua una majukumu mengi na unaweza kusahau baadhi ya vitu.
Mheshimiwa Rais; naomba nikukumbushe kidogo kuhusu hili la "Rasilimali watu" kwa leo ambapo kwa mazingira haya nazungumzia "watumishi wa umma katika upana wake". Nimeona nilizungumzie hili kwa kuwa pengine ndilo eneo kubwa zaidi ambalo linaweza kuamua hatima ya taasisi yeyote ile, kwa muktadha huu; "Serikali yako tukufu".
Mheshimiwa Rais wetu mpendwa; Ili taasisi yeyote iweze kufanikiwa (Serikali yako adhimu kwa muktadha huu) ni lazima 1. iwe na Rasilimali watu/ Watumishi wenye uwezo mzuri na 2. Itumie mbinu za kitaalam na zinazokubalika kitaalam au kimaumbile (universally acceptable) za kuwafanya watumishi hao wafanye kazi kwa ari, juhudi na maarifa ili kuleta matokeo yanayolengwa na taasisi (kwa muktadha huu, malengo ya serikali yako mh.Rais).
Mheshimiwa Rais: ukiangalia tasisi zote duniani za umma au binafsi zilizofanikiwa sana, utagundua kwamba waliajiri watumishi wenye uwezo mzuri na kisha wakawekeza katika kutumia mbinu za kitaalam zinazowajenga watumishi ili watekeleze malengo na kuleta matunda yaliyokusudiwa na kinyume chake taasisi zilizoshindwa nasikuwekeza kwenye maeneo hayo. Najua mh.Rais wewe ni mtafiti na hilo unalijua vizuri sana.
Mheshmiwa Rais wetu; Kote ulimwenguni, wataalamu wa masuala ya kazi, ajira na mambo ya rasilimali watu kwa ujumla, wanakuballiana (kinadharia na kiutafiti) kuwa ili taasisi ifanikiwe, ni lazima wafanyakazi washughulikiwe katika namna ambayo inawatia hamasa na ili kuwatia hamasa ni lazima yafuatayo yawepo;-
Kuwe na hali ya Kukubalika (appreciation). Wafanyakazi huhamasika sana pale wanapofanya jambo jema bosi wao akaonesha “appreciation”. Kinyume chake hujikatia tama na kuamua bora liende.
Heshima “ be valued” wafanyakazi huhamasika wanapohisi kuwa wanadhaminiwa na kuna hali ya kuheshimiana na viongozi wao. Kinyume chake hukata tama na kujiona ni viumbe wasio na maana kwenye taasisi.
Kuaminika “be trusted” mfanyakazi akigundua kuwa bosi wake anamuamini, huhamasika kujitahidi zaidi ili kulinda uaminifu wake kwa bosi wake kinyume chake akiona haaminiki hata pale anapotunza uaminifu hukata tamaa.
Kushirikishwa kwenye maamuzi na kupewa majukumu; wafanyakazi hupenda kushirikishwa kwenye maamuzi kwa namna nzuri na kisha kupewa majukumu (kwa namna ya kuelekezwa zaidi kuliko kuagizwa), hali hiyo huwafanya kujihisi kwamba wao ni sehemu kamili ya maamuzi na majukumu wanayotekeleza hivyo kujituma haswa.
Mkuu mheshimiwa Rais wetu mpendwa; yako mengi, ila sipendi nikuchoshe zaidi hasa ukizingatia una majukumu mengine mengi na muhimu. Hata hivyo, nakushauri kuwa, kama ikikupendeza, inaweza kuwa na faida kama utayazingatia hayo hapo juu katika serikali yako tukufu kwani kwa kufanya hivyo, watumishi wa umma watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufanikisha malengo ya serikali yako tukufu katika upana wake na hivyo kuiletea nchi yetu matunda stahiki.
Mwisho nikuombe radhi mh. Rais wangu kwa kukuchukulia muda wako kusoma mambo yote haya.Yapo mengi lakini siwezi kuyazungumza yote kwa wakati mmoja. Kadhalika kama nitakuwa nimekuudhi au kukukosea kwa namna yeyote ile unisamehe kwani mimi ni mtu mnyonge sana nisiye na hili wala lile na nisiye na wakunitetea kama ukiamua kunifanya lolote.Nikutakie kila la heri katika majukumu yako.