Umasiki na Uchoyo ndo vinaisumbua hii mada! Kuna watu sio WACHOYOkama hela anayo anaitumia kuwafurahisha marafiki zake! Uwe demu wake usiwe demu wake hela yake unaila kama kawaida! WANAITA TREATING wenyewe! Mda mwingine unakuta mwanaume akiona mwanaume mwenziea ana hadhirika anamsaidia tu kibingwa! Out anaambiwa aje na demu wake, bills zote zinakuwa covered na wenzie kiutu uzima! Au kama hela anayo hata akiwakuta watu bar hawajui mkaongea arsenal hivi, man you hivi, mnaunganisha meza na kama mko na wanaume anazungusha, na wanaume mliokuja nao wanazungusha mpaka mnanawa! Akikuta wanawake tupu anawafanyia toa chupa weka chupa mpaka mnaomba poooh! Mtatafuna mbuzi mpaka mnasukumizia na funda la bia, Wala hawatongozi! Akichoka anaaga huyo! Hawa ndo watu wa MAANA! Hata mwanaume mwenzie akila hela yake haoni hasara! Kwake hasara roho tu, pesa karatasi!
Ila kuna wanaume WACHOYO hatariiii! Tena ukimlegezea atakupiga FREE P na kukukopa juu! Hawa unakuta hata wanaume wenzie wanamkimbia kwenye kutoka! Wanamjua MCHUNGU! We mtu hawezi kumpa mwanamke anaemkojolea hela ndo atanunulia washkaji bia asio wajua? Thubutuuuuu! HAWA WA KUKAA NAO MBALI KABISAA WANATHAMINI VIJICHENCHI KULIKO UTU!