kma ni kweli ulipost thred y kumtukan mhe.zito nkupongeza kwa uungwana wako wako wa kumuomba radhi kupitia jukwaa hilihili ulilomtumia,
''nchi yetu hivi sasa ipo taabuni shauri ya wajinga wachache wasioona mbali ni kweli yawezekana mitambo ile ni ya kifisadi lakini by that time we had no option lakini watu wakaona labda kama vile kuna watu fulani watamake kwelikweli,huo haukuwa uamuzi mzuri'',
inafsi ni mfuatiliaji mzyri wa television series ya kimarekani ya 24,kuna seasons zingine mfano season 3 au season 7 jack bauer analazimika kufanya mahusiano na magaidi just ili apate anachokitaka na kwa kwetu tulichokitaka ni nchi kuwa kwenye umeme ili shughuli za uzalishaji mali zisisimamae,leo hii nani anaweza kutueleza ni mamiliono mngapi yanapotea kutokana na viwanda au ofisi mbalimbali kuwa hazifanyi kazi?au ghrarama ambazo zinakuwa incurred kwa ajili ya majenereta?
BANIANI MBAYA LAKINI KIATU CHAKE DAWA
Nasisi tulioshimoni je? No Dowan even the sun. Better to stay as always
Mh Zitto, nianze kwa kukiri mimi nilikuwa miongoni mwa wana JF wengi tuliokuzonga kwa kejeri, shutma, kashfa na dhihaka kadha wa kadha kuhusiana na msimamo wako kwenye suala zima la ununuzi wa mitambo ya Dowans.
Mheshimiwa, ulikuwa sahihi kwa kusimamia kile unachoamini ni sahihi. Hii ndio sifa adimu ya kiongozi. Naamini hata wewe mwenyewe ulijua toka mwanzo kuwa uamuzi wako wa kutetea ununuzi wa mitambo ile hautakuwa popular na pengine ni kitanzi cha kisiasa. Lakini kwa ujasiri usiomithilika uliendelea kujenga hoja na wengi tulitia pamba masikioni mwetu na kukuita majina mabaya lukuki. Binafsi nilikwenda mbali zaidi na kukuita fisadi. Hili ndilo limenisukuma kuandika waraka huu mfupi ili kukuomba msamaha kwa maandishi yote machafu juu yako. Naamini tupo wengi wa aina hii lakini wenzangu wanakosa uthubutu wa kukiri na wanajichimbia kwenye keyboard zao.
Taifa leo lipo latika kiza, kwa sababu ya watu wachache waliokataa ushauri wa wataalam. Wale "wapiganaji" wanaona soni nyuso zimewashuka wanatapatapa kutafuta justification ya uamuzi wao mbovu ambao umeligharimu na utaendelea kuligharimu taifa kwa hasara kubwa.
Mheshimiwa watani zangu wazaramo wana msemo ufuatao "akutukanae kilabu cha pombe usisubiri kesho yake na wewe mrudishie matusi yake huko huko kilabu cha pombe" Kwa kuwa kashfa nilizitoa hapa JF nalazimika kuomba msamaha hapa hapa JF na ni matumaini yangu utanisamehe.
Nimalizie kwa kukiri na kusema kuwa Mh, wewe ni hazina ya taifa hili. Kama kiongozi vision yako ni kubwa kuliko umri wako. Pamoja na kuwa wanasiasa wanaepuka sana kujiingiza katika masuala tata kwa kuchelea kushusha credibility zao wewe umeweka utanzania wako mbele bila kuogopa kupoteza umaarufu wako wa kisiasa and spot on, you got it right.
Bravo Mh Zitto na endelea na misimamo yako thabithi yenye manufaa kwa taifa letu.
Mheshimiwa naomba kuwasilisha
DARK CITY LABDA TUBAKI WAWILI HATA MIMI NAKUUNGA MKONO ZITTO HAKUWA SAHIHI. hATUWEZI KUVUNJA SHERI A ZA MANUNUZI KWA KUNUNUA MITAMBO CHAKAVU. pIA KUNUNUA MITAMBO AMBAYO MUSTAKABALI WAKE MPAKA SASA HAUJULIKANI. kUNA SWALI LIMEULIZWA WATU WOOOTE WANAIKANA DOWANS, JE HELA HII ATALIPWA NANI? OFISIS ZAO ZIKO WAPI? KAMA NI CHAKAVU KWA NINI IUZWE BEI KARIBU MARA 2 YA KUAGIZA MIPYA.
MIMI KWANGU NI AFADHALI MGAO KULIKO KUNUNUA DOWANS
Mimi nafurahia angalau kuona kuna watu wako serious wanapotoa hoja, humu JF kuna watu wamejaa vidudu vichwani mwao kila wanapoandika wenzao huona ni utani, mara nyingi huua hata hoja ya msingi kabisa na kuendekeza madudu, hata wengine hujisifia eti wao hawaandiki ila ni watching dogs. Inakera kweli! Mimi nadhani ukitaka kuwa watching dog kaa kimya usibweke hovyo bila vina.
Leka
Naamini tupo wengi wa aina hii lakini wenzangu wanakosa uthubutu wa kukiri na wanajichimbia kwenye keyboard zao.
Taifa leo lipo latika kiza, kwa sababu ya watu wachache waliokataa ushauri wa wataalam.
wataalamu hawakushauri tununue mitambo ya wizi, walio toa uamuzi wa kununua mitambo ya wizi ni idrisa akisaidiwa na baadhi ya wapambe ambao wengine hatujajua nini ili kuwa interest yao. walicho sema wataalamu ni kununua mitambo in general, specific ilikuja kwa watawala au viongozi, ku-source hiyo mitambo ya wezi, ambao mpaka leo hii aliyekuwa analipwa hizo hela hatuambiwe, kwanini? kama hakuna kitu cha ajabu?
Mimi nafurahia angalau kuona kuna watu wako serious wanapotoa hoja, humu JF kuna watu wamejaa vidudu vichwani mwao kila wanapoandika wenzao huona ni utani, mara nyingi huua hata hoja ya msingi kabisa na kuendekeza madudu, hata wengine hujisifia eti wao hawaandiki ila ni watching dogs. Inakera kweli! Mimi nadhani ukitaka kuwa watching dog kaa kimya usibweke hovyo bila vina.
Kuna mambo mengine ni ya kiutani na hivyo wanaochangia nao wanachangia kiutani, labda kuwafanya watu wacheke kidogo na waendelee mbele kwa furaha. Lakini kuna mijitu inakatisha kila mahali na kukatisha tamaa mwendelezo wa uchangiaji, hivi kuna ugumu gani kutambua hoja nzito na hoja za vichekesho?
Nampongeza sana mtoa hoja MASATU kwa kujieleza bayana. Kwa kuwa ameona kuwa aliharibu na sasa anasafisha kupitia njia zilezile. Huo ndio uungwana. Nina hakika Zitto akisoma atamsamehe hapo hapo, kwani ni mwanasiasa anayejua anafanya nini, hata kama ni kijana kiumri, kakomaa kisiasa maana ameyapitia mawimbi hayo. ''Nilitegemea wengine wangejiunga kutambua mchango wa Masatu na kutubu kama na wao wameona. Sasa tuko gizani Tanzania, bado kuna watu wanachukulia utani japo Taifa linadhurika na giza hili. Nadhani kama kungekuwa na umoja wa kimawazo JF ingejengeka vizuri zaidi kuliko watu wanavyoyachukulia mambo yanapoletwa kujadiliwa''.
Wakati fulani niliona wanatanzanet fulani wakikandia sana JF kwamba hakuna jambo la maana. Kumbe ndio natambua kwamba mtu akisoma warukiaji watatu mfululizo wenye hoja zisizo na mwelekeo unaofanana na hoja ya msingi anaweza kishia majumuisho hayo. JF ina michango ya maana na tena mizito kweli, tena inasomwa na watu wengi wenye mamlaka na wanayafanyia kazi. Lakini virukia njia vikiharibu wanaweza vipi wenye dhamana kuchjumuisha mawazo yetu ili wafanye tunachowashauri kufanya?
Kama mtu hajui kubainisha hoja nzito na vichekesho, ni bora akae chini ajifunze kuandika, maana JF inahitaji hoza za watu wote zisomwe.
Leka
Wacha kucheza na maneno hapa, wataalamu walikuwa wazi kuwa mitambo ya kununuliwa ni ya Dowans simple kwa kuwa ndiyo iliyokuwa available.
Mbona unatufanya Watanzania sote hatuna maana ukiwapamoja na wewe kwa kusema kuwa mchezo huu wote ulikuwa wa mtu mmoja na kwa sababu ya mtu mmoja huyo si serikali na Rais wake, si Bunge na wapiganajiwake Si Jamiiforum ikiongozwa na August, walioweza kungamuwa ubaya wa huyu mtu na kutafuta njia mbadala na kuepukana na mgao.
Wacha Bwana! kama tulishindwa kwa kila hali na kamati ya Bunge ikithibitisha kuwa hatuwa zifaazo zimechukuliwa lakini tatizo bado lipo ni dhahiri kuwa wataalamu walikuwa sahihi na kama si hivyo basi kwa umoja wetu na tutafute suluhisho badala ya lililopendekezwa na Fisadi Rashid (kwa maoni yako, kwani mimi sioni kuwa alistahili lawama)
Hivi wale walio on the ground (whatever the hell that means) wanaamini kuwa tukinunua hiyo mitambo tnka kampuni e feki ya dowans ndiyo giza litatoweka TZ? Kama hii ndiyo imani basi tuna tatizo kubwa zaidi.
Mkuu pengine sijasoma post zako zote, ushauri wako ni nini katika wakati kama huu? we all know long term strategies, na zimesemwa tangu JK akiwa huko huko, tukarogwa akapewa urais.
Kuhusu Tanesco tunajua hamna kitu pale, unaweza ukamchukua mtoto wa darasa la nne akaongoza Tanesco.
However, Poor innocent people are dying out there what is the solution NOW!
Your contribution on this matter at hand will be greatly appreciated
Mkuu pengine sijasoma post zako zote, ushauri wako ni nini katika wakati kama huu? we all know long term strategies, na zimesemwa tangu JK akiwa huko huko, tukarogwa akapewa urais.
Kuhusu Tanesco tunajua hamna kitu pale, unaweza ukamchukua mtoto wa darasa la nne akaongoza Tanesco.
However, Poor innocent people are dying out there what is the solution NOW!
Your contribution on this matter at hand will be greatly appreciated
Mimi sitaki kukaa kimya, kwani nikikaa kimya hata hicho kidogo nilichonacho moyoni bila kuchangia nitakuwa sijajitendea haki wenzangu pia.
Mimi kwa upande wangu DOWANS sikubaliani nayo bora tukae gizani.