Kumpa mwanao jina la EX wako ni sawa?

Kumpa mwanao jina la EX wako ni sawa?

Nilufer

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
9,863
Reaction score
14,350
Habari zenu wana JF, hope mko wazima kabisa kwa uwezo wa muumba.

Leo nimepata kesi kutoka kwa rafiki yangu ambaye ni mjamzito. kama mnavyojua siku hizi, watoto majina wanapewa wakiwa bado tumboni. rafiki yangu na mume wake (ndoa yao bado ni changa sana) wameanza kushauriana kuhusu majina ya mtoto wao pindi atakapozaliwa. wameshachagua jina la kiume endapo mtoto atazaliwa wa kiume na wameshaafikiana.

Sasa ishu imekuwa ngumu kama mtoto atazaliwa wa kike, jamaa kapendekeza jina na kudai hilo jina ni la rafiki yake wa kike wa siku nyingi na anamuheshimu sana...sasa best angu kakataa kwa madai kwamba hilo jina litakuwa ni mojawapo wa wanawake zake na amedai hawezi kuruhusu mwanae apewe jina la hawala wa mume wake.

Sasa wapendwa naomba tujadili hapa je ni sahihi kumpa mwanao jina la ex wako? na je mwanamke ukigundua kwamba jina la mwanao ni jina la ex wa mumeo utajisikiaje na je wanaume ukigundua kwamba jina alilopewa mwanao ni jina la ex wa mkeo utafanyaje?
naomba kuwasilisha.



cc Munkari Chocs Malafyale Eiyer Excel Karucee Kaizer Ennie watu8 Heaven on Earth Lady doctor Mwanyasi valentine utafiti nameless girl mahondaw Daudi1 Dinazarde Zinduna na wengineo ............
 
Demba si vidhuli hata kidogo utasababisha mwanao achukiwe milele mwenza wako akigundua
 
Haaah! Sitaki kabisaaaaaaa huo mchezo x x tu alimuheshimu alifanyaje sitakiiiiii !! Majina kwenye bible yamejaa tele tena mazuri yenye baraka pia wazazi si wanamajina ?lah 2uunde yakwetu otherwise BIG NO !! kumpa mwanangu mjina wa x wake !!
 
Ukiacha kumchagulia mama bora upendo kwa mwanao pia unaoneshwa na jina bora unalompa! So chagueni majina mazuri kureflect future zao
Kwa wale ambao hawajaoa wawapenda wanao kabla hawajazaliwa kwa kuwachagulia mama/baba bora then watakapozaliwa wawape majina mazuri
 
Sidhani kama ni busara kumpa mtoto jina la ex wako maana hakuna siri ya milele,unaweza ukasababisha mtoto akapewa jina jipya akiwa na miaka 6!!
Ila waumini wa hili mara nyingi ni wanaume,sijui ni kwa nini wanafanya hivi! Nimeshuhudia mwanaume amempa jina la mkewe mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa na nyumba ndogo!!!
 
Haaah! Sitaki kabisaaaaaaa huo mchezo x x tu alimuheshimu alifanyaje sitakiiiiii !! Majina kwenye bible yamejaa tele tena mazuri yenye baraka pia wazazi si wanamajina ?lah 2uunde yakwetu otherwise BIG NO !! kumpa mwanangu mjina wa x wake !!

Nimependa hapo kwenye mjina tu!
 
Demba si vidhuli hata kidogo utasababisha mwanao achukiwe milele mwenza wako akigundua

ukimchukia mtoto utakuwa humtendei haki coz yeye alipewa tu tena alikuwa mdogo na haelewi kitu.
 
Asante kwa kunialika katika ukumbi huu,kwanza kabisa hata mkiwa na mpenzi wako kumtaja x tu ni dhambi kubwa sana sembuse kumpa mtoto jina la x,nakumbuka nilikuwa na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mpenzi wangu miaka ya nyuma tukiwa kunako dimba la chamazi ulimi ukateleza baada ya kunogewa na utamu nikamtaja x mihemko na utamu wote na baby zote ziliishia hapo mpaka nikajuta aisee maana yake inakuwa ni nini kwamba bado mapenzi yapo kwa yule wa mwanzo hakuna cha kumuheshimu wala nini jibu tena kwa herufi kubwa haifai na haipendeziiiiiiiii! over
 
Basi inabidi kuridhiana akizaliwa wa kike apewe jina na mama, akiwa wa kiume anapewa jina na baba ili kuepusha mambo hayo kutokea.
 
Haaah! Sitaki kabisaaaaaaa huo mchezo x x tu alimuheshimu alifanyaje sitakiiiiii !! Majina kwenye bible yamejaa tele tena mazuri yenye baraka pia wazazi si wanamajina ?lah 2uunde yakwetu otherwise BIG NO !! kumpa mwanangu mjina wa x wake !!
haa haa haa sasa best ukijagundua hivo mtoto ndio kashamaliza STD 7 utafanyaje, utambadilisha ama!!!
 
Shem kwanza asante kwa kuniita. Kumpa mtoto jina la X wako si busara sana na utaonyesha ni jinsi gani bado unamkumbuka na hutaki kumsahau, hapo si ndio migogoro inaanza?
 
Hakuna tatizo na hakuna hatua mbaya yoyote nitakayoifanya mbona kawaida tu
 
Sidhani ni sahihi maana ukimuita x wako it means bado yupo kwenye nafsi yako na inaonyesha ni jinsi gani hutaki kumtoa kwenye kumbukumbu zako
 
Haaah! Sitaki kabisaaaaaaa huo mchezo x x tu alimuheshimu alifanyaje sitakiiiiii !! Majina kwenye bible yamejaa tele tena mazuri yenye baraka pia wazazi si wanamajina ?lah 2uunde yakwetu otherwise BIG NO !! kumpa mwanangu mjina wa x wake !!

haa haa haa sasa best ukijagundua hivo mtoto ndio kashamaliza STD 7 utafanyaje, utambadilisha ama!!!
 
Bora tu amuite hata la bibi yakee lasivyo na tutawaita majina ya ma ex kibao!!!!!
 
Niseme tu kuwa huyo jamaa hana maana hata kidogo na wala haijui thamani ya mke ni ipi

Hivi unaonaje kuwa ni sawa kumuita mtoto uliezaa na mke wako mpenzi na unamuita jina la hawara?

Eti unamuheshimu,Nyambaf kama unamheshimu kwanini hukumuoa?

Hakuna heshima iliyo kuu kama kumuoa mwanamke unaempenda,sasa huyo jamaa analeta hadithi za kijinga hapa

Hebu niishie hapa nisije nikaharibu mazingira!
 
Asante kwa kunialika katika ukumbi huu,kwanza kabisa hata mkiwa na mpenzi wako kumtaja x tu ni dhambi kubwa sana sembuse kumpa mtoto jina la x,nakumbuka nilikuwa na mwanamke mmoja ambaye alikuwa mpenzi wangu miaka ya nyuma tukiwa kunako dimba la chamazi ulimi ukateleza baada ya kunogewa na utamu nikamtaja x mihemko na utamu wote na baby zote ziliishia hapo mpaka nikajuta aisee maana yake inakuwa ni nini kwamba bado mapenzi yapo kwa yule wa mwanzo hakuna cha kumuheshimu wala nini jibu tena kwa herufi kubwa haifai na haipendeziiiiiiiii! over

Mkuu hebu mrudishe Donie Yuen bana!!!!!!!!!!!!!

images
images
images
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom